Mchumba wangu anahitajika kuolewa

Mchumba wangu anahitajika kuolewa

docta sule

Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
42
Reaction score
6
Wakuu naombeni msaada wenu,

Nina mchumba wangu ambae ni mwaka sasa tangu tuanzishe mahusiano yetu, nimefikia muda wazazi wake wanapokea wanaume wanataka wamuoe mchumba wangu ila mchumba wangu amekataa katakata.

Amewaambia wazazi wake kua ameshampata mchumba ambae ni mimi sasa wazazi wake wanataka nikajitambulishe kwao then mimi kimaisha bado naishi kwa wazazi wangu na nina kibarua kwenye kampuni sina chumba sina godoro sina kitanda.

Sasa wazazi wake wamemwambia nikapeleke mahari sasa nimechanganyikiwa sijui nafanyaje juu ya swala hili na mchumba nimeshamwambia kua sina kitu chochote cha kuanzia maisha.

Wakuu msaada wenu
 
Mbona unalialia kwani umejipangaje ?
unataka msaada wa nini ?
wa hela au mawazo ?
kama hela humu hupati.

Huyo mwanamke sio kwamba anakupenda ila anakuonea huruma tu.
 
Mbona unalialia kwani umejipangaje ?
unataka msaada wa nini ?
wa hela au mawazo ?
kama hela humu hupati.

Huyo mwanamke sio kwamba anakupenda ila anakuonea huruma tu.

ckuhitaj hela mkuu ni msada wa mawazo tu ungetosha sana.so kunionea huruma kwake m kuna affect gan?
 
Huyo mchumba ako nae mchunguze, siku hizi hakuna mwanaume anayepeleka posa bila kukubaliana na mwanamke, asikudanganye kizamani bhana.

Pia kama unaona hujajipanga na yeye anataka kuolewa, usimpotezee muda mwache aolewe, hadi wewe ujipange utapata mwingine.

Pia huyo sio mchumba wako maana kwao hawakujui, sema mpenzi wako. uchumba ni hatua nyingine.
 
Thank you ma broo thank so much.godbless you
 
Pole sana. Wafahamishe wazazi wako kwanza, kisha waende kwa wakwe zako wafanye taratibu za wew kuoa. Maisha yatakubali tu kma tayari una kazi.
 
Pole sana. Wafahamishe wazazi wako kwanza, kisha waende kwa wakwe zako wafanye taratibu za wew kuoa. Maisha yatakubali tu kma tayari una kazi.

Wazaz nimewafahamisha tayar wamenambia kua nijipange kimaisha sa tatzo wazaz wa mwanamke wananihitaji
 
Waambie wazazi wako wakusaidie kama wewe unashindwa
 
waachie waoaji. jipange kwanza utapata mwingine.
 
1.Kibarua hakikulipi hivyo wewe binafsi hujiwezi unaongeza mtu mwingine kwenye hayo matatizo uliyonayo,Acha ujinga usitake kukimbia ungali kutembea hujui,jipange kwanza Ndio uanze starehe za wanawake

pole kwa kukurupuka
 
pole kwa kukurupuka

Si kukurupuka nyie Ndio mnaopotezea muda mabinti wa watu ni dhahiri huna uwezo wa kumuoa la sivyo utaomba michango hadi jf baada ya Hapo maisha ya shida binti anaanza kujuta unaanza kuchapiwa,usiruke stage jiweke sawa kwanza unaonekana bado hujapevuka kwa kitendo cha kuishi kwa wazazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom