Mchezaji bora wa Septemba bara kujazwa noti

Mchezaji bora wa Septemba bara kujazwa noti

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
Mshambuliaji wa timu ya Mbeya City Anthony Matogolo, aliyeibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba anatarajiwa kukabidhiwa zawadi ya Sh. milioni 1 na kombe kesho katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, baina ya timu hiyo dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema wakiwa wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanajisikia fahari kuona wachezaji wanajituma na kuleta ushindani katika mechi za ligi hiyo.

Alisema Vodacom imeona ni jambo bora kutoa zawadi ya mchezaji bora wa kila mwezi ili kuleta ushindani na hamasa kwa wachezaji ili waweze kujituma zaidi.

“Tunaamini kwa kufanya hivi tutaweza kuongeza ushindani na hamasa zaidi kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kujituma na naamini hii ni fursa ya kipekee kwetu kama wadhamini kutoa motisha kwa wachezaji ili ligi yetu iweze kuwa na msisimko,” alisema Twissa.

Aliongeza kuwa zawadi hiyo kwa mchezaji bora kila mwezi na lengo lake ni kuongeza kasi ya kujituma kwa wachezaji na kuleta msisimko kwenye ligi pia inaongeza kipato kwa wachezaji watakaobahatika kushinda kama moja ya njia ya kuwakwamua kwa kipato na kuboresha maisha yao kupitia michezo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, alisema jambo hilo ni jema na linaongeza hamasa miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

Alisema ni wakati wa wachezaji wenyewe kujituma na kushindana kuonyesha uwezo wao ili kuweza kujinyakulia Sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo kila mwezi.

Ligi hiyo itazikutanisha timu mbili kubwa zaidi nchini za Simba na Yanga katika mechi ya watani wa jadi kesho.




Nipashe
 
Ingekiwa hata million 10,mil 1 kitu gani,ndo maana wachezaji wetu timu ya taiga hawana moyo
 
Back
Top Bottom