Mchanganuo wa gharama za kuagiza gari toka nje ya nchi

Mchanganuo wa gharama za kuagiza gari toka nje ya nchi

mew 123

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2024
Posts
307
Reaction score
193
Habari,

Pasipo kupoteza muda naomba niende Moja Kwa moja kwenye mada na kutoa ufafanuzi yakinifu.
Katika mchakato wa kuagiza au kununua gari Toka nje ya nchi kama vile Japan China marekani Dubai na uingeeeza(UK) huwa kuna gharama tofauti tofauti ambazo ningependa tuzijadili hata kama ni Kwa uchache lakini Vizur.

1. Gharama za ununuaji wa gari
Hii ni Bei halisi ya gari, ni jambo muhimu ambalo pindi unapotaka kununua gari unapaswa kujua. Mfano unataka kununua gari aina ya SUBARU FORESTER - SHJ SUV 2012 ukimuuliza agent Bei yake kabla hajakupa mchanganuo yaani kataja Bei ambayo ni jumuishi ya gharama zote, ni Vizur ukajua gharama halisi au Bei halisi ya gari kabla ya gharama zingine sababu pindi unapoagiza gari, malipo hufantwa Kwa awamu kuu mbili, awamu ya kwanza ni ulipaji wa hela ya kununulia gari na awamu ya pili ni ulipaji wa gharama zingine ingawa kama unaweza unaweza kulipa yote.

Mfano wetu ni gari a SUBARU FORESTER - SHJ SUV 2012 labda Bei yake ni MILIONI 26 ukijumuisha na gharama zingine, Kwa hesabu za haraka Bei halisi ya kununulia gari au kuagiza gari ni 12,500,000/=

2. Gharama za Kodi za TRA
Pindi gari linapofika ktk bandari ya dar es salaam huwa kuna Kodi ambazo gari huwa linatozwa l, Kodi hizi ni kama vile import duty, excuse duty, VAT lkn pia na gharama za usajili wa gari

Kwa mfano gari ni SUBARU FORESTER - SHJ SUV 2012 ambalo Bei yake halisi ilikuwa ilikuwa ni milioni 12,500,000/= Kodi unaweza kuwa 11,150,000

3. Gharama za bandarini
gharama hizi hufahamika clearance and forwarding fees gharama hizi huwa haziko specific Bali hutofautiana kutokana na ukubwa wa gari mfano gari aina ya Toyota harrier gharama zake huweza fika Hadi milioni Moja(maximum) wakati Nissan civilian bus mhuweza fika Hadi milioni 2.5

4. Gharama zingine
Gharama hizi ni kama vile gharama za usafirishaii hususani Kwa nchi ambazo kampuni unayotumia kununulia gari gharama za usafirishaii hazijajumuishwa ktk total cost, gharama zingine ni gharama za clearance and forwarding agent fees hizi ni za agent anayekufanyia clearance and forwarding bandarini, gharama zingine pia ni ukataji wa bima ya gari

OZB CAR IMPORTERS AGENTS
Tunajihusisha na uagizaji wa magari Toka nje ya nchi tukishirikiana na kampuni ya Beforwad. Kazi zetu kuu ni kutoa ushauri wa kitaalamu Kwa wateja wetu na kuwasimamia katika suala zima la ununuaji wa gari Toka nje ya nchi, kuwasaidia katika taratibu zote kuanzia uagizaji wa gari Toka nje ya nchi, ulipaji wa Kodi na gharama zingine kama vile clearance and forwarding agent fees, usajili wa gari na ukataji wa bima ya gari. Kiufupi tunasimamia na kushuggulikia taratibu zote za ununuaji na uagizaji wa gari kuanzia hatuna ya kwanza ya mteja kuchagua gari Gani anahitaji, kuweka order na taratibu zingine zote Hadi pindi gari linapomfikia mkononi.

Pindi utakapoichagua OZB CAR IMPORTERS kuwa msimamizi na mshauri wako katika suala zima la ununuaji wa gari hususani Toka nje ya nchi, tutakupa ushauri Bora na sahihi kuhusiana na uchaguzi wa gari lako, tutakupa ushauri na mchanganuo wa kiujumla kuhusiana na gharama za usafirishaii, Kodi za TRA, gharama za clearance and forwarding agent fees na pia tutakupa ofa ya kukukatia bima ndogo ya gari kwani tuna ubia na kampuni ya Britam insurance kupitia wakala wake Barontam insurance. Kwa wateja wetu ambayo watahitaji kukata bima kubwa ya gari gharama za ukataji wa bima kubwa zitakuwa juu ya mteja na sio kampuni, kampuni itahusika na uslaidizi katika ukataji wa bima kubwa na sio gharama tofauti na bima ndogo ambayo kampuni huwajibika katika usaidizi na gharama pia. Lakini pia TUNATOA mkopo wa ununuzi wa gari Toka nje ya nchi Kwa wale wote ambayo wanakuwa wamapungukiwa na kiasi Cha pesa kinachohitajika katika uagizaji wa magari kwani tuna ubia na kampuni ya platinum credit.

OZB CAR IMPORTERS tunatoa ushauri wa Bure pasipob gharama yeyote kuhusiana na uagizaji wa magari Toka nje ya nchi kuanzia uchaguzi sahihi wa gari kutokana na uwezo wako wa kiuchumi, muda ambao gari lako litachukua kusafiriahwa Toka nchi husika mpaka kukufikia, muda ambao utatumika katika kukamilisha taratibu za kisheria na namna Gani ambayo unapaswa kufanya malipo lakini pia na ushauri mwingine ambao mteja atataka kujua.

Kwa wale wote ambao watakuwa na changamoto ya upungufu wa fedha hususani katika uagizaji wa gari au ulipaji wa Kodi za TRA na ufanyaji wa clearance and forwarding bandarini, basi OZB CAR IMPORTERS tutakusaidia kupata mkopo Kwa gharama nafuu na ambazo mteja anaweza kuzimudu.

Ili kuweza kupata taarifa zaidi kuhusiana na huduma zetu ni Vizur zaidi ukitembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii ambapo utaweza kujifunza mengi lakini pia unaweza kuwasiliana nasi Moja Kwa Moja kupitia Whatsapp+255686153806
TikTok: OZB CAR IMPORTERS
Instagram: OZB CAR IMPORTERS
Facebook page: Ozb car importers.
Whatsapp: +255686153806
Asante karibuni sana.
 
Nilisikia kuwa kodi za "imported cars" zinaongweza. Sasa hapa ni kwa maslahi gani?

Kuna kiwanda cha magari nchini kinalindwa ilibwatu wanunue ya hapa waache kuagiza?
 
Uchanganuzi mzuri. Sema ushuru bandarini ndiyo kikwazo cha watu wengi kushindwa kuagiza ndinga.
 
Nilisikia kuwa kodi za "imported cars" zinaongweza. Sasa hapa ni kwa maslahi gani?

Kuna kiwanda cha magari nchini kinalindwa ilibwatu wanunue ya hapa waache kuagiza?
kile kiwanda cha saturn au
 
Nipo singida. gari ikifika bandarini, tumeshalipia hatua zote, lakini sina udhoefu kuendesha barabara za Dar. Je mnahuduma ya madereva?
 
Back
Top Bottom