Mchumba wangu anahitajika kuolewa

Mchumba wangu anahitajika kuolewa

Mwambie huyo mchumba ako akope kwa baba ake then akupe hiyo hela ya mahali ukatoe kwa mzee wake tena
 
Wewe sio muoaji,muache mtoto wa watu aolewe kabla ajawa bibi!
 
Unaomva ushauri huku wakati kuna baadhi ya mambo unafanya siri, mimi nilitaka nikuchangie ila kwa mtindo huo, mmmmmh
 
Ni kweli inaonekana umechanganyikiwa maana hata uandishi wako unaakisi hilo,nafikiri sasa jitathmini na uamke kama mwanaume achana na mambo yakivulana,toka kwa wazazi wako kajitegemee,onyesha unahitaji kuoa kwa vitendo,acha kulialia na kudeka...
 
Sasa tunaanzia wapi kukushauri? By the way huyo ni demu wako na si mchumba ! Kwani tafsir ya mchumba ni yule ambaye tayar kuna taarifa na makubaliano pande zote mbili yaani KE & ME! lakini huyo waala si mchumba bado na siku si nyingi watakuja kubeba, utamlindaje huna hata silaha? (Furusi)
Ningekuwa mimi ningemuambia aolewe tu! Kwani hata mimi nishafanya hivo kwa wadada watatu, nakaa nae kisha tunashauriana na tunafikia hitimisho namruhusu aolewe
 
Mwambie avumilie mkuu, nawe weka jitihada kwa kiwango chako ili uweze kujitegema, hapo ukishapata hata chumba kimoja na vitu kidogo vya kuanzia sio mbaya vingine ni mbele kwa mbele, lakini kuishi nyumbani hiyo hapana, pia muombe Mungu akutoe hapo ulipo na upige hatua nyingine nzuri zaidi. MO11, amesema hapo juu, huyo hakupendi ila anakuonea huruma, inaweza kuwa ni kweli, na kama ni hivyo athari yake utaiona mara baada ya kumuo na kuwa ndani.

Ushauri wangu mkubwa, muombe Mungu zaidi juu ya huyo mchumba wako, atakupa majibu
 
ukose godoro, ukose chumba, ukose na mchumba? hata sikubali! kakope ofisini kwako fasta upeleke mahari.
 
Kwa presha hiyo angalie usije ukawa mtu wa "ndio mzee" kwenye hiyo ndoa.Kwanza kwanini wazee wawapangie kuoana mapema.Chunguza ujue kwanini wanataka ndoa ya haraka,wakati mwingne huyo Dada anaweza kuwa Bomu wanataka waliondoe mikononi mwao.
 
We nenda tu hata kama huna chochote...., ili mradi uwaonyeshe kuwa uko serious, na pia waone kuwa anaposema anaye anamaanisha anaye...........! USIPOENDA aisee
 
Mwambie huyo mchumba ako akope kwa baba ake then akupe hiyo hela ya mahali ukatoe kwa mzee wake tena

unanikumbusha novel ya "three suitors one husband" Juliette alivyoiba hela kwao na kumpelekea Oko
 
1-Umenza kazi lini?
2-una umri gani?
3-huyo mwenzio ana umri gani na anajishughulisha na nini?

Ushauri: Nenda huko kwao kajitambulishe wakufahamu uwaeleze msimamo na mipango yako juu ya binti yao. Kama kwa sasa muda wako wa kuoa haujafika na wakaridhika na msimamo na mipango yako juu ya binti wao hawatakulazimisha umuoe hadi utakapokuwa tayari maana mipango ya ndoa hupangwa na anayeoa!
 
hivi kuoa nako ni dharura kiasi kwamba muanze kuvutana mashati?

kikubwa dogo nenda kajitambulishe wakufahamu kwanza aafu waambie utatuma mshenga.
miezi miwili utakuwa umepata kalaki unatuma mshenga.
watajadiliana mahari aafu unawaambia mnajiandaa mtaenda.
 
Wakuu naombeni msaada wenu,

Nina mchumba wangu ambae ni mwaka sasa tangu tuanzishe mahusiano yetu, nimefikia muda wazazi wake wanapokea wanaume wanataka wamuoe mchumba wangu ila mchumba wangu amekataa katakata.

Amewaambia wazazi wake kua ameshampata mchumba ambae ni mimi sasa wazazi wake wanataka nikajitambulishe kwao then mimi kimaisha bado naishi kwa wazazi wangu na nina kibarua kwenye kampuni sina chumba sina godoro sina kitanda.

Sasa wazazi wake wamemwambia nikapeleke mahari sasa nimechanganyikiwa sijui nafanyaje juu ya swala hili na mchumba nimeshamwambia kua sina kitu chochote cha kuanzia maisha.

Wakuu msaada wenu

Mchumba wako ni wa kabila gn?
 
We nenda tu hata kama huna chochote...., ili mradi uwaonyeshe kuwa uko serious, na pia waone kuwa anaposema anaye anamaanisha anaye...........! USIPOENDA aisee

waweza fikia hatua ukajiua ee
 
waweza fikia hatua ukajiua ee

hapana..., hakuna haja ya kufika huko, siku hizi angalau maoni yao yanasikilizwa kidogo..., yeye akisema anaye afu wewe huonekekani watamsema, ukitokea kijasiri then hapo ndo utakuwa umewahakikishia....!

Gamila khaye gata daamit, kangok way
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom