Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 223
- 202
Hivi karibuni Benki ya Dunia imehairisha kupiga kura ya kuikopesha Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya sekta ya elimu nchini.
Kuhairishwa huku kwa kikao hiki kunatokana na kile kinachosadikika kuwa kampeni za wanaharakati na wanasiasa wachache wa vyama vya upinzani wanaotumika na baadhi ya nchi kuhujumu nchi ya Tanzania pamoja na serikali kwa hoja dhaifu kuwa serikali ya Tanzania inawabagua watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni.
Ukweli ni kwamba,kamwe serikali ya Tanzania haibagui wanawake wanaopata mimba mashuleni bali inawasaidia kwa kuwapa upendeleo ambao kimsingi sio haki yao.Upendeleo huu ni ule wa serikali kuwaruhusu wakasome katika shule binafsi ili waweze kuwa na muda wa kulelea mimba zao pamoja na watoto wao kutokana na maamuzi yao. Ruhusa hii miaka ya nyuma haikuwepo kwani wazazi walikua wakiwatoa watoto wao mashuleni na huvyo kutokuendela na masomo kutokana na aibu na Changamoto zingine.
Kitendo cha mtoto wa kike kupata mimba shuleni ni kigezo pekee cha kumfanya kubadili hadhi yake ya kutoka usichana kwenda umama.Majukumu yake yanabadilika pamoja na upeo wake wa masomo darasani,hivyo kulazimika kuwa sawa na wanafunzi wengine ni kero pia kwa wanafunzi wengine.
Endapo kuhairishwa kwa kikao cha Banki ya Dunia kinatokana na sababu hii,basi ni wazi kuwa wajumbe wa Benki ya Dunia watakuwa wanashirikiana na wale wanaohujumu juhudi za serikali katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Zipo sababu anuai zinazothibitisha hili kama zifuatazo:-
1. Sote tunafahamu kuwa tunawapeleka watoto mashuleni wakasome na sio kwenda kufanya ngono zembe.Kitendo cha kuruhusu mkanganyiko wa wajawazito kusoma pamoja na wanafunzi wasio wajawazito kitachochea ngono zembe kwa watoto wetu.
Ni wazi kuwa ondosho la viboko mashuleni pamoja na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii unachochea sana masuala ya ngono katika mashule yetu. Watoto wengi wameambukizwa magonjwa ya zinaa na Virusi vya Ukimwi, na wengine wamepata mimba utotoni na kusababisha vifo vyao pamoja na watoto wanaozaliwa. Ukubwa wa tatizo hili ni zaidi ya zuio la wajawazito kurudi mashuleni na kupata elimu mbadala.
Tishio la serikali kuwapa elimu mbadala kwa wale watakaopata mimba mashuleni na kutokuwaruhusu katika shule za serikali limepunguza idadi kubwa ya wanafunzi wanapata mimba pamoja na ile ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na vifo vya mama na watoto.
2. Pili, hasara inayoweza kupatikana kwa Benki ya Dunia isipotoa huo mkopo,na serikali ikabaki na msimamo wake kuwa mwanafunzi atakayepata mimba shuleni atapata elimu mbadala ili aweze kumlelea mtoto wake vizuri pamoja na kuangalia afya ya mzazi itawalenga watoto wengi wa kike na wa kiume watakaofaidika na mkopo huu ukitolewa. Kama Benki ya Dunia hailengi kuzima juhudi za Tanzania kujiletea maendeleo, basi izingatie hili pia.
3. Sote tunafahamu majukumu ya mama kwa mtoto na adha ambayo anapata mama kipindi cha ujauzito.Je kwa mwanafunzi wa shule ambaye amepewa mimba na mhuni ambaye hayupo tayari kuchukua jukumu la kulea mimba na kumsaidia msichana huyu ambaye ndio mimba yake ya kwanza, aibu kwa jamii na familia yake, pamoja na adha zingine serikali inamtaka apate elimu mbadala ili aweze kumudu hali hii wakati wanaharakati na wanasiasa wanataka akiwa katika hali hii aendelee kusoma. Je nani kati ya serikali na wanaharakati wa kusikilizwa kama kweli Benki ya Dunia anamtendea haki mtoto wa kike?
4. Mkopo huu unawasaidia wale wanaosoma katika shule za serikali, ambao wengi wao ni wa kipato cha kati na cha chini.Watoto wa wanaharakati na wanasiasa wao wanasoma shule binafsi na zile zilizopo nje ya nchi. Serikali kukosa huu mkopo ni juhudi zao za kuendelea kufanya watawaliwa kuwa watawaliwa na watawala kuwa watawala.
Zipo sababu nyingi za kuonesha kuwa unaweza kuwa mchezo mchafu unatengenezwa na mabeberu kuhujumu serikali ya awamu ya tano ambayo inawaletea maendeleo ya kweli wananchi.