Mch. Mwingira, Kakobe na Ndegi waingia choo cha kike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Mwingira, Kakobe na Ndegi waingia choo cha kike

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mr.Professional, Mar 16, 2011.

 1. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sijui inakuwaje ila nahisi ni maslahi binafsi ndo yaliowaongoza hawa wachungaji maarufu kuponda tiba ya babu na hata kuifananisha na mchezo wa upatu kama DECI. Kama hawaamini si bora kukaa kimya au kama vipi wakajaribu kwenda kupata kikombe nao.

  Biblia inasema kuwa:Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi.kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa...(Mt.7). Pia katika kitabu cha 1Wakorintho 4:5 tunaambiwa kuwa "basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

  Hawa jamaa wameona wanakosa waumini waliokuwa wanawalazimisha kutoa pesa nyingi kama sadaka pamoja na vitu vya thamani sasa wanaanza kumbwela na babu. Nadhani ni bora tuwaombee tu kwa wanayoyazungumza na kuyafundisha.
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  pure envy...! wanaogopa kupoteza waumini...! SHAME ON THEM
   
 3. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hawa akina Kakobe mbona nasikia wanatumia nguvu ya giza? Mtu yeyote anayetumia nguvu za giza huogopa sana nguvu ya kweli ya Mungu.
   
 4. m

  matunge JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Wamepotea njia. Ama kweli nyani haoni .........!, wamesahau kwamba hata wao hutoza fedha japokuwa wao huziita sadaka. Mbaya zaidi huweka michango ya aina nyingi na vipindi vingi ili wakamue fedha za waumini. Heri ya babu ameainisha kabisa kiwango ..sh. 500 tu. Wanafikiri babu asipotoza hiyo fedha ataendesha vipi kazi yake.
   
 5. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Wanamuonea donge mchungaji wa ukweli, wao nguvu zao za kuungaunga.
   
 6. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Haya makanisa ya kipentekoste nguvu zao zote huwa kwenye kuombea wajonjwa ambao kupona kwao ni "questionable". Kwa kuwa sasa amepatikana mtu ambaye atawafanya hao wagonjwa wapone KIUKWELI, ni wazi kuwa hapo nafasi yao itakuwa hatarini. Kwa kweli wanahangaika tu maana huu siyo wakati wao tena. Kwanza jiulize kitu kimoja kidogo; inakuwaje Kakobe kwa miaka yote hii na pesa zote alizokusanya iweje asiwe hata na NURSERY AU DISPENSARY? Hawa ni matapeli tu na watu wanapaswa kuamka kuwa hawa ni wahujumu wa maendeleo yao. Tuwakatae.
   
 7. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  yaah nadhan hoja hapa zinazotolewa kutoka kwa wana jf hazina mshiko. askofu kakobe amepinga anachofanya babu kwani inapingana na biblia. afu msiwe mnachukua andiko moja moja na kuleta hapa. sasa nadhan jf ishachakachuliwa. ivi kati ya ninyi wote kuna ndugu yenu kapona? maana hata rostam ndugu zake wa5 hakuna aliyepona. think u people.
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Babu Babu Babu
  Loliondo Loliondo Loliondo
  Tiba Tiba Tiba
  Kikombe Kikombe Kikombe

  TUMECHOKA NA THREAD ZA BABU KHA!!!!!!!!!!!!!
   
 9. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Umenivunja mbavu!.....ujambo lakini dada DA?
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haha, umechoka dada?

  pole sana. hapa ndio the home of great thinkers. tuvumilie tu dada wengine bado tuna madukuduku kibao na hicho kikombe.

  kama wewe umeishaelewa,tusaidie mawazo mpendwa

  stay blessed
   
 11. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Mi naamini kabisa hawa wanampango wa kwenda huko Samunge kupata kombe,lakini wanaogopa macho ya watu,waache wachlewe chelewe wakute mwana si wao!!
   
 12. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Avatar yako inanivunja mbavu!......ngoja niwapigie cim maMODZ wakupige BAN.......... haaaaa....jokes man!!!!!
   
 13. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Usiogope swahiba,mbavu zikivunjika Samunge kupo kwa babu,unaenda kuwa defragmented na unakuwa formated,yaani unakuwa scanned na cleaned papo hapo,pata kombe la uzima!!
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Sijambo mpenzi wangu mzima wewe mbona umepotea sana wajameni
   
 15. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Maana ya babu inapotea sio swala la kuchoka peke yake tu
   
 16. LD

  LD JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakati utaamua mambo!!! Mwenye kuamini aamini, asiye amini tusimlazimishe wala tusimlaumu!!! Acha tu kuna wakati utafika ukweli utajitenga na uongo.
   
 17. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Na siku hiyo nitacheka sana mi rada yangu inamscan mrema je kapona ,mbona aligwaya kunywa soda?
   
 18. k

  kapuchi Senior Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ukweli utabaki pale pale Mchungaji wa Loliondo hajafunuliwa na mungu,zile ni nguvu za kuzimu kabisa.nataka niwaambie watanzania kadiri siku zinavyoenda mtasikia ukweli lazima mungu wa kweli atamfunua kwamba ni muongo nyie subirini tu.

  hizi ni siku za mwisho watu wengi wanatekwa akili za na shetani ili waingie maagano na yeye. unapokwenda huko unapigwa chapa za kishetani na uwe tayari kucheza miziki ya kuzimu

  poleni wote ambayo macho yenu baada yako kwenye kiza kinene.
   
 19. mediaman

  mediaman Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
  Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
  Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
  Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
  Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
  Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
  Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
  Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
  Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
  Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
  Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
  Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

  Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
  Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
  Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum, kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante
   
 20. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  asante sana mediaman,

  nimeishazungumza mengi sana juu ya huyu babu na nimeanzisha na thread ya Mch. Mwasapile vs. Mch, Rwakatale. huko nimeeleza mengi sana na kufafanua hoja nyingi sana na zinazogfanana na hii yako. namshukuru Mungu kwa kuwa anaongeza sauti ya tafakari juu ya huyu babu na ndoto zake.

  ubarikiwe sana mpendwa. nakubaliana na wewe 100%

  Glory to God
   
Loading...