huyu majjid ni mpuuzi wa kutupwa,ndo maana hata blog yake imepungua wasomaji baada ya kugundua kua ana akili mbovu.mimi na marafiki wengi hatupiti kabisa kwake.Ni upuuzi na uwenda wazimu kuhusisha umaskini wetu na vita ya kagera miaka 35 iliyopita!. Hivi wajerumani waliopigana vita vya dunia mara 2 uchumi wao upoje?. Hivi kupigna vita ndo kunatunyima akili kiasi cha kuingia mikataba ya aibu?. Taifa linaongozwa na wapuuzi, wananchi nao ni wapuuzi kama mleta mada alivo jipambanua! hataki kugusa kiini cha matatizo bali kueleza matokeo ya matatizo kana kwamba vita hutokea tutokea bila sababu.
Mimi sio mwanasiasa ila mwananchi wa kawaida tu. Mtoa mada amepotosha kidogo kwenye hoja ya kutofanya vizuri kiuchumi kwa taifa letu. Simlaumu sana kwani bado alikuwa mdogo wakati huo. Baada ya vita vya kumng'oa nduli Amin katika miaka ya 80 hivi tuliwekewa vikwazo vigumu sana na serikali ya Reagan wakati huo. Hapo maisha yalikuwa magumu sana kwani hatukuweza kuimport chochote madukani kulikuwa hakuna kitu, mashelf yalikuwa yamepambwa na majani ya chai peke yake. Kipindi hicho hata kuoga tulikuwa tunatumia foma kama mnakumbuka. Ni dhahiri kuwa ukuaji wa uchumi wetu ulikuwa duni sana hata tulilazimika kudevalue shilingi kwa kiasi kikubwa sana. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa vifisadi uchwara waliobahatika kuwa RTC na NDL na wahindi wachache waliohoard mali katika majumba yao. Hali ilizidi kuwa mbaya hadi wakati ule Sokoine akiwa waziri mkuu aliwatolea uvivu wahujumu uchumi wa wakati huo. Kwa bahati mbaya Sokoine aliaga dunia baada ya ajali akitokea Dodoma kuja Dar. Katika kipindi hiki mbegu ya ufisadi ilishapandwa na ikaanza kuota miongoni mwa Watanzania na haswa katika chama tawala. Serikali ya awamu ya pili iliingia na haikufanya lolote kurekebisha ufisadi huu. Matokeo yake ni kuwepo kwa wimbi kubwa la matajiri wakiingia kwenye siasa na kugombea ubunge kupitia ticket ya chama tawala. Kwa sababu ya kulewa madaraka na kukosa dira ya uongozi serikali ilishindwa kurekebisha au ku-address changamoto ilizokuwa nazo kama tatizo la uhaba wa umeme. Badala yake serikali ilianza kuingia kwenye mikataba mibovu ambayo ndiyo imetufikisha hapa tulipo leo.
maggid,
..YES,vita ya kagera vilituathiri kiuchumi.
..but it is more than 30 yrs since the war ended.
..Now, dont u think it is IRRESPONSIBLE kudai kwamba matatizo yetu ya sasa ya uchumi yamesababishwa na, au chanzo chake ni, vita vya Kagera?
..kwanza vita ile ilipiganwa ktk eneo dogo sana la nchi yetu.
..hiyo ni tofauti na nchi kama Msumbiji ambao walipigana nchi nzima, tena kwa miaka mingi zaidi yetu sisi.
..leo hii Msumbiji wako sawa na sisi, kama siyo kutuzidi, ktk juhudi za kujikwamua kiuchumi.
..TATIZO LETU NI UONGOZI MBOVU CHINI YA SERIKALI ZA CCM.
cc: Mchambuzi, Nguruvi3, Nyani Ngabu
Mchambuzi,Kwa kuongezea tu, Vita Vya Kagera viligharimu taifa dola za kimarekani milioni mia tano ($500,000,000); Nje ya vita hivi, taifa lilikuwa katika hali ya amani na utulivu kutokana na wananchi kuwa na imani na serikali pamoja na viongozi wao lakini muhimu zaidi, matumaini makubwa juu ya hatima za maisha yao; Tanzania ya leo, amani na utulivu vimetoweka kutokana na wananchi walio wengi kuzizi kupoteza imani na serikali na viongozi wao (CCM) na pia kukata tamaa kimaisha; Katika muktadha huo, ni dhahiri kwamba kila mwaka taifa linapoteza zaidi ya fedha tulizopoteza kwenye vita vya kagera kutokana na ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma; Madhara yake ni mwananchi kuzidi kuumia, wengi wao wakiwa ni vijana; Katika mzingira kama haya, unashawishije vijana kwamba matatizo yanayowakabili yanaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kwa njia ya amani, vijana ambao wengi wao have nothing to lose hata vita vikija kesho? Maandamano ya amani na utulivu ni moja ya njia halali na effective katika demokrasia yoyote ile kwa watu kuonyesha kutoridhishwa na hali zao za maisha; je kwetu Tanzania, ni nani anayegeuza njia hii ya amani na utulivu (maandamano) kuwa ni njia ya kivita, wananchi au serikali waliyoiweka madarakani?