Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,185
- 307
Ninaomba kunukuu baadhi ya vipengele kwenye hotuba ya Zito ambavyo ningependa tuvijadili:
"Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa aliyetoka kuzungumza hivi sasa [mheshimiwa Mzindakaya] alizungumza kuhusiana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.
Mwaka 2005 Chama cha Mapinduzi kiliwaahidi Watanzania kwamba watahakikisha kwenye ilani yao sekta ya kilimo inakua kwa asilimia 20 [!]. Kwa mujibu wa MKUKUTA wa kwanza ambao tunaumaliza sasa ilitakiwa sekta ya kilimo ikue kwa asilimia kati ya 8 mpaka 10 ili kuweza kuwaondoa nusu ya Watanzania kwenye umaskini [wa kutupwa].
Kwa masikitiko makubwa kwa taarifa ya hali ya uchumi ambayo Waziri wa Fedha ameisoma jana sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 3.2 tu mwaka 2009 [ukiweka na wastani wa ukuaji wa idadi ya watu pamoja na madhara ya mfumuko wa bei ukuaji huu ni hasi (negative growth)].
Katika kipindi cha miaka 5 toka Serikali ya awamu ya 4 iingie madarakani sekta ya kilimo imekua kwa wastani wa asilimia 4 peke yake. Mmeshindwa hata kufikia nusu ya malengo yenu ya ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mmeshindwa hata kufikia nusu ya ahadi kwa mujibu wa MKUKUTA. Hii ni aibu kubwa sana na tumewapa jumla ya shilingi trilioni 26 kwa miaka 4 iliyopita na mmeshidwa kukuza kilimo angalau kufikia nusu ya mambo ambayo nyinyi mlikuwa mmeyatarajia.(Makofi)......
Mheshimiwa Naibu Spika, yaani katika kila shilingi 100 tunaitumia katika matumizi ya kawaida shilingi 23 inabidi twende tukakope, tunakopa kulipa mishahara, tunakopa kulipa posho, tunakopa kununua mafuta ya magari yetu, hii ni nchi ya namna gani? ....
Kwa sababu ni bajeti ya kuchumia tumbo, ni bajeti ya chote tunachokikusanya tunakila hatuendelei na bado tunabakia na gap ya kwenda kutafuta na kwenda kukopa na misaada kwa ajili ya kula na sio kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa sababu asilimia 65 ya bajeti ya maendeleo bado inategemea wafadhili na ukichukua recurrent na development budget asilimia 44 ya bajeti yetu na sio 33 kama Waziri alivyosema bajeti bado tunategemea wafadhili.
[Bajeti ya matumizi ya kawaida ina nakisi ya Tshs 1.8tr ambayo itazibwa na misaada ya wafadhili na mikopo kutoka ndani na nje. Inasemekana mwaka huu Serikali itafanya Deficit Financing (PRINTING MONEY!!!) ya thamani ya takribani 350bn. Katika Bajeti ya Maendeleo kuna nakisi ya Tsh 2.4tr ambayo ni sawa na asilimia 65 ya Bajeti ya Maendeleo na itazibwa na misaada na mikopo kutoka ndani na nje ya nchi]."
Tabia ya kutegemea kukopa ili ununue mahitaji yako ya muhimu ni moja ya tabia ambayo kama mtu hutaweza kuishinda ni certificate ya umasikini wa kudumu... kama hatuwezi kupunguza matumizi (safari, kualika wageni kupita uwezo wetu na ukarimu mwingine usiokuwa na tija kwa kisingizio cha kuitangaza nchi ni vitu wanavyofanya masikini na watu wenye akili za kimasikini) tunaweza tukiamua, lazima tujibane. Ninaogopa kama Kikwete atachaguliwa tena 2010 Tanzania ya 2015 itakuwa sawa na Zimbabwe ya 2005, nasema hivyo kwa sababu mtani wangu huyu Mkwere anapata faraja kwa kuonekana kwenye picha na watu maarufu, si kwa kuona watu wake wanaondokana na umasikini, kwa bahati mbaya kabisa an hulka za kimaskini, hatufai huyu!