Caroline Danzi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2008
- 3,713
- 1,269
Yaani umeshindwa kum-face ukamweleza tabia ambazo huzifurahii na ukamshauri abadilike unakuja kushtaki jf! Halafu unajisifu we mkali.
hizo ni dalili mbaya sana...atabadilika kusave mahusiano then later atakuja na hari na kasi mpya,nyumba itakuwa uwanja wa vita...binafsi mdada akileta dharau tu hata kam nimemtambulisha namdelete
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.
Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa
Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.
1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.
2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.
Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?
Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.
Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!
Ushauri
Afu anasema anapika akiwa kwenye mood???? Huyu si mchafu na mvivu tu ila ni mjeuri...mimi ninawajua watu wa hivyo kaka kaa chonjo.
mwanamke mvivu aisee sikushauri sana
for those married man like me sitegemei eti mwanamke awe mvivu
tunasaidiana ndio lakini kama hajui wajibu wake kama mama nyumba itakuwa sio nyumba
utakuja kujuta sana mbele ya safari, ndio huyo hata mtoto akijisaidia atamwacha au amwite housegal ambadilishe
atafanya chumba chenu kunuka,she will not bother.
my wife nakiri ni msomi kuliko mimi ana kazi nzuri zaidi yangu lakini sio mvivu
tunasaidiana sana lakini kuna vitu anapenda kufanya mwenyewe yeye kama mama
kaa nae chini mjadiliane ukiona habadiliki amua kivingine mapema
NDOA HAIJARIBIWI USITEGEMEE ATABADILIKA KAMA HAJABADILIKA SASA.
Mkuu Tigga Mumba toa ajira kwa House girl / boy atafanyakazi zote mwache mke mtarajiwa ajipumzishe kazi yake kubwa ni kukuzalia watoto na kukuliwaza.
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.
Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa
Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.
1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.
2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.
Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?
Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.
Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!
Ushauri
Mkuu Tigga Mumba toa ajira kwa House girl / boy atafanyakazi zote mwache mke mtarajiwa ajipumzishe kazi yake kubwa ni kukuzalia watoto na kukuliwaza.
Afu anasema anapika akiwa kwenye mood???? Huyu si mchafu na mvivu tu ila ni mjeuri...mimi ninawajua watu wa hivyo kaka kaa chonjo.
Ni kweli. Je kuna namna unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya usafi/kupika?