Kambaku,
Serikali ina miradi mingi kwa sasa na yote ina kipaumbele,elimu ina kipaumbele kama ilivyo miundombinu,bila barabara mwanafunzi hawezi fika shule,bila hospitali akiumwa hawezi pona,nakadhalika.
Mabeberu sio pesa zao,,,hii ni WB ambao na sisi ni wadau,lakini wanataka kutumia hiki chombo kututawala,na pesa inayopatikana hapa ina umuhimu kwetu kwani ni mkopo wenye masharti nafuu na sio bure.
Kumbe huna ufahamu wowote na unajiandikia tu ndugu yangu....
WB siyo SACCOS kwamba, unatoa changizo lako la mwaka kisha unakuwa na haki ya kukopa....
By the way, kama usemacho ni kweli kuwa Tanzania ni mdau wa WB kwa mrengo wa mtazamo wako, hebu tuthibitishie hapa mchango wa TZ kwa mwaka ni dola ngapi?
Ninavyofahamu mimi ni kweli Tanzania ni mdau wa taasisi hii kwa sbb ya umasikini wetu....!!
Na lengo la taasisi hizi za kifedha za kimataifa ni kuzisaidia nchi masikini kiuchumi kwa kuzipa mikopo ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu yenye riba na masharti nafuu....
Lakini hii haifanyiki kienyeji tu bali ni lazima hiyo nchi (leo ni sisi Tanzania) pamoja na umasikini wake ikidhi masharti na vigezo vilivyowekwa na kukubaliwa kimataifa....!!
Tatizo lako wewe ni moja tu. Unafanya uchambuzi wako kwa mrengo wa siasa zenu uchwara za ndani za kusifia mtu (Rais wenu JPM) huku mkiweka ukweli pembeni na kushabikia ujinga na upumbavu.....!!
Eti unawalaumu na kudhani kuwa wanasiasa walio nje ya serikali (wapinzani??) ndiyo wamesababisha mkopo huu kuzuiliwa....
Kweli? Kweli kabisa ndugu yangu?
Na kwanini usiwalaumu wanasiasa wenye dhamana katika serikali kwa maana ya wana CCM wenzako huko kwa sbb kwa vipimo vyote wao ndiyo chanzo cha haya yote kwa sababu ya SERA, SHERIA na MIPANGO mibaya inayokinzana na kutokidhi vigezo vya kupata fedha hizo??
Wewe unadhani Bodi ya WB inaweza kufanya maamuzi nje ya vigezo na masharti waliyojiwekea kwa sbb eti ya kelele za wanasiasa walio nje ya serikali Tanzania unaowaita wapinzani??
Really? Really?
Kama ndivyo, basi wewe hufai kuwa mchambuzi makini wa masuala ya kisiasa na uchumi popote maana unalisha wasomaji wako matango pori kutoka katika kina cha kukosa maarifa ndani yako!!