Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Serikali yabomoa nyumba za mamilioni Mbezi Beach
Katapila likibomoa moja ya nyumba nne za Tibe John katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam jana.
Picha na Beatrice Moses.
Na Beatrice Moses na Ally Nguba, Mwananchi
Kwa ufupi
Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.
Dar es Salaam.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebomoa nyumba nne zenye thamani ya Sh800 milioni mali ya Tibe K. John zilizojengwa katika eneo la Mbezi Beach bila kibali na kinyume na sheria za mipango miji.
Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.
Wakati wa ubomoaji huo uliosimamiwa na Manispaa ya Kinondoni chini ya Mhandisi Baraka Mkuya, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki na mabomu ya machozi, wakiongozwa na Ofisa wa Operesheni, Emmanuel Tille.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata alisema kuwa ametoa agizo hilo kwa sababu sheria zinapaswa kuzingatiwa na kwamba nyumba hizo zilijengwa bila kuwa na kibali chochote cha manispaa kama inavyotakiwa.
"Kuwapo kwa kesi mahakamani hakuzuii sheria nyingine kutekelezwa, wamejenga hawana kibali," alisema Kidata.
Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.
"Anajua wazi kuwa alichokifanya ni kinyume cha sheria, ameingilia uhuru wa mahakama," alisema.
Augustino alisema hawajui watamshtaki nani ili kudai fidia, hasa kwa kuwa katibu mkuu alitoa agizo la mdomo na hakuna barua yoyote aliyoandika ambayo ingeweza kutumika kama ushahidi.
Wakili wa anayedaiwa kuwa mmiliki wa kiwanja hicho cha Janet Kiwia, ambaye ni Howard Msechu kutoka katika Kampuni ya Uwakili ya Homac, alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu walikiuka amri ya Baraza la Ardhi ya kupiga marufuku shughuli za ujenzi kuendelea.
Acha kufikiri kimasaburi wewe, hapo ccm imehusikaje?ccm ni ukoo wa panya.
Acha kufikiri kimasaburi wewe, hapo ccm imehusikaje?
Wakati mwingine tunapaswa tu kushukuru tunapopewa taarifa kama hizi. Ni fundisho tosha kwa wanaojifanya kuwa wapo juu ya sheriaKwahiyo unatuambia tufanyeje!
kwa mujibu wa ufuo Saro nyumba ni za mbunge viti maalumu Mama Rwakatare ila kaandika majina ya mtoto wake.
Nyumba nne eneo la mbezi beach ikiwamo no. 314 zilizopo ufukweni mwa bahari ya hindi zimebomolewa leo na serikali
Hata kiongoz wa dini naye anadhulumu!
Hata kiongoz wa dini naye anadhulumu!
Hongera sana serikali yangu. Mkosaji ni mkosaji tu. haijalishi hadhi yake
.....mbona umemumunya maneno????..ungesema tu ni nyumba zinazohusishwa na lile limama Lwakatare.....ambaye tayari anahusishwa na dhuluma na ufisadi....pasipokusahau biashara haramu ya watoto....Alafu anajiita mchungaji......Unafiki wa wanasiasa wetu huu..Nyumba nne eneo la mbezi beach ikiwamo no. 314 zilizopo ufukweni mwa bahari ya hindi zimebomolewa leo na serikali