Mchango wa CPC katika ukuaji wa kipekee na wa ajabu wa China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1377431860.jpg

Na Eric Biegon - NAIROBI
Ukuaji wa kasi wa China hasa katika kuafikia uwezo mkubwa wa kiuchumi ulimwenguni umekuwa suala la kuzungumziwa katika karne hii. Kwa muda, uchumi wa nchi hiyo umeimarika na kuwa wa pili kwa ukubwa duniani nyuma tu ya Marekani.

Tangu kuasisiwa kwa taifa hilo mwaka 1949, China imebadilika kutoka kuwa jamii iliyokumbatia mambo ya kale na kuwa taifa lenye maendeleo ya kisasa.

Hamna ubishi kwamba hatua hii muhimu imepigwa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti ambacho uongozi wake kwa miaka mingi ulianzisha mageuzi ambayo yalihakikisha taifa hilo katu halitengwi tena kwa suala la uchumi.

Hiki ni chama ambacho ni cha pili ulimwengu kwa idadi ya wanachama wa msingi ambao ni zaidi ya milioni 90 ikifuata Chama cha Bharatiya Janata, maarufu kama BJP, kutoka India ambacho wanachama wake wanakadiriwa kuwa milioni 180.

Lakini bado swala la uhalali wa Chama cha Kikomunisti cha China hutokea karibu kila wakati, haswa katika mataifa ya Magharibi. Wakosoaji wanadai kuwa chama hicho kimekataa kuzingatia uongozi wa kidemokrasia.

Lakini kulingana na wafuasi wa chama hicho, mfumo wa kisiasa uliowekwa na CPC hutoa muundo bora na mzuri zaidi wa utawala kwa China. Chama hicho kinasisitiza kwamba jukumu lake kwa taifa limeimarishwa na kiwango cha kuongezeka kwa uchumi wa nchi, ukuaji wa uchumi na utulivu wa ndani.

Aidha, si siri kwamba CPC pia imetoa mwongozo kwa nchi hiyo kuukumbatia utawala wa makubaliano au uongozi wa pamoja. Mabadiliko kutoka kwa utawala wa mtu binafsi hadi uongozi kwa njia ya chama yamesifiwa kwa kuleta utulivu wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi nchini China.

Aidha, mustakabali wa nchi hiyo ilionekana kuchukua mkondo mpya mara tu baada ya mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha 1978 ambacho kilizindua upya itikadi ambayo ililenga kuzingatia maendeleo ya uchumi. Hii iliweka msingi wa sera ya mageuzi na ufunguzi wa taifa la China.

Kuashiria mwamko mpya wa nchi, Chama cha Kikomunisti kiliandaa na kujitolea hadharani kutimiza malengo ya karne. Lengo la karne la kwanza na ambalo limetwikwa mikono mwa chama cha CPC ni "kujenga jamii yenye utajiri kwa kiwango chochote" ifikapo mwaka ujao wakati chama hicho kitaadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 baada ya kuanzishwa kwake 1921.

Hii inamaanisha kufikia uchumi dhabiti, demokrasia, sayansi ya juu zaidi na elimu, utamaduni unaostawi, maelewano zaidi ya kijamii, na maisha bora.

Hii imekuwa dhamira na nia ya kiongozi yeyote aliyepewa mamlaka na chama kuongoza nchi tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China zaidi ya miaka 70 iliyopita.

Kuanzia Mao Zedong, Deng Xiaoping, Jiang Zemin, Hu Jintao hadi Rais wa sasa Xi Jinping, uongozi wa kisiasa nchini humo umehakikisha kuwa uchumi wa nchi umeendelea kuongezeka kwa kasi, na kwamba jamii inabaki kuwa yenye umoja na udhabiti, na hali kadhalika, kuhakikisha kuwa marekebisho kadhaa yamefanywa ili kutoa msukumo kwa maendeleo endelevu ya China.

Lakini mbali na nyumbani, China pia ni nguzo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa dunia. Viongozi wa nchi hiyo kwa sasa wana ushawishi mkubwa kwenye jamii ya kimataifa. Iwe katika Asia, Afrika au Amerika ya Kusini, nyayo za China zimeonekana wazi.

Mpango wa Ukanda Mmoja Njia Moja, ambayo ilipendekezwa na Rais Xi Jinping, na ambayo sasa imenakiliwa katika katiba ya chama, kwa mfano, inazileta pamoja nchi kutoka bara mbali mbali kwa madhumuni ya kipekee ya kuongeza ujenzi wa miundombinu, ushirikiano wa kifedha, na kubadilishana utamaduni.

Nchini China, chama tawala kimefanikiwa kuhamasisha raia wake kukataa ufisadi au kuwa na kiu ya kujinufaisha kibinafsi na badala yake kujitolea kutimiza ndoto ya China, ambayo ni uamsho wa kitaifa.

Tangu kuwepo kwake, Chama cha Kikomunisti kimekuwa kikiendeleza dhana ya "Utumishi kwa Watu", pamoja na kauli mbiu kama "Usijinufaishe binafsi ila kila wakati ujaribu kuwanufaisha wengine." Kauli hizi zimekuwa kanuni zinazotoa mwongozo kwa chama tawala na wanachama wake.

Hadi leo, Chama cha Kikomunisti kina jukumu la kuunda sera huku serikali ikihakikisha utekelezaji wake. Itakumbukwa kuwa kutokana na sera hizi, China iliweza kuwa nchi ya kwanza kuafikia malengo ya maendeleo ya milenia haswa kwa kuwatoa mamilioni ya watu kutoka kwa umasikini.

Kwa sasa, watu zaidi katika maeneo yaliyo na umaskini wanafurahia nyumba bora, umeme wa bei rahisi, maji safi, huduma bora za matibabu, na elimu.

Ni vyema kukumbuka kuwa tofauti na sehemu zingine za ulimwengu, CPC inatekeleza mfumo wa kipekee ya uwajibikaji ambapo katika kila ngazi ya mamlaka nchini China, kiongozi wa serikali hutumikia pamoja na afisa mwenye kiwango cha katibu wa chama.

Maafisa hawa wa chama wanapatikana katika mashirika anuwai kama vile katika kampuni zinazomilikiwa na serikali, kampuni binafsi, kampuni zinazowekezwa na wageni, vyuo vikuu, hospitali, na taasisi zingine za serikali.

Mahala ambapo maafisa hawa wa chama wanahudumu, wanahakikisha kuwa ajenda ya serikali inatekelezwa ipaswavyo. Aidha, Chama cha CPC ina zaidi ya mashirika ya kiwango cha msingi milioni 4.6 kote nchini ili kukabiliana na mambo ambayo yanahitaji kushughulikiwa na serikali kwa haraka.

Rais Xi Jinping akiwa usukani, CPC imetekeleza dhana ya maendeleo, na kupitisha mkakati wa kipekee wa maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kijamii na kiikolojia. Tangu alipochukua hatamu za uongozi mnamo 2012, Xi amezindua miradi mbali mbali za kuhakikisha udhabiti wa nchi na ustawi.

Katibu wa zamani wa hazina ya kitaifa nchini Marekani Henry Paulson alimsifu Xi akimtaja kiongozi huyo wa China kama "mtu anayefahamu jinsi ya kufanikisha kila jambo linalohitaji kushughulikiwa."

Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha CPC, kwa mfano, alizindua kampeni maasusi dhidi ya ufisadi ambayo inawalenga raia wa ngazi zote katika Jamii bila kujali hadhi au cheo, bila kusaza wanachama wa chama tawala, na ambayo kulingana na wengi imefanikiwa kwani imesaidia kupunguza uvujaji na utumiaji mbaya wa rasilimali za umma.

Bila shaka, chama hicho kinaendelea kukita mizizi na kuhalalisha uongozi wake nchini China kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii kwa Wachina. Walakini, kazi ya kuafikia malengo yake ya karne moja bado inatoa changamoto.

Lakini kupitia kanuni za mwongozo za chama cha CPC, China inaonekana iko tayari kutoa michango muhimu katika kushughulikia changamoto hizi.
 
lengo la uzi nini?
au unataka kutuaminisha kuwa ccm kiwe chama pekee na vingine vifutwe,
 
Kweli China imekuwa hata Sasa imemwaga wanapropaganda kindakindaki humu mitandaoni kujadili na kuyasema wayafanyayo, waliyoyafanya, na watakayoyafanya kwa namna ya chumvi Sana.
Su mbaya NI hatua Nzuri kuelekea hatua za kuwa taifa kubwa
 
Lakini kulingana na wafuasi wa chama hicho, mfumo wa kisiasa uliowekwa na CPC hutoa muundo bora na mzuri zaidi wa utawala kwa China. Chama hicho kinasisitiza kwamba jukumu lake kwa taifa limeimarishwa na kiwango cha kuongezeka kwa uchumi wa nchi, ukuaji wa uchumi na utulivu wa ndani.
 
Back
Top Bottom