Mchumba anakuambia anakupenda sana ndio maana.....

Slave

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
5,315
2,634
Eti wana mmu,hili limekaaje ?

Kijana katika harakati zake za kutafuta jiko ama ubavu wake wa kushoto,anajikuta amepata sehemu ambapo karibu vigezo vyote mtoto wa kike anavyo.

Wakiwa wanaendelea kupanga na kupangua baadhi ya mambo kuelekea ktk ndoa.

Kijana anaanza kuambiwa na mchumba kuwa.... mie nakupenda sana ndio maana nimewakataa wachumba wengi sana,miongoni mwao ni yule tajiri, na jana tu alikuja nyumbani na gari akaniomba tukakae hotel fulani,tulienda akaniambia kuwa anataka anioe mie nikakataa nilimwambia ninae mchumba ambae ni wewe.

Mwingine ni John yeye nae ananitaka hata hii gari niliyonayo ni yeye alinipa kama zawadi tu,nae pia huwa ananitongoza lakini mie simtaki nakutaka wewe.

Wapo wanaume wengi wenye hela zao wananitaka kunioa.

Na kuna kuna mwingine anaitwa...aliwahi kuniita kwake eti alikuwa na shida muhimu,nilipofika kwake akaniambia anataka anioe mie nikakataa akaamua kunibaka.

Unamfahamu yule jirani yetu mwenye duka??! Yule nae aliwahi kunibaka na kunitoa usichana wangu hii ni baada ya kumkataa.

Kama wewe ndo huyo kijana utafanya nini?
 
kwa mimi baada ya hapo naomba nami niitoe bikra ya tingho!
Unaonaje hapo mdau...si ngoma droo?
 
Mie yashanikuta hzo habari za kua flani ananitaka mara ooh watu wenye pesa wananitaka..aliponambia hvyo nikamuacha papo hapo..ili akaolewe na hao wenye pesa na magari......
 
Kweli wewe ni slave wa mapenzi. Bado uko na huyo changudoa?? Jamani mkizaa watoto au kuchagua ID muwe makini. Mtu anamwita mtoto Shida, Tatizo, vumilia n.k. Mwishowe wanaishi maisha hayo hayo.
 
Hakuna "Mke Mtarajiwa" anayekupenda na mwenye akili timamu anayeweza kukwambia maneno kama hayo, labda awe ameathirika kisaikolojia na hivyo vitendo vya kubakwa kila wakati. Vinginevyo, hayo maneno yana maana ya "wewe siyo type yangu".
 
Hapa sasa naona lazima ni script za bongo movie umeziiba ukatuletea huku,hizi peleka kule kwenye comedy.
 
Jamii ndo hii hii, kila binaadamu anayo mapungufu yake,wengi huficha mapungufu yao na yanapo jitokeza kwa kasi hutafsiliwa kama wehu ama wanatatizo la kisaikorijia. Nilicho jifunza ni kwamba inawezekana mwanamke anatabia mbaya that why anamuandaa mwenzie kwa kumpa ukweli iliasije shangaa huko mbele ya safari.lakini pia inaweza ikawa ni mbinu ya mdada kumpa vitisho mume iliasijisahau na kujiona yupo pekeyake na kumfanya mume achapulishe mambo
 
Huyo hata hauhitaji ushauri, hamtofika mbali maana hadi kumleta JF inaonekananashakuboa tyr
 
kwani ulikuwa unajifunza kuandika scripts au vipi maana kwa hali hii hata sanaa huiwezi kalime matikiti
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!! Yamenikuta saaaaana hayo aiseee naona ndo gia zao ili ujue kuwa anapendwa sana na watu weny nazo na lengo lake anakutia hamasa ili umuweke ndan faster
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom