Mchange, Shonza kuhamia CCM punde

Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote. Tunakuomba adui zetu wajulikane kabla hawajatudhuru. Uwalinde viongozi wote waadilifu na wapenda amani na maendeleo ya watu wote. Wape upofu mafisadi wasiweze kufanya uovu bali mema yatawale mioyoni mwao.
 
Hivi Mchange ni nani hasa mbona mimi hata simjui? maana mimi niko Mwanza kuna watu wengine hata hawana impact yoyote viongozi cdm malizeni kabisa masalia watu wako nyuma yenu.
 
Yaani jamani Tanzania tuna bahati mbaya sana. Watoto wanafeli, hospitali hazina dawa, wamama wanajifungulia sakafuni, maji ni tabu, bei za bidhaa hazikamatiki, wananchi wanauana kwa sababu za dini.....matatizo yoooote hayo bado CCM wanaona mikakati bora inayofaa kwa sasa ni kurubuni vijana wasio na msimamo!

Hivi wazungu wakitudharau sisi waafrika na hasa sisi Watanzania watakuwa wanakosea? I just can not imagine, kwa mfano, Waziri mkuu wa Uingereza na team yake waanze kujikita kwenye siasa za mamluki kwenye hali ambayo 94% ya watahiniwa wamefeli! People will eat them alive!

Niweke tu kwenye lugha ya kiungwana, wanasiasa vijana wa CCM wanatakiwa waliletee heshma hili Taifa. Kwa sasa ni kama kichwa cha mwendawazimu, tofauti na wanavyodani. Tumekuwa kama kituko hata ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Matokeo ya watoto wetu ndiyo kabisa yanalifanya hili Taifa lionekane kama limeondoa Oxygen tank!

Hivyo basi, wanasiasa hawa vijana wa CCM wajitahidi kuonDokana na hizi siasa za ki-soviet, zilizochuja na kurudi kwenye ulimwengu wa sasa illi waindoe Tanzania kwenye hili tope la aibu.

Badala ya kujikita kwenye siasa za ki-mamluki, wangekaa chini na kutafuta ni jinsi gani ya kufikisha maji kwa wananchi, ni namna gani ya kuinua huduma za afya, elimu na hali duni ya maisha kwa jumla. Kuendelea na hii mikakati ya kiuwendawazimu, ya kurubuni vijana, ni madharau kwa watanzania, na mbaya zaidi ni kutaka kulimaliza kabisa hili taifa. Hii haikubaliki hata kidogo. Ifike mahali wanasiasa vijana wa CCM waambiwe enough is enough. Nchi inakwenda vibaya.
 
Hawa wote ni wanafiki na bora waligundulika mapema fagio la chuma likapita kwani ni kama makamasi na pua,makamasi usipoyatoa mapema yataziba pua na utashindwa kupumua congrats BAVICHA.
 
Huwa nachukia sana ninapoona thread zinazohusu majitu majinga yakijadiliwa. Hivi huyo Mchange sijui nani analipi la kuonyesha mfano kuwa kutoka kwake Chadema kuna athari fulani? Tusiwape promo vijana waliokosa mwelekeo kwa kuwaandika andika mpaka wenyewe wanakesha mtandaoni kujisoma kuwa wanajadiliwa.Ukiona kijana wa kiume anashikwa kiuno kisha anabadili uelekeo basi kama mwanao jua huyo si ridhiki kabisa na huna haja ya kujisifia mbele ya wenzio kwamba una mwana kidume,hao ukichunguza kwa undani swala la kutokuwa riziki haliko mbali sana nao. Vijana wangapi wame vunjwa miguu na hata kuuwawa wakitetea hiki kinachopiganiwa halafu wengine kwa kupewa lunch na mvinyo kidogo wanasaliti juhudi hizo mnadhani wako sawa hao kiakili? Pse msituletee habari za harakati zao,pelekeni habari hizo kwenye blog za wanazi wa CCM au FB. Eboh!
 
Mchange najua unapitia hapa JF,umemwelewa mkuu Kanundu anachomaanisha? Basi hayo ndio mawazo ya wengi kuwa pengine hiyo ndio hali halisi.
Kama ndiyo basi hakuna shida zamani zamani tulikuwa tunasema Dukinaa,ila kama sio kwa nini unaweka utu wako reheni mpaka ufikiriwe hivyo?
 
Haya masalia yanawasaidia nini, mbona akina shonza hakuna walichofanya, masikini maccm yanatapatapa kila tawi wanaloshika linatelewa, sasa wanakaribia kufika chini, anguko takatifu.
 
Jamani Mgamba fanyeni kazi kuwanusuru wananchi, CHADEMA wamebalikiwa na MUNGU/ALLAH....
 

Chuki yangu dhidi ya CCM na kwakua vyama vingine vya upinzani ni hopeless basi ni heri niunge mkono CDM kwakua kiukweli kuna watu wanajenga hoja zenye mantiki na si ushabiki tu na kupiga piga kelele. Hizi hila za kuhadaa wananchi zinazidi kunifanya nione CCM kama ni mtu anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Na huyo mchange kwa mara ya kwanza nimeanza kumsikia humu JF kwe sakata la kina saa nane sa kwamm ambae kila siku niko JF na vyombo vya habar sjui hata ana qualities gan je kwa raia wa kawaida atakua na influence.?
Advice to CCM; acheni propaganda nchi inakufa angalau kwa hii miaka michache mmebakiza jaribuni kutimiza wajibu wenu. Do u think propaganda zita hold hadi 2015?
 
Waache wapoteze muda na kupewa matumaini kama wapewayo walimu wa Tz kuwa ipo siku serikali itawajali kimaslahi kumbe ni danganya toto!!

Kihakika Machange anapoteza muda wake tu.

Acha kuchezea walimu wewe, sisi si watoto wadogo nadhani bado hamjatujua. Matokeo ya 4m 4 yanadhihirisha mjinga ni nani pale kati ya wanafunzi (hata viongozi wa serikali tumewafundisha sisi) na walimu .
 
Hawa vijana si kwa sasa siyo wanachama wa chama chochote. Kwani kujiunga CCM kuna tofauti gani na mwananchi mwingine. Mbona watu hapa wanapiga kelele sana.

Waacheni kwa vile wanatimiza haki yao ya kikatiba, kuwachagulia sehemu ya kwenda au kuwabeza ni kutaka kubaka haki yao ambayo wewe unajivunia.

Kwenye siasa, hakuna mtu mwenye haki miliki pekee hata kuwa na hisa za kisiasa zaidi ya mwingine.

Kwa kelele hizi isije ikawa ni jiwe la pembeni.

Ni angalizo tu.
 
Hivi Mchange ni nani hasa mbona mimi hata simjui? maana mimi niko Mwanza kuna watu wengine hata hawana impact yoyote viongozi cdm malizeni kabisa masalia watu wako nyuma yenu.

Ni mwizi wa simu.
 
Kitu cha tar 18 Jan raia wanatoana macho March kasoro
 
dawa ya masalia ni kuwapotezea tukiwaongelea sana tunawapa promo za bure ambazo hawastahili kwakweli....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…