Mchumba wa kweli huyu hapa.

Mchumba wa kweli huyu hapa.

malisoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Posts
1,860
Reaction score
2,639
siri ya kupata mchumba wa kweli ni yule mwanaume anayekupenda kwa dhati licha ya madhaifu uliyonaya ATAKUFAA.
 
siri ya kupata mchumba wa kweli ni yule mwanaume anayekupenda kwa dhati licha ya madhaifu uliyonaya ATAKUFAA.

Mimi nasema siri ya kumpata mchumba wa kweli ni kumjua mungu na wala si kufata mawazo ya wanadamu kila mtu anaibuka na lake akili yake inavyomtuma. Bila mungu hakuna lolote na hakuna njia ya mkato; watu wanazikwepa kweli za mungu na kuingiza mawazo yao binafsi ndio mana ndoa zote chini ya mbingu ziko juu ya mawe.
 
Kupenda kwa dhati ndiko kukoje? Kipimo ni kipi???
 
Mimi nasema siri ya kumpata mchumba wa kweli ni kumjua mungu na wala si kufata mawazo ya wanadamu kila mtu anaibuka na lake akili yake inavyomtuma. Bila mungu hakuna lolote na hakuna njia ya mkato; watu wanazikwepa kweli za mungu na kuingiza mawazo yao binafsi ndio mana ndoa zote chini ya mbingu ziko juu ya mawe.

Mungu kwanza

Kwahio wale ambao kwa bahati mbaya ndoa inaharibika au wenza wao wanawatenda hawamjui Mungu ?
 
siri ya kupata mchumba wa kweli ni yule mwanaume anayekupenda kwa dhati licha ya madhaifu uliyonaya ATAKUFAA.

Sidhani kama tatizo ni kujua yupi anayefaa bali jinsi ya kumpata / yupo wapi na yule aliyepo ni mkweli au muigizaji / msanii
 
Mapenzi ni two way traffic
Mwanamme akionesha mapenzi kwa msichana anategea hivyo hivyo kutoka kwa msichana ....akiona haoni mapenzi kutoka upande wa pili, huanza kupunguza mapenzi taratibu na pengine kwisha kabisa...na sio kwamba mwanamme anakaa na kuamua sasa aanze kupunguza mapenzi; inatokea tu yenyewe...naturally
 
siri ya kupata mchumba wa kweli ni yule mwanaume anayekupenda kwa dhati licha ya madhaifu uliyonaya ATAKUFAA.

watu hatutafuti wachumba, tunatafuta wake/waume, kama unapiga magoti kuomba mchumba pole,uchumba hautambuliki thats why kuna pingamizi la ndoa, sema siri ya kupata mume/mke wa kweli, edit hiyo thread uchumba ni hatua tu ila haina nafasi kubwa katika ndoa kwani wapo wengine hata hawajachumbiana, wanakwenda home wanakuta wameshaandaliwa wake/waume.
 
watu walipiga goti na wakalamba garasa,mie am begining to question if theres God,and if he is there...he is fair????:shut-mouth::A S 11:
 
Mungu baba mwenye huruma na upendo, usie lipa kisasi kwa wanao Baba wa Mbinguni; mimi nilie maskini na kuishi maisha ya ufirauni mokozi mpendwa naomba kwa ukarimu na dhamira ile ya kumtoa mwanao mpendwa pale msalabani unipe MKE mwema eh Baba wa mbinguni. Tazama yote nimeyajaribu lakini sasa nasema wewe baba watosha mengine yote ni ubatili mtupu na kujilisha upepo. Amen
 
Je wewe ni mwema? kama ndivyo, hakuna haja ya kuomba atakuja wa kufanana na wewe
 
Kwahio wale ambao kwa bahati mbaya ndoa inaharibika au wenza wao wanawatenda hawamjui Mungu ?

Unaongea JIBU. Ukiwa na mungu na umeyashika maagizo yake juu ya namna ya kuenenda katika maisha haya hakuna baya lolote linaloweza kukupata.Wewe ni sumaku na unavuta yale yanayofanana na wewe mwenyewe ulivyo, kwamba ni mwovu uovu utakuandama na kwamba ni mwema wema tele utakuijilia juu yako. Mtu huvuna alichopanda na atendwaye kuna mahali na yeye alimtenda mtu. Malipo ni hapa hapa duniani na mbinguni baadaye
 
Je wewe ni mwema? kama ndivyo, hakuna haja ya kuomba atakuja wa kufanana na wewe

Umesema kweli kabisa kwa kuwa binadamu ni sumaku na huvuta kile kinachofanana na yeye mwenyewe, kwamba ni mwovu, atavuta mchumba mwovu, na ya kwamba ni mwema atavuta mchumba mwema. Yani mahesabu ni rahisi kabisa namna hiyo, huwezi kuuandama uovu halafu ukakesha unaomba ukataraji kuvuna lolote.
 
watu walipiga goti na wakalamba garasa,mie am begining to question if theres God,and if he is there...he is fair????:shut-mouth::A S 11:

Ndugu yangu ni nani huyo kakuloga huamini tena kwamba mungu yupo? maombi sio goti peke yake ni pamoja na matendo yako kwa kuwa imeandikwa wawili wakikubaliana jambo chini ya mbingu baba yangu aliyeko mbinguni atalifanya. Wawili hawa wanaokubaliana ni nani? maombi yako na matendo yako. Kulivyo ndani, kulivyo nje. Nje kuna maombi ya goti lakini ndani nafsini mwako kumejaa uchafu usioendana na maombi yako. Unataka upate mke mwema lakini unatembea na wasichana kila anayepita. Unataka upandishwe cheo lakini unamwibia mwajiri. Wawili hao hawapatani na mungu hawezi kutenda; unapoomba lazima uchukue hatua kwa kuwa maombi ya goti kama yalivyo sio hatima ya kila kitu.
 
Unaongea JIBU. Ukiwa na mungu na umeyashika maagizo yake juu ya namna ya kuenenda katika maisha haya hakuna baya lolote linaloweza kukupata.Wewe ni sumaku na unavuta yale yanayofanana na wewe mwenyewe ulivyo, kwamba ni mwovu uovu utakuandama na kwamba ni mwema wema tele utakuijilia juu yako. Mtu huvuna alichopanda na atendwaye kuna mahali na yeye alimtenda mtu. Malipo ni hapa hapa duniani na mbinguni baadaye

Na wale watoto wanaobakwa au kuwa abused ni sumaku na wenyewe ni wabaya ndio maana ubaya unawafika ?, waliokumbwa na Tsunami je ?, au vitoto vichanga vinavyozaliwa na wazazi wao kutoweka ?, au wazazi wazembe wanaozaa watoto na kuwatupa hao watoto ni sumaku ?

Mkuu wangu acha kuwa na imani hadi inakupofusha unakuwa kipofu (kama unaamini Mungu alikupa akili na busara, basi tumia akili yako na busara zako kuruka viunzi na kufanya maamuzi bora) sio kusingizia ni mipango ya Mungu pindi mambo yakienda kombo.., na kila anayekumbwa na baya sio kwamba amefanya kosa.
 
Back
Top Bottom