DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Moses Matonya, amesema viongozi wa Tanzania wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha amani, umoja na mshikamano vinaendelea kudumu nchini, hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza Jumatatu, Oktoba 27, 2025, katika Kongamano la Amani la Kitaifa kuelekea Uchaguzi Mkuu linalofanyika jijini Dodoma, lenye kaulimbiu “Kupiga Kura ni Haki Yetu, Kulinda Amani ni Wajibu Wetu,” Mchungaji Matonya amesema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika kwa namna dini mbalimbali zinavyoshirikiana bila migawanyiko.
Aidha, amewakumbusha Watanzania kutotumia tamaa za madaraka au siasa kama sababu ya kugawa taifa, akisisitiza kwamba amani ni urithi muhimu unaopaswa kulindwa na kila mmoja.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi wa dini, wanasiasa na wadau wa amani kutoka mikoa mbalimbali nchini. Mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo.