the great wizard
JF-Expert Member
- Dec 21, 2015
- 1,482
- 887
Mwanaume huyo anataka kampuni hiyo imlipe 500,000 rubles (pesa ya urusi) ambayo kwa haraka haraka ni sawa na dola za kimarekani 7050 (Zaidi ya milioni 14 za kitanzania). Malipo hayo anadai yatakuwa kwa ajili ya kwa ajili ya kipindi kigumu alichopitia na huzuni ambavyo vyote vilisababishwa na gemu hilo. Anasema hakujua kama gemu hilo linaweza likamtawala mchezaji (kumfanya alicheze sana hata wakati ambao inabidi awe anafanya mambo mengine)
Bado mchezaji huyo anazidi kujitetea kwa kusema kuwa kampuni ya ‘Bethesda and SoftClub’ ambayo ni kampuni ya urusi, ingejitahidi hata kuweka stika ambayo ingetoa onyo kwa mchezaji na hiyo ingeweza saidia haya yote yasitokee.
“Kama ningejua gemu hili lingeweza nitawala kabla, basi nisingelinunua au hata kama ningelinunua ningesubiri mpaka wakati wa likizo nipo nilicheze, ningesubiri likizo ya mwaka mpya ndio nianze kulicheza” – alisema mchezaji huyo.
Kwa kufanya hivyo matokea yake ikawa ni kuanza kutega kazini mpaka alipofukuzwa, baada ya hapo akaacha kuona famili na kuongea na marafiki zake. Pia aliacha kula na kulala kwa mpangilio ambayo hii ilichangia afia yake kwa ujumla kudhoofika. Baada ya kuona hivyo mke wake aliamua kumuacha kwa kuwa alikua na tabia mbaya.
Kama kesi hii itaenda mpaka sehemu ya hukumu mahakamani itakuwa kesi ya aina yake kwani mahakama ya urusi haijawahi kupata kesi ya aina hii hivyo wataangalia ni mbali kiasi gani wanaweza kwenda na kesi hii.
Hii sio mara ya kwanza kwa kesi kama hii kutokea. Hata mwaka 2010 Craig Smallwood, kutoka Hawaii iliishtaki kampuni ya korea NCsoft kutokana na gemu la Lineage II. Alilalamika kwa kusema kama angelijua gemu hilo lilikuwa linaweza mfanya mchezaji awe mtumwa angecheza hata gemu la MMORPG.
Kutokana yeye (Smallwood) alisema kuwa alitumia masaa takribani 20,000 katika kulicheza gemu hilo. Ambayo yote haya yalisababisa huzuni na wasiwasi katika mwili wake na baada ya hapo alilazwa kutokana na hali yake aliyokuwa nayo.
Hakimu kutoka shirikisho la marekani ambaye katika kesi alikuwa pamoja na bwana Smallwood, aliamuru kampuni la NCsoft limlipe mdai (Smallwood) haki yake katika mfumo wa hela.
Kama ukifuatilia vizuri wachezaji hawa wote wako sawa katika madai yao. Kuna vitu vinaweza vikakakufanya ukawa mtumwa mpaka watu wakakushangaa, michezo ya magemu ikiwa ni moja kati ya vitu hivyo. Kama makampuni hayatakuwa makini kutoa tahadhari kabla watu hawajatumia gemu zao basi kesi zitazidi kuwa nyingi. Hata sigara isingekuwa na onyo mpaka sasa ingekuwa na kesi za kutosha au hata kiwanda kingekuwa kimeshafungwa.