BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,331
Imeandikwa na Na Maulid Ahmed;
Tarehe: 8th July 2010
Habari Leo
MBOGA za majani, ukiwemo mchicha, zinazolimwa kwa kumwagiliwa maji ya Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam,si salama kwa matumizi ya binadamu na wanaotumia wana hatari ya kupata saratani na kuathirika mfumo wa akili.
Mboga hizo; mchicha, matembele, kabichi na spinachi zimekutwa na madini ya risasi, shaba na kromiamu, ambazo kwa miaka kadhaa baadaye zinaweza kumsababishia mlaji magonjwa, ukiwamo utendaji mbovu wa figo.
Madhara hayo yalibainishwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU), kilichofanya utafiti katika bonde la Mto Msimbazi wilayani Ilala, mwaka jana, kwa kupima maji kwa vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS); udongo na mboga zenyewe.
Akizungumzia utafiti huo katika Maonesho ya 34 ya Biashara ya Kimataifa yaliyomalizika jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, Mhadhiri wa Uhandisi wa Mazingira, Dk. William Mwegoha, alisema waligundua mabwawa ya majitaka yanayotoka Mabibo, dampo la Vingunguti na gereji mbalimbali yakimwaga maji kwenye mto huo.
Baada ya kupima maji hayo, tulikuta yana madini ya shaba, risasi, kromiamu na ladimiamu na ni sumu, alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kupima pia mboga hizo za majani zilikutwa na sumu iliyotokana na madini ya risasi, shaba na kromiamu ambazo zote zina madhara kwa binadamu.
Alisema utafiti huo ulihusisha wakulima 35 wa maeneo ya Jangwani, Kigogo, Vingunguti na Tabata Shule, ambao wanatumia maji ya mto huo kumwagilia mboga.
Dk. Mwegoha alisema katika utafiti huo uliofanywa na mwanafunzi na yeye kumsimamia, mboga hizo za majani zinauzwa zaidi kwenye masoko ya Ilala na Kariakoo.
Pia Buguruni, Veterani, Tazara, Mwananyamala, Mnyamani, Kigogo, Kisutu, Vingunguti, Tabata, Mikoroshini na maeneo ya jirani na wakulima hao.
Baada ya hapo tulifanya utafiti tukabaini mboga hizo zinanunuliwa katika masoko hayo na kuuzwa katika masoko mengine ya Mwenge na Mwananyamala, hivyo watu wanaendelea kununua na kula chakula hicho chenye sumu, alisema.
Alisema licha ya Vingunguti kukuta bango kubwa likitoa hadhari kwamba maji ya mto huo si salama kwa matumizi ya binadamu, wanyama na kumwagilia mazao, bado wakulima hawana uelewa na wanaendelea kuyatumia.
Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 71 ya wakulima wa mboga za majani wanatumia maji hayo na asilimia 63 hawajui kama yana madhara na hayafai kumwagilia mazao, huku asilimia mbili wakisema wanafahamu kuwa yana sumu.
Mhadhiri huyo alisema wakulima hao hupata kipato cha kuendesha maisha yao ambapo kwa wastani kwa mwezi mkulima hupata kati ya Sh 89,000 na Sh 300,000 kutokana na biashara hiyo.
Tayari Chuo Kikuu hicho kimeshapeleka utafiti huo kuchapishwa katika majarida; la Sayansi na Teknolojia ya Mazingira katika Afrika na la Kimataifa la Utafiti wa Mazingira.
Sababu ya chuo hicho kufanya utafiti huo ni utafiti finyu kufanywa na mwanafunzi mwingine mwaka juzi juu ya uharibifu wa maji ya mto huo, na hivyo chuo kuamua kufanya utafiti mpana zaidi kwa kuangalia maji, mboga na udongo.
HABARILEO ilitembelea eneo la bonde la Mto Msimbazi na kukuta wakulima hao wakiendelea kunyweshea mboga hizo kwa maji hayo hayo.
Wakulima hao walisema wao ndio wanaolisha Dar es Salaam kwa mboga hizo na soko lao kubwa ni Ilala.
Mmoja wao, Evarist Leo, alikiri kuwa maji hayo si salama na yamekuwa yakisababisha wakose soko la mboga hizo katika maduka makubwa - Super Market.
Kanuti Baltazar, alisema licha ya kupeleka mboga hizo Ilala, pia wachuuzi wadogo, hujazana kila siku asubuhi kununua kwenye matenga na kuuza majumbani kwa watu katika maeneo yote ya Jiji.
Pamoja na kutambua kuwa wanatumia majitaka, mkulima huyo aliitaka Serikali iwamilikishe eneo hilo, ili wawekeze na kuzalisha mboga hizo kwa tija.
Hata hivyo, Abraham Kiondo, alisema amekuwa akichimba visima vidogo na kutumia maji safi kumwagilia mboga hizo.
Lakini mwandishi wa habari hizi, alipoangalia moja ya visima hivyo, alibaini kuwa maji yake ni yale yale ya mfereji wa maji taka ambayo huyavuta kwa pampu na kuyaingiza visimani kumwagilia mboga zake.