Habari za kutwa wadau nianze moja kwa moja kama thread inavyojieleza. Ninapenda kuwapongeza mamlaka ya bandari tpa kwa namna walivyoendesha mchakato wa kuajiri hivi karibuni.
Ni kweli kwamba ajira katika taasisi za kiserikali ni magumashi na urasimu mkubwa. Ninapowapongeza sio kwamba wapo fair au wamefanya vizuri. Ni kweli walijaza watu duce , ifm na baadae uwanja wa taifa.
Nimepongeza muda waliotumia kufanya mchakato wao/magumashi yao na hatimaye ndani ya muda mfupi sana/wiki kadhaa waliweza kuwapata watu wao wanaowataka.
Nimeandika hili kwa lengo la kuwaonyesha ndugu zetu wcf, lapf na ppf ambao wanajaza watu duce,ifm na uwanja wa taifa lakini mchakato unachukua hadi miezi 9 kupata majibu, hili linawasumbua vijana wengi ambao wanabaki kusubiri majibu ambayo hayajulikani yatatoka lini. Mfano mzuri watu walijazwa duce na ifm mnamo tarehe 18/03/2017
Na workers compensations fund (wcf) na kufanya aptitude test ya kushade majibu ambayo yanasahishwa kwa computer lakini cha kushangaza mpaka leo hii tarehe 19/05/2017 hawajatoa ata majibu tu ya huo mtihani, sasa wakitoa leo au kesho je mchakato utakamilika baada ya miezi mingapi mpaka mtu kupata mkataba na kuanza kazi?
Je ni mwaka mzima au miwili ?. Hizi ni dalili mbaya sana na watu wanaanza kuamini kwamba huu ni urasimu mtupu na kuna watu walishaandaliwa. Ni bora mkafupisha mchakato ili watu wajue waliokatwa ni nani na waliopata ni nani ....Tuache kutesa watanzania kwa kuwaita watu 7000 kwenye usaili wakati nafasi za ajira ni 4 au 6.
Kama ni urasimu fanyeni kimya kimya waiteni mnaowajua na sio kutesa maelfu ya watu kutoka mikoanina mnajua wazi kabisa hamuwapi ajira. Ppf, wcf,lapf jifunzeni kuhurumia wasomi wanaoteseka na kusaka ajira katika taasisi zenu
Hongera tpa kwa kufupisha mchakato na waliokatwa wameshasahau maumivu na waliopata wameshajielewa na tayari kuanza kazi.