Ushimen
Platinum Member
- Oct 24, 2012
- 43,997
- 110,403
Maafisa wa usalama wa Tanzania walimkamata, wakamhoji, wakamweka ndani na kesho yake wakampakia kwenye ndege na kumrudisha kwao Uingereza kupitia Uholanzi.
Jihadi John aka Mohammed Emwazi alizaliwa Kuwait mwaka 1988 kabla ya kuhamia Uingereza akiwa na umri wa 6. Ana shahada ya kompyta kutoka chuo kikuu cha Westminster.
Jihadi John hakuwahi kushtakiwa kwa makosa yoyote ya ugaidi. Alitaka kuingia Tanzania baada ya mahafali yake ya chuo. Taarifa nyingine zinadai kuwa alitaka kuingia Tanzania kwa ajili ya safari ya mapumziko.
Hata hivyo, alianza kuingia kwenye rada za maafisa wa usalama wa Uingereza kati ya mwaka 2009 na 2010 wakati wakifanya uchunguzi wa Waingereza waliokuwa wanajiunga na wapiganaji wa al-Shabab.
Jihadi John alitaka kuingia Tanzania kwa jina la Muhammad ibn Muazzam. Alikuwa anasafiri na Mwingereza mwingine kwa jina Abu Talib na mwingine Mjerumani aliyeitwa Omar.
Baada ya kuhojiwa na vyombo vya usalama vya Tanzania, Jihadi John aliiambia Cage, ambayo ni taasisi iliyoko London inayotetea haki za watu wanaonyanyaswa na vyombo vya usalama, kuwa walinyanyaswa na kudhalilishwa na maafisa wa usalama.
Kwa mujibu wa Cage, aliporudishwa, Jihadi John alihojiwa na vyombo vya usalama vya Uholanzi na Uingereza. Inaonekana baada ya hapo walimwacha kurudi Uingereza.
Kuwait kuishi na ndugu wa baba yake na pia kuanza maisha mapya Mashariki ya Kati. Alipata kazi nzuri kwenye fani aliyosomea na akawa na mipango ya kuoa na kuishi Kuwait.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa mwaka 2010 alikataliwa kwenda Kuwait baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa masaa sita katika uwanja wa ndege wa kimataifa Heathrow ulioko London.
Akiwa mahabusu, alidai kuwa alinyanyaswa na afisa mmoja wa usalama. Kwa mujibu wa Cage, hii ndiyo ilimfanya Jihadi John abadilishe mkondo wake wa maisha. Kabla ya hapo alikuwa amepanga kumwoa mchumba wake nchini Kuwait na alikuwa ameenda London kumalizia mipango ya ndoa.
Cage inadai kuwa Jihadi John alikuwa ana hasira kuondoka Uingereza na mwaka 2013 alibadilisha jina na kuitwa Mohammed al-Ayan.
Jihadi John alikuwa akiishi kwenye gorofa huko Queens Park, London Magharibi
Baada ya kubadilisha jina alijaribu tena kwenda Kuwait lakini alizuiliwa tena na vyombo vya usalama vya Uingereza. Mwezi Agosti, wazazi wake walimripoti kupotea, na miezi minne baadae inadaiwa polisi waliiambia familia yake kuwa alikuwa Syria, japokuwa familia yake walidhani alikuwa anafanya kazi ya kujitolea Uturuki.
Haijulikani alienda Syria lini lakini mwaka huo huo iliripotiwa kuwa alikuwa Idlib akisaidia kulinda mateka wa nchi za Ulaya.
Agosti 2014 alionekana kwenye video inayoonyesha mauaji ya mwandishi wa habari raia wa Marekani, James Foley. Miezi iliyofuata alionekana kwenye video za mauaji ya Steve Sotloff, David Haines na Alan Henning japokuwa haijulikani kama ni yeye aliwauwa.
Lakini Novemba 2014, Jihadi John alionekana kwenye video moja akihusika kumwua mwanajeshi wa Syria. Pia alisimama juu ya kichwa cha Mmarekani Peter Abdulrahman Kassig. Miezi miwili baadae alitokea tena kwenye video nyingine ambapo alimwua mateka wa Kijapani, Kenji Goto.