Mchango wa Upinzani kwa Yaliyotokea Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchango wa Upinzani kwa Yaliyotokea Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Apr 11, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kufuatilia threads mbalimbali juu ya yaliyotokea huko Dodoma. Nimeona wachangiaji wengi kama akina Field Marshall, etc wakiwafagilia watu walio ndani ya CCM kwa mabadiliko hayo. Pia tusisahau contribution iliyofanywa na upinzani hasa Chadema kwenye haya mabadiliko ya uongozi CCM.

  Naweza kusema kuwa, kwa mara ya kwanza Tanzania, tumeona jinsi upinzani unavyoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa chama tawala kufanya mabadiliko makubwa kwenye ngazi zake za uongozi. Naamini kabisa kuwa haya mabadiliko yasingefanyika kama yalivyofanyika kama upinzani ulikuwa umelala. Kwa mara ya kwanza kabisa chama tawala kimesoma alama za nyakati kuwa wananchi wameanza kugundua au kuelekea kukubali kuwa there is an alternative.

  Of course, kuna watu ndani ya CCM wamechangia kwa kufanyika haya mabadiliko. Lakini vitu kama yale maandamano yaliyofanywa na Chadema mikoani hivi karibuni yamewapa CCM picha halisi kuwa wananchi were openly making their frustrations and options known. I am sure in future tunaweza kuona mabadiliko makubwa kama Tanzania ikiwa strong opposition ready to challenge the ruling party in every angle. Bado Tanzania ina njia ndefu sana ya kuwa na strong oppoistion, but I can sense something here. Upinzani sasa unatakiwa ku-build on this momentum because as Dr Lwaitama said "The resignation of the top leaders is only geared to win public sympathy".
   
 2. k

  kayumba JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Time will tell!
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Upinzani juu!
   
 4. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa na furaha sana kuona chama tawala kujua hatma yao inatoweka taratibu watu wengi waliona wao ni miungu watu.Nawapongeza sana CHADEMA kama sio wao CCM wangeimaliza nchi yetu hongera CHADEMA ndio wapinzani wa kweli hapa nchini.nilikuwa nawashangaa CUF,TLP,UDP na wengine waliokuwa na mtazamo mbaya kwa CHEDEMA sasa wameumbuka walikuwa wanaona na walishirikiana na hao wanaotoswa na CCM kukilaani na kukikandamiza CHADEMA nasema tena sifa wapewe CHADEMA na wala si wengine wameleta mchango mkubwa sana na ninaomba wahakikishe serikalini nako kuna fumuka na wahalifu kuondolewa na kuchukuliwa hatua za kisheria.Nitaendelea kupenda CHADEMA mpaka mabadiliko ya kweli yanafikiwa hasa kwenye rasilimali za taifa letu kumilikiwa na watanzania wenyewe na wala si kikundi kidogo.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  True mkuu
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  hivoo! so cdm ni consultant wa CCM,na wanataka CCM waendelee kuongoza nchi hii milele? you mean goli limefungwa badala ya kuitaka chadema itafute mbinu ya kuingia ikulu, unafurahia jinsi wanavyokipalilia CCM kubaki ikulu!!
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio kazi ya upinzani, yaani kukosoa na kushauri nini kifanyike kwa maslahi ya umma. Upinzani uiolala huo sio upinzani tena bali ni vibaraka wa chama tawala. Hata kama CHADEMA wangekuwa chama tawala, kungekuwa na wapizania wao. Tatizo ninaloliona katika upinzani wa Tanzania ni lile la kila chama kuwa mpinzania kwa mwenzake na kutoaminiana na kwa mtindo huo hata wananchi kutoviamini vyama vya upinzani.
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kazi za upinzani sio kutafuta mbinu ya kuingia ikulu tuu, bali pia kama alivosema Sawanho hapo juu, "kukosoa na kushauri nini kifanyike kwa maslahi ya umma." Yaani wewe unafikiria kukimbilia ikulu tuu? Kuna nini huko. Utapataje mbinu ya kuingia ikulu tuu kama hukikosoi chama tawala na serikali yake kwa manufaa ya umma? Sidhani kama CDM kipo kwa ajili ya kukimbilia ikulu. Kama nia ilikuwa hiyo then, kulikuwa hakuna haja ya kuikosoa serikali kwa manufaa ya umma. One of the most important jobs of the opposition is to constantly question the government. Any Government has to remain answerable to the public at all times, and a good opposition can put the spotlight on serious issues and have them resolved quickly. If the opposition can put on the spotlight serious issues and have them resolved quickly, then the public will be in a better position to trust trust them.
   
Loading...