Mchakato, upembuzi yakinifu na umeya wa Jiji Dar.

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,210
Mara nyingi nimekuwa nikimsikiliza Rais wangu JPM wa Hapa ni Kazi TU! akisema Hataki kusikia mtu anasema oohh tuko katika mchakato, mara oohhh upembuzi yakinifu, oohh tunajipanga; kwamba Tanzania tumechelewa sana na kwamba anataka mambo yaende kwa kasi. Ni Jambo Jema!


Sasa hiki kiloja cha uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam hebu sote tujadili; suala liliko chini ya TAMISEMI, iliyoko katika ofisi ya RAIS na Raisi ni John Pombe Magufuli wa Hapa Kazi TU! mbona hakina tofauti na habari ya TUKO kwenye Mchakato, upembuzi yakinifu, tunajipanga? Hii ni upuuuzi mtupu! Kila mwenye akili anajua sifa za wajumbe wa kupiga kura ya uchaguzi wa Meya, idadi ya wajumbe iko wazi lakini suala hili haliishi, mara wanachama CCM wameweka pingamizi, mara wajumbe feki wamekuja kupiga kura, mara pingamizi feki limeleta vurugu, aliyeleta pingamizi feki hachukuliwi hatua yoyote lakini wanaolalamikia pingamizi feki wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka, hii nini sasa!


Jambo hili linalazimisha wananchi kuamini maneno ya Bwana Lowasa na Maalim Seif kwamba walishinda katika uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 lakini hawakutangazwa, sasa kama umeya imekuwa hivi sembuse urais?


Tuseme ukweli kuwa JIPU ni Mkuu wa Mahala TAMISEMI ilipo, SIYO OFISI YA WAZIRI MKUU TENA BALI - OFISI YA RAIS! Tatizo jipu lipo mgongoni mwa mtaalam wa kutumbua majipu, anashindwa egeuze vipi mikono na macho kuliona na kulitumbua, ukweli uko palepale kuwa analisikia, linamuuma ajabu, na huenda hapati usingizi kwa maumuvu hayo.


CCM Msaidieni huyu mtaalam wetu wa majipu, acheni uchaguzi ufanyike. Anzeni kujifunza taratibu kuachia ngazi za uongozi katika baadhi ya maeneo. Ukijua kushinda usiishie hapo, jifunze na kushindwa, ndivyo sheria ya demokrasia ilivyo. Demokrasia haina kung'ang'ania uongozi la hasha! DEMOKRASIA NI KUSINDA NA KUSHINDWA. Kung'ang'ania ni UDIKTETA!, nadhani nyie sio madikteta!


"IT IS EASY TO BECOME NUMBER ONE THAN REMAINING NUMBER ONE! Wanafalsafa waliyajua haya mpemaaaa, kuweni wastaarabu. Kuna wimbi kubwa nyuma yenu, vijana bado wana kiu ya mabadiliko, na wengine ni wanajeshi na vyombo vingine vya usalama msiwachokoze. Waswahili wanasema Ukimuudhi mchija Mbwa Wazimu watakurudia!


Jambo la kuzingatia ni kwamba Mabiliko haya ni natural, ndivyo binadamu alivyo, ndiyo maana leo utapenda kula ugali, kesho wali, keshokutwa ndizi, kwani hili CCM hamulijui!


Mwenye masikio na asikie!
 
Katika hali ya kawaida, Ccm wana kawaida ya kuitegemea Serikali iwabebe ktk mambo wanayokwama. Kama hakuna mkono wa serikali uchaguzi huo ungeshafanyika. Rejea suala la Kinyerezi. Inapofika mahali Raisi hataki Meya wa Manispaa akae meza kuu wala kutambulishwa, atakubali Meya wa Jiji atoke Ukawa?
 
mtaangukia palepale tuliposema sisi kina gogo la shamba kwamba,Makufuli hawezi kuamua haki pale kwenye mvutano kati ya ccm na vyama pinzani, lazima atawapendelea wale waliolazimisha ushindi wake
 
Back
Top Bottom