Mchochezi ni mtu wa aina gani?

Mchochezi ni mtu wa aina gani?

verykeys

Senior Member
Joined
Mar 29, 2016
Posts
155
Reaction score
90
Natamani kujua mchochezi kwenye nchi yangu ni mtu wa aina gani.

Wakiongea wengine ni wachochezi ila akisema yeye tusiwasikilize hao ila tumuunge yeye tu mkono hiyo sio mchochezi. Mtu mwingine akisema hali halisi iliyo nchini ni mchochezi, akisema yeye hali halisi iliyo nchini sio mchochezi.

Wapinzani wakismamishwa na wananchi watoe japo neno wanakamatwa kwa sababu wanakusudia shughuli za uchochezi, ila akisimamishwa yeye na kuongea atakavyo sio mchochezi. Ukikosoa ni kumdhalilisha na uchochezi ila akikosoa yeye ni msema kweli wa mungu.

Najaribu kuwaza sana ila nakosa majibu ya busara kwenye kichwa changu.

Serikali yangu ipo kwenye vita na matajiri na wezi. hadi hapo akili yangu inaniambia nipo salama mana mimi sio tajiri wala mwizi. Najaribu kutafuta kundi langu ili nijue hali hii ngumu inayonigusa kwan napigana na serikali kupitia kundi gani au mm ni adui wa serikali kupitia kundi gani.

Au labda na mm ni mchochezi?

Naombeni jibu wananchi hivi mchochezi ni mtu wa aina gani?
 
Hata mtoto nyumbani akihoji "baba mbona Jana ulichelewa kurudi home" hata kama ni kweli huyo ni mchochezi anasabanisha uvunjifu wa amani nyumbani, ni lazima nimshughulikie, anahoji yeye ni nani? Yeye ni mtoto tu asubiri akiwa na mji wake akafanyie kwake, mbafu
 
Mchochez ni mgonjwa anayekimbilia Nairobi na muhimbili ipo
kama ni hivyo basi hata wanafunzi wanaoenda shule za private na wamechaguliwa shule za serikali ni wachochezi. au unaonaje na hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom