wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,542
Wakuu hii siyo story ya kufikirika hata kidogo, bali ni tukio la ukweli kabisa.
Siwezi kumtaja jina wala kuweka picha yake humu kutokana na maadili ya uandishi, endapo nikifanya hivyo, anaweza kuishtaki JF Kwa kumchafua na hasa ikizingatiwa kuwa, serikali ya Tanzania haiamini uchawi na wala hakuna sheria inayotambua uwepo wa uchawi Tanzania.
Ukimwona huwezi kumdhania hata kidogo, ni mzee wa makamo hivi, mweusi, mwembamba kiasi, anapenda Sana kuvaa kofia, kabila lake ni msukuma na pia ni mwenyeji wa Bariadi ktk kijiji cha Gamboshi.
Kazi yake kubwa ni kuuza vitabu, huwa anauzia Mwanza mjini mkabala na mataa ya Nyerere road.
Yupo serious muda wote, huwezi kumwona anacheka wala kutabasamu, yeye siyo mwandishi ila ni muuzaji tu wa vitabu, na ana urafiki mkubwa Sana na mwanasiasa mmoja wa chama tawala, na inadaiwa ndo huwa anampatia dawa za kichawi.
Mwanasiasa huyo miaka ya nyuma Sana aliwahi kusemekana kwamba aliweka dawa bungeni.
Mzee huyo anajiamini kupindukia utadhani ana uwezo wa kuumba binadamu.
Ameshadhulumu mamia ya watu wanaompelekea kuuza vitabu na ukimfuatilia Sana, anakuambia "live " kuwa uachane naye maana utakufa.
Na ukishindana naye unakufa kweli.
Eneo analoishi watu huwa hawalali usiku, inasemekana wanaolala vizuri ni wacha Mungu tu.
Keshaua makumi ya watu kichawi.
Na inadaiwa kuwa yeye ndo mwenyekiti wa Wachawi kanda nzima ya ziwa.
Cha ajabu inasemekana kuwa ana Elimu nzuri tu ila sasa ndo hivyo keshakuwa mchawi
hatari.
Taarifa za uhakika ni kwamba, kila ijumaa usiku huwa wanazungukia hospital zote na kisha kufanya yao.