Eti wana mmu,hili limekaaje ?
Kijana katika harakati zake za kutafuta jiko ama ubavu wake wa kushoto,anajikuta amepata sehemu ambapo karibu vigezo vyote mtoto wa kike anavyo.
Wakiwa wanaendelea kupanga na kupangua baadhi ya mambo kuelekea ktk ndoa.
Kijana anaanza kuambiwa na mchumba kuwa.... mie nakupenda sana ndio maana nimewakataa wachumba wengi sana,miongoni mwao ni yule tajiri, na jana tu alikuja nyumbani na gari akaniomba tukakae hotel fulani,tulienda akaniambia kuwa anataka anioe mie nikakataa nilimwambia ninae mchumba ambae ni wewe.
Mwingine ni John yeye nae ananitaka hata hii gari niliyonayo ni yeye alinipa kama zawadi tu,nae pia huwa ananitongoza lakini mie simtaki nakutaka wewe.
Wapo wanaume wengi wenye hela zao wananitaka kunioa.
Na kuna kuna mwingine anaitwa...aliwahi kuniita kwake eti alikuwa na shida muhimu,nilipofika kwake akaniambia anataka anioe mie nikakataa akaamua kunibaka.
Unamfahamu yule jirani yetu mwenye duka??! Yule nae aliwahi kunibaka na kunitoa usichana wangu hii ni baada ya kumkataa.
Kama wewe ndo huyo kijana utafanya nini?