Mchakato wa katiba mpya walio nje je?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa katiba mpya walio nje je??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Apr 17, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Kuapishwa kwa tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba mpya kunaashiria kuanza rasmi kwa mchakato huo wa kupata katiba yetu mpya. Kuna watanzania wengi sana waliopo nje ya nchi kikazi, kimasomo kibishiara au kwa shughuli nyingine yoyote ya kujipatia kipato.Watanzania hawa wanaweza kuwa na mchango na mawazo mazuri sana kwa katiba yetu hasa kutokana na elimu zao lakini kikubwa zaidi uzoefu wao wa kimataifa na kukutana na watu mataifa mbalimbali na kuona au kuguswa na tamaduni na sheria mbalimbali za mataifa wanamoishi.
  Nawasilisha hoja hii nikitaka tuchangie njia sahihi za kupokea maoni kutoka kwa watu hawa walio nje ya nchi na namna ya kupiga kura ya maoni kuhusu katiba muda ukiwadia! Itakuwa ni makosa kupuuza maoni ya hawa watanzania wenzetu walio nje tukitilia maanani uzoefu wao na haki yao ya kikatiba kushiriki kikamilifu kuandaa katiba yetu,. Nawasilisha
   
Loading...