mchakato wa katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mchakato wa katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mr zam, Apr 2, 2011.

 1. M

  Mr zam Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana JF, mchakato wa katiba mpya unategemea kupelekwa bungeni katika kikao kijacho cha bunge kwa mujibu wa taarifa ya mwisho wa mwezi wa March ya Mheshimiwa raisi lakini inakuaje yale makongamano, semina nk yanayotoa ufahamu wa namna ya undwaji wa katiba hiyo mpya ili umuakisi kila mtanzania kwa hadhi yake hayaanzi kutolewa au mpaka waanza vyama vya upinzani?
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu muswada unaotarajiwa kuletwa bungeni, pamoja na mambo mengine unapashwa kutoa utaratibu rasmi utakaotumika siyo tu katika kukusanya maoni ya wananchi, lakini pia namna maoni hayo yatakavyoratibiwa na hatimaye kujumuishwa katika rasimu ya katiba itakayoandikwa kufuatia ukusanyaji wa maoni hayo. Hivyo kwasasa kazi ilyoko mbele ya sisi zote wenye mapenzi mema na taifa ili, ni kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba sheria itakayotungwa na bunge baada ya kuwasilishwa kwa muswada huo inatoa fursa na uhuru wa kweli kwa raia wote kushiriki katika mchakato uandikaji wa katiba mpya.
   
Loading...