Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,972
- 22,933
Usijifananishe na king Solomon, huna hela na wala huwezi kupata utajiri kama alivyokuwa Solomon.Solomon kwenye hio hio biblia alikuwa na wake wengi na michepuko
Kwa leo ni wanaume tu.Hii inatuhusu wanaume tuuu au na baadhi ya wanawake wanaotongoza wanaume ili wawekane ilhali wameolewa?
Usisahau pia yupo mjuba mwingine huwa anakuja kwa huyo mchepuko wako kumlala kisha anasepa, unadhani ni wako peke yako?Mtu nikishalala nae sio mchepuko, simuiti mchepuko coz she's mine...hivyo tu!!
Na wewe je haukuji ?Wanakuja
Hakuna pahali Nimesema Polygamy ni dhambi, na ninakazia pia kuwa wana Polygamy waliomwamini Yesu watakwenda mbinguni.Africa bara la Giza,
Hadi wakorea wanatushangaa...[emoji26]View attachment 2497269
Sent using Jamii Forums mobile app
Eeeh kwa kweli hapa kuna jambo,Africa bara la Giza,
Hadi wakorea wanatushangaa...[emoji26]View attachment 2497269
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa maskini hakunifanyi mimi niache kujifunza ya watangulizi wetu kwenye bibilia Solomon hakuwa mzinzi uzinzi mmleta nyie mwanaume hajaumbiwa mwanamke mmoja mmebadilisha maandikoUsijifananishe na king Solomon, huna hela na wala huwezi kupata utajiri kama alivyokuwa Solomon.
Nikushauri tu, acha uzinzi.
Mpango wa Mungu ni mke mmoja kwa mume moja na kwa kulizingatia hilo alimfanyia" msaidizi" na si wasaidizi" mpango wa mitaala ni mapokeo ya wanadamu kama ambavyo baadhi yao walilala na umbu zao, Ruth aliyelala na bint zake, zilikua zama za Giza ambazo Mungu alijifanya haoni.Kuwa na mchepuko ni siri chafu ya mwanamume aliyeko katika ndoa ya - siri hiyo huenda sambamba kwa mwanaume kumdanganya mke wa ndoa kuwa anampenda yeye tu! Akiingia mtaa wa pili ana mchepuko, huko hufanya uzinzi kwa kwenda mbele.
Mchepuko sio mkeo wa pili.
Katika tamaduni ambazo mitala inatekelezwa, kuoa wake 2, 3, 4,…,nk huwa si siri – wanafamilia wote wanafahamiana na kukubaliana – licha ya ushindani baina yao kati ya nyumba na nyumba hakika huwa wanatambuana na kuheshimiana.
Binafsi sitetei ndoa ya wake wengi bali ninatetea sana ndoa ya Mume Mmoja, Mke Mmoja.
Tangu awali mpango wa Mungu kwa wanadamu kuhusu ndoa ulikuwa Mwanamume Mmoja, Mwanamke Mmoja.
Yesu alisema ".. na hao WAWILI watakuwa mwili mmoja"
Mathayo 19:5.
Maana yake hawatakuwa 3, 4, 5,…, waje kuwa mwili mmoja.
Pamoja na hayo ulimwengu huu umevunjika na uko mbali na mapenzi kamili ya Mungu. maana Mungu aliruhusu mitala kinyume na mapenzi yake kamili. Napenda kumtumia Yakobo kama mfano - Wana 12 wa Yakobo - walizaliwa kutoka kwa wanawake 4 tofauti - wakawa mababa wa makabila 12 yaliyobarikiwa ya Israel - waliobarikiwa kutokana na mitala!
Katika 1 Mambo ya Nyakati 3:1-9, Biblia inaorodhesha wake 7 wa Mfalme Daudi - Ahinoamu, Abigaili, Maaka, Hagithi, Abitali, Egla na Bath-sheba. Na Daudi alikuwa na wanawake wengine ambao majina yao hayakutajwa katika Biblia. Hata hivyo, Mungu hakuwahi kumhukumu Daudi kwa mitala - Mungu alimhukumu tu Daudi kwa kuchukua Bathsheba mke wa Uria.
Naamini kuoa wake wengi ni katika MAPENZI YA RUHUSA ya Mungu lakini SIO katika MAPENZI KAMILI ya Mungu.
Katika Agano Jipya, Paulo aliwataka maaskofu kuoa mke mmoja tu ili kutoa mfano wa muungano kati ya Kristo (Bwana harusi) na Kanisa (Bibi-arusi).
1 Timotheo 3:2 - Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja.
Sababu ya Paulo kutoweka hitaji hili la mke mmoja katika kanisa la kwanza ni kwa sababu na ndugu wengi ambao walikuwa na wake wengi. Aliongeza neema, sio hukumu.
Ni heri ubaki na mke mmoja pasipo mchepuko, au uongeze mke wa pili na sio kuzini na huyo mchepuko wako.
Mchepuko sio mke wako wa pili.
Ubarikiwe.
Sipotoshi mpendwa, Ila ni vyema ukijua kuwa mwanaume hahukumiwi kwa kosa la kuoa mke zaidi ya mmoja, Biblia ipo wazi "wazinzi hawataurithi uzima wa milele"Mbn huzungumzii watu walioikimbia zinaa na wakashinda licha ya uzuri na utamu wa mbususu kama Yusuph ,
Acha kupotosha kwa kutumia maandiko
Kwa taarifa yako king Solomon alitoa angalizo kuhusu kumiliki wanawake wengi kwa kusema huo ni ubatili mtupu.Solomon hakuwa mzinzi uzinzi mmleta nyie mwanaume hajaumbiwa mwanamke mmoja mmebadilisha maandiko
Kwenye biblia hakuna huo mstari unaosema mwanaume hahukumiwi kwa polygamy labda utuoneshe lkn si kuchukua mifano ya watenda dhambi wenzet kujustfy uzinzi.Sipotoshi mpendwa, Ila ni vyema ukijua kuwa mwanaume hahukumiwi kwa kosa la kuoa mke zaidi ya mmoja, Biblia ipo wazi "wazinzi hawataurithi uzima wa milele"
Hakuna andiko lenye madai ya mwanaume kuhukumiwa kisa Polygamy.
Ndio maana nimesisitiza "mchepuko sio mke wa pili"
Mwanaume anayeongeza mke wa pili kihalali huyo sio mzinzi, Ila yule anayechepuka na mchepuko huyo ni mzinzi na hata urithi uzima wa milele.
Kwa suala la Polygamy Biblia ipo kimya kabisa kwa maana ya kwamba hakuna hukumu kuhusu hilo jambo.mwanaume hahukumiwi kwa polygamy labda utuoneshe lkn si kuchukua mifano ya watenda dhambi wenzet kujustfy uzinzi.
Kor 1:7 lakini kwasababu ya uzinzi Kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe ,Kwa suala la Polygamy Biblia ipo kimya kabisa kwa maana ya kwamba hakuna hukumu kuhusu hilo jambo.
Kwa suala la uzinzi Biblia imekemea mara nyingi sana, na ina msisitizo mkubwa kwa watu waache uzinzi vinginevyo hawataenda mbinguni.
Ni vyema ukitambua POLYGAMY sio uzinzi
Mwanaume anayetoka na mchepuko ni mzinzi
Mwanaume anayeoa mke zaidi ya mmoja huyo sio mzinzi.
Soma bandiko vizuri utaelewa mpendwa.