Mchepuko oyeee!

Mchepuko oyeee!

dagaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
290
Reaction score
382
Habari wanajamvi,

Wacha niende moja kwa moja kwenye hoja. Mimi ni mke wa mtu nina miaka kadhaa kwenye ndoa zaidi ya kumi, namuheshimu mume wangu na nampenda sana pamoja na watoto wetu, naye analitambua.

Huu ni mwaka wa sita sasa niko na mchepuko wangu na mchepuko wangu naye ni mume wa mtu, na sitegemei kumwacha. Na naweza sema jamani michepuko inaimarisha kutunza ndoa ukiwa na mchepuko wako ukakupenda na mkaheshimiana na mkawekeana misingi yenu, wacha niendelee kusema michepuko hoyee.

Sitaki ushauri wenu wa hoo sijui maradhi yapo, jibu ni kwamba tuko makini na mchepuko wangu kuliko mjuavyo, na ananikuna haswaa na ananijali sana.

Ila swali moja la kizushi, kwanini wanaume mlioko kwenye ndoa mkiwa kwenye sita kwa sita amuwapi mashamsham wake zenu ila mkitoka nje mnaonyesha ufundi ambao hamuwapi wake zenu? Hata mimi nina imani huyu mume wa mtu niliye nae ananipa mashamsham kama yote ila najua kwa mkewe atakuwa anampapasa.

Kwakweli mimi sijutii, na kama dhambi nimeshatubu sababu hata Mungu naye ni shahidi anaona ninachopata.

Wale wote wenye bibi wa kando na babu wa kando tuseme hoyeeeee.

Kwa kumalizia nasema hivi: Mchepuko wangu nampenda sana na na mume wangu nampenda na ndoa yangu siachi na yule naye namshauri sana asimwache mkewe, sisi tupo kwa ajili ya kurutubisha ndoa zetu na kujenga.

Karibuni.
 
Unasema mko makini na mchepuko wako kuhusu maradhi?lakini unakubali kwa mkewe hafanyi kama anavyofanya kwako?na mkewe akiwa na mchepuko wake wa kumkuna kwa siri?na huo mchepuko wa mkewe nao kama una mke ambae nae ana mchepuko?bado sijamzungumzia mumeo na mchepuko wake na mchepuko wa mchepuko wa mumeo
 
Back
Top Bottom