Jehovah Shamah
Member
- Aug 29, 2016
- 18
- 10
Tanzania Kupaa kiuchumi na kuneemeka miaka ijayo.
Mchungaji Michael Nhonya, Katibu Mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania, amesema hana mashaka Tanzania KABISA kwani uchumi wa Taifa hili utapaa kuelekea uchumi wa kati na kufanana na mataifa mengine makubwa kiuchumi, kijamii, na hata kiroho duniani.
NHONYA amesema Uongozi wa Mh Rais John Joseph Pombe Magufuli. Umegusa kwenye maeneo MAKUBWA ya uzalishaji katika nchi yoyote duniani.
Miradi mikubwa kama vile:
1.Uzalishaji wa umeme wa Kizalendo wa mto Rufiji, utakaozalisha zaidi ya megawati 2115 ni chanzo Kikubwa cha kwanza kuwatoa Watanzania kwenye dimbwi la umasikini na giza.
Ukishakuwa na umeme wa uhakika tena wa kwetu wenyewe, unazalisha kila unachokitaka na kila mahali na kwa gharama nafuu.
2. MIUNDO MBINU YA USAFIRI:
Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa maarufu (standard gauge) ambao umeanza ni eneo lingine la kuzibua njia za mapato kwenye taifa hili.
Watu watakuwa matajiri ndani ya nchi hii miaka michache ijayo Kwani usafiri wa Reli utasafirisha mizigo mingi na wananchi wake kwa bei rahisi na kwa wingi na wakati mmoja.
Aidha Usafiri wa anga na Majini umepatiwa ufumbuzi. "Kufufua shirika la ndege ATCL na kununua ndege zaidi ya 7 kwa muda mfupi kwa fedha ya ndani ninaona MATUMAINI makubwa kwa Taifa langu." Amesema.
3. VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Hili ni eneo KUBWA la ajira kwa Watanzania, kaya nyingi zitapata chakula, maana Watanzania wengi wataajiliwa na kujiajiri.
Aidha Mchungaji Nhonya amsema NCHI IMENYOOKA!
Dhana ya Hapa kazi tu imenyosha watu. sasa hivi Watanzania wanachapa kazi sana. watumishi wa uma wanawajibika na tunashuhudia nidhamu, na ufisadi katika nchi umepungua kwa asilimia KUBWA.
Napenda kumpongeza Mh Rais John Joseph Pombe Magufuli na Serikali ya awamu ya Tano kwa KUCHAPA kazi! Na kwa kusimamia ndoto ilioanza taifa Baba wa taifa lakini ikazimwa na wingu la Ufisadi katika nchi. NAONA MWANGA!
Changamoto zipo, ikiwemo baadhi ya watumishi wa uma bado hawajaelewa ndoto ya Tanzania kuelekea uchumi wa Kati wataelewa siku moja.
Nawaomba Watanzania tutoe ushirikiano na kuwapa fursa watendaji wetu wa Serikali watekeleze wajibu na majukumu yao.
Ameitaka Serikali kuendelea kusimamia sheria, na utawala bora na amani ya taifa kwani hayo ndiyo misingi ya Uchumi wa nchi yoyote.