Mchanga kwenye Figo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchanga kwenye Figo

Discussion in 'JF Doctor' started by MAMA POROJO, May 22, 2012.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kuna aina yoyote ya chakula kinachoweza kuzuia mchanga kukaa kwenye figo, na ni dawa gani inaweza kutumika kuondoa mchanga huo au hadi upasuaji ufanyike?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Lemonade prevent formation of kidney stones

  Accommodation and orange drinks can prevent the formation of
  kidney stones. This is the conclusion by researchers from Massachusetts General
  General Hospital (USA).


  According to them, these sweet drinks containing high levels of citrate
  (Citrate), which prevent oxalate stones from

  calcium. As we know, kidney stones (concretions) results
  metabolic disorders, urinary tract infections, difficulty passing

  urine in the urinary tract and other problems. In case of violation of the metabolism
  uric acid uric acid concretions are formed when calcium-phosphorus chaos

  Metabolism - phosphate, and when the body is more oxalate
  - Oxalate. According to compulenta.ru, are common calcium oxalate-
  stone. To prevent their formation for a long time doctors have used

  potassium citrate (potassium citrate). 10 years ago, experts found
  that home-made lemonade, increased significantly the level of citrate

  in the urine of those whose bodies are tend to form kidney stones. How
  this way to prevent acne lemonade, she remained
  clear, but some doctors still recommend patients drink more often

  This drink. In recent work, researchers tried to find out
  containing soda factory as much citrate as lemonade house.
  The results showed that in diet drinks, from citrus (7Up,

  Sunkist Orange, sprite, ginger Ale Fresca and Canada Dry) level is much
  higher than in home-made lemonade. As for Coke, it is
  Citrate or very little, or almost none.

  source www.realt5000.com.ua


  Tiba ya kusafisha figo na kibofu cha mkojo

  changanya kwa pamoja juisi ya kiazi sukari juisi ya tango na juisi ya karoti kunywa kila siku mara tatu au mara nne kwa siku.

  Pia kunywa sana maji inasaidia kusafisha mchanga kwenye figo
  ( Drink of Water ) Can Help


  Promotes Weight loss
  Combats cancer
  Conquers kidney stones
  Smoothes skin


   
 3. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,963
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]KADRI sayansi na technolojia inavyozidi katika nchi zinazoendelea wataalamu wamekuwa wakitambua baadhi ya magonjwa ambayo miaka michache iliyopita yalikuwa hatambuliki kirahisi au wakati mwingine yakachanganywa na magonjwa mengine kwa sababu ya ukosefu wa vipimo sahihi. Leo tunaona tatitizo la mawe katika figo likijitokeza zaidi na wahusika wanashangaa kwa nini tatizo hili liongezeke zaidi? [/FONT]

  [FONT=&amp]Jibu la kwanza ni kwa sababu zamani hakukuwa na vipimo vya tatizo hilo kama CT-SCANER, Lakini pia kubadilika kwa maisha kunachangia kuongezeka kwa tatizo hili. Mawe katika figo au ”kidney stones” ni aina ya madini yanayotengenezwa katika figo au katika njia ya mkojo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Mawe haya hutengenezwa zaidi na madini ya calcium na oxalate au phosphate. Mawe haya yanaweza kutengenezwa kwenye figo au katika kibofu cha mkojo. Ukibwa wa mawe haya unatofautiana kuanzia mawe madogo kama 4mm mpaka 10mm. Ukubwa wa mawe huchangia sana aina ya matibabu anayopewa mgonjwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Chanzo[/FONT]
  [FONT=&amp]Chanzo kikuu cha mawe hayo ni kutopata mkojo wa kutosha amabayo inaweza kuchangiwa na kutokunywa maji ya kutosha au kuongezeka kwa madini yanayotengeneza mawe haya mwilini. Hi husababisha calcium nyingi katika mkojo ambayo huanza kutengeneza mawe. [/FONT]
  [FONT=&amp]Kuna baadhi ya magonjwa na yanayohusishwa na kuwa na mawe na kuna aina za dawa sinazohusishwa na ongezeko la mawe katika figo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Magonjwa hayo ni pamoja na ‘gout’ ambao huongeza tindikali (acid) katika damu na mkojo hiyo kutengeneza mawe yaitwayo uric acid stones. [/FONT]

  [FONT=&amp]Tatizo za ufyonzaji mkubwa wa calicium katika chakula ni tatizo la kurithi nalo husababisha kukithiri kwa kiwango cha calicium kwenye damu ambayo hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo na hivyo kuteneza mawe kwenye njia ya mkojo. Magonjwa mengine yanayohusishwa na mawe ni kama kisukari, shinikizo la damu nk. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kuna dawa zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa mawe ni zile zitumikazo kutibu magonjwa ya tumbo ya kupunguza tindikali tumboni tumboni, dawa za kuongeza mkojo na dawa za Ukimwi na hasa dawa iitwayo ‘indinavir’.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tabia ya ulaji wa vyakula vifuatatavyo kupita kiasi unaweza kukuweka katika hatari ya kupata mawe katika figo na kibofu cha mkojo. Navyo ni vyakula vya protini itokanayo na wanyama, chakula chenye chumvi nyingi, kutumia vyakula vyenye sukari kupita kiasi, vyakula vyenye vitamini D kupita kiasi na vyakula vyenye ‘oxalate’ nyingi kama spinach. Kutokuwa na tabia ya kunywa maji inakuweka kwenye hatari zaidi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dalili zake[/FONT]

  [FONT=&amp]Dalili za mawe katika figo hutofautiana kutokana na mtu na mtu lakini zaini ni maumivu na vichomi ya tumbo upande wa chini (flank pains) na damu kwenye mkojo. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa makali kutokana na ukumbwa wa mawe.[/FONT]

  [FONT=&amp]Matibabu ya mawe katika figo na njia ya mkojo yanategemea ukubwa wa mawe pia. Mawe mmadogo ya ukubwa wa 4mm yanaweza kutoka yenyewe ndani ya masaa 48 kwa njia ya mkojo na mgonjwa atashauriwa kunywa maji kwa wingi. [/FONT]

  [FONT=&amp]Matibabu[/FONT]

  [FONT=&amp]Dawa za maumivu hutolewa kwa wenye maumivu makali na maumivu madogo. Pia kuna dawa zinazoweza kuyeyusha mawe lakini wakati mwingine hushindwa kufanaya kazi, hivyo njia nyingine za matibabu hutolewa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Njia hizi ni kama kuwekewa kifaa maalumu chenye mtetemo ambacho hupasua mawe na kuwa kwenye vipande vidogo ambavyo hutoka kirahisi kwa njia ya mkojo baada ya kunywa maji mengi. Njia ya upasuaji mdogo inayoitwa ‘lithotripsy’ inatumika mawe yanaposhindwa kupita kwenye mirija ya mkojo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kinga [/FONT]

  [FONT=&amp]Ili kujikinga usipate mawe katika figo na njia ya mkojo ni muhimu kunywa maji mara kwa mara, kuangalia vyakula tunavyokula kuepuka wingi wa calcium na oxalate. Ukitumia dawa nilizotaja hapo juu unywe maji mengi ili kuondoa madini kabla hayajatengeneza mawe.[/FONT]
   
 4. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,963
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Removal-of-Kidney-stones.gif

  k_stonef1.jpg  1444760_com_kidney_sto.jpg

  Juu ni baadhi ya mawe hatari ndani ya figo, yapo mawe ambayo ni saizi ya mchanga, haya ni rahisi kutoka kama una tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku.

  Mchanga huo hujikusanya na kujifinyanga hadi kuwa makubwa, yapo mawe makubwa kwa kipimo cha mpira wa tenisi. Mawe yenye vipembe ni hatari zaidi kwani husababisha kukwaruza kuta za mirija ya figo na kibofu cha mkojo, na mtu anakuwa anakojoa mkojo uliochanganyika na damu. Mawe haya makubwa huziba njia ya mkojo kabisa hadi ufanyike upasuaji wa kuyaondoa.

  Kinga muhimu ya hili tatizo ni unywaji wa maji ya kutosha kila siku kuondoa chembe chembe za uchafu zinazojikusanya taratibu kwenye figo kwa njia ya mkojo.
   
 5. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Punguza chumvi, kunywa maji mengi. Pia kama unakunya dawa hakikisha unamjulisha daktari wako kuhusu hizo dawa, kuna dawa zina changia kupunguza performance ya figo.
   
 6. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya wakuu darasa zuri sana mbarikiwe sana
   
Loading...