Mch. Mwingira, Kakobe na Ndegi waingia choo cha kike

Sijui inakuwaje ila nahisi ni maslahi binafsi ndo yaliowaongoza hawa wachungaji maarufu kuponda tiba ya babu na hata kuifananisha na mchezo wa upatu kama DECI. Kama hawaamini si bora kukaa kimya au kama vipi wakajaribu kwenda kupata kikombe nao.

Biblia inasema kuwa:Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi.kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa...(Mt.7). Pia katika kitabu cha 1Wakorintho 4:5 tunaambiwa kuwa "basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

Hawa jamaa wameona wanakosa waumini waliokuwa wanawalazimisha kutoa pesa nyingi kama sadaka pamoja na vitu vya thamani sasa wanaanza kumbwela na babu. Nadhani ni bora tuwaombee tu kwa wanayoyazungumza na kuyafundisha.
Mi nakumbuka ile kauli ya Kakobe "KANYAGA BABU WA LOLIONDO KANYAGA" hapo nimemnukuu tu. Bila shaka aungane na wenzake wakapate "Kikombe kwa Babu" kwn wanajihukumu wenyewe. ANAJIKANYAGA YEYE MWENYEWE,tena awahi kabla Elinno haijakolea kwn atakosa njia. Pumbafuuuuu sanaaaaa Kakobeiiiii!!! ATASHANGA MWENYEWE.
 
Mie namwamini babu katumwa na MUNGU kama wewe huamini basi usiende kunywa tuachie sisi tujinywee vikombe vyetu tupone, hao wakina kakobe, mwingira na kina rostam wana conflict of interest kutokana na anachokifanya babu, Mie Kakobe na Huyo Mwingira ndo wala hawaingii akilini mwangu afadhali hata ya huyu babu wa Loliondo
 
yaah nadhan hoja hapa zinazotolewa kutoka kwa wana jf hazina mshiko. askofu kakobe amepinga anachofanya babu kwani inapingana na biblia. afu msiwe mnachukua andiko moja moja na kuleta hapa. sasa nadhan jf ishachakachuliwa. ivi kati ya ninyi wote kuna ndugu yenu kapona? maana hata rostam ndugu zake wa5 hakuna aliyepona. think u people.

Wengi wametoa ushuhuda wamepona na Mrema Lyatonga ni shahidi namba 1
 
:A S-omg:Tumeshavamiwa....karibuni walitajwa kwenye kichwa cha habari
Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum, kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante
 
Wamepotea njia. Ama kweli nyani haoni .........!, wamesahau kwamba hata wao hutoza fedha japokuwa wao huziita sadaka. Mbaya zaidi huweka michango ya aina nyingi na vipindi vingi ili wakamue fedha za waumini. Heri ya babu ameainisha kabisa kiwango ..sh. 500 tu. Wanafikiri babu asipotoza hiyo fedha ataendesha vipi kazi yake.

iyo miatano yenyewe babu anaambulia mia tatu tu! Ukiangalia kazi anayofanya na anavyo jituma ukiachilia mbali umri wake. Ile kazi co ndo kuchota vkombe elfu mbili kwa cku co kdgo.
 
Apa waumini tuko kwenye wakati mgumu kuelewa nani wa kumwamini either kakobe au babu apa ningeshauri viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kuomba MUNGU. Kutuonyesha njia iliyobora.
 
asante sana mediaman,

nimeishazungumza mengi sana juu ya huyu babu na nimeanzisha na thread ya Mch. Mwasapile vs. Mch, Rwakatale. huko nimeeleza mengi sana na kufafanua hoja nyingi sana na zinazogfanana na hii yako. namshukuru Mungu kwa kuwa anaongeza sauti ya tafakari juu ya huyu babu na ndoto zake.

ubarikiwe sana mpendwa. nakubaliana na wewe 100%

Glory to God

Acheni kuwa wanafiki nyinyi na katika thread yako nilikuuliza ili nisikuone mnafiki sema unasali kanisa gani na nani aliyekutuma kuja humu kumkosoa babu wewe na mwenzako Mediaman? kama kweli nyinyi mnauwezo na Mungu wenu kawafunulia na kuwaonesha ile tiba ya babu ni feki basi fungeni kwa maombi na mikemee ili isiendelee zaidi ya hapo nawaona kama watu mnaotafuta umaarufu usio na maana kama mnaweza nendeni mpaka Arusha mkaipinge na kukemea kabisa sio mmekaa kwenye keyboard zenu mnaanza kuleta porojo zisizo na mashiko hatutaki kuwasikia na tumewachoka kama vp nendeni pale Ubungo mkahubiri watu wasinde loliondo.... zaidi ya hapo mimi nitawaona kama wale wenzenu masabato masalia waliotaka kwenda ulaya bila visa wala ticket matokeo yake waliisha Ukonga. shame on You acha watu wapate uponyaji maana huko kanisani kwenu mmewakamua pesa zao mpaka wamekosa imani na nyinyi
 
Apo ndo utakapoona tofauti kati ya wafanyabiashara kupitia mgongo wa dini na wanaoneza dini.
Nakumbuka ata Yesu aliletewa report na mitume kuwa kuna watu wanaponya kwa jina lako tukawakataza,Yesu alingaka na kuwakemea mitume kuwa wasingeliwakataza as wanaponya kwa jina lake.
Sasa ninyi akina Kakobe na wenzio ni akina nani mpaka kuanza kumponda Babu
 
Huyu Babu wa Loliondo kwakuwa amemhusisha Mungu kwenye tiba yake inabidi tutumie pia Neno la Mungu kupima iwapo anayosema au anayoyafanya ni ya kweli au la. Baada ya kuchunguza Neno la Mungu kwa makini mimi nionavyo uponyaji wa Babu huyo hautokani na Mungu kwa misingi hii.
Kwanza: Mungu kwa njia ya Yesu Kristo anaponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Watanzania hawasumbuliwi na magonjwa hayo manne tu? Wengine wana mafua yasiyopona, wengine wana majipu ya muda mrefu. Wengine wana magonjwa mabaya ya ngozi nk. Ingekuwa ni Mungu amemtuma, angemwambia aponye magonjwa yote. Yesu alipokuwa hapa duniani aliponya maradhi yote.
Pili: kitendo cha kusema kwamba ni yeye tu Babu mwenye uwezo wa kufanya dawa hiyo iponye magonjwa sio cha kibiblia. Biblia inasema "na ishara hizi(uponyaji ukiwemo) zitafuatana na kila aaminiye..."
Tatu: Yesu alisema "Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa nao watapata afya" Sio mtawapa kikombe na kuwaombea.
Nne: Kitendo cha kuuza dawa hiyo sio cha kibiblia. Maadam anasema amepewa uwezo huo na Mungu basi hapaswi kuuza uponyaji huo hata kwa shilingi moja. Na kama lengo ni kupata pesa hizo ili kuwapa wasaidizi wake kwanini iwe sh. 500 tu? Shilingi 500 zinafaa nini katika hali ngumu ya maisha waliyo nayo Watanzania leo?
Tano: Mungu anapowaponya watu anawaambia pia waache dhambi. Yesu alimwambia yule aliyemponya "Usitende dhambi tena lisije likakupata lililo baya zaidi kuliko hilo" Huyu Babu anawapa watu dawa tu bila kuwaambia waache ufisadi, rushwa, ujambazi...wakipona si ndio wataendelea kufanya madhambi hayo kwa nguvu zaidi? Mungu hawaponyi watu ili waendelee kufanya dhambi.
Sita: Kama hiyo dawa inaponyesha kwa imani, kwanini anaichemsha kwanza? Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Saba: Babu anadai kwamba dawa hiyo inaponyesha kwa imani. Mbona basi watu wanapotaka kujichukulia dawa hiyo anawaambia kwamba hawatapona? Yule mama (katika Biblia) aliyekuwa anatokwa damu aligusa upindo wa vazi la Yesu akapona kwa imani. Lakini huyu Babu hataki mtu ajichukulie kikombe mwenyewe hata kama anayo imani.
Nane: Watu wanapotaka kumpa huyu Babu sadaka(magari, nyumba), kwanini anakataa? Wana wa Lawi (katika Biblia) waliambiwa watakula madhabahuni. Sadaka zilipotolewa hawakukataa.
Tisa: Mungu akiponya, uponyaji wake hauwi nusu nusu. Kitabu cha Agano Jipya kinaeleza wazi jinsi watu walivyoponywa kwa ukamilifu magonjwa yao. Kwanini basi katika hao walioenda kwa Babu baadhi yao wanasema kwamba wanajisikia nafuu badala ya kusema wamepona kabisa?
Kumi: Mtumishi wa Mungu ni mtiifu. Mungu anapomwambia jambo anatii. Huyu kama Mungu alimwambia atumie dawa hiyo tangu mwaka 1991 kwanini amempinga Mungu kwa miaka 20? Ni watu wangapi wamekufa kwa magonjwa muda huo wote. Kwanini amekuwa mbishi muda huo wote? Ana huruma kweli na wagonjwa? Mungu hapendezwi na watu wasiomtii.Yona katika Biblia alipoambiwa aende Ninawi alikataa. Kilichompata ni kumezwa na Nyangumi.Kwa msingi huo siamini kwamba Mungu ndiye aliyemwambia atumie dawa hiyo. Vinginevyo Mungu asingemvumilia kwa miaka hiyo yote huku Watanzania wanaendelea kuangamia kwa magonjwa.
Mwisho, najiuliza: Yesu alipokuwa hapa duniani mbona hakuponya watu kwa kuwapa magamba ya miti, majani ya miti nk. Alisema neno tu na magonjwa yakatoweka. Ina maana mti huo utakapokwisha Loliondo na uponyaji ndio utaishia hapo?

Nikiangalia pia Maandiko Matakatifu naona kuwa walikuwepo watu waliosema Mungu amewatuma kufanya hivi au vile na kumbe ni uongo. Biblia pia inasema juu ya "mungu"(wa herufi ndogo)wa dunia hii. Naye anatenda ishara na miujiza. Wakati wa Musa, kule Misri, Musa, Mtumishi wa Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa na waganga na wachawi wa Misri wakati huo nao wakafanya ishara kama hizo. Na hata waganga wa kienyeji nao pia husema kwamba wanaponya kwa uwezo wa mungu.
Maandiko Matakatifu yanatueleza pia kwamba nyakati za mwisho(naamini hizi ni nyakati za mwisho maana ishara alizozitaja Yesu zimetimia) watatokea manabii wengi wa uongo na kuwadanganya wengi.
Mwisho kabisa nawashauri wamiliki wa Jamii Forum, kama inawezekana muandae mdahalo katika redio au televisheni(mdahalo huo muudhamini ninyi)na kisha muwaombe wale wanaomuunga mkono huyo Babu waje wajieleze katika mdahalo huo na wale wanaompinga Babu kama Mch Mwingira, Askofu Kakobe, Rostam nk nao wawepo kwenye mdahalo huo. Nadhani hiyo itakuwa nafasi nzuri ya watu hao kujieleza vizuri na wananchi wapewe nafasi ya kupiga simu na kuwauliza maswali ili umma wa Watanzania upate kujua ukweli na undani wa jambo hili. Huu ni wakati wa ukweli na uwazi. Asante

Mkuu hili bandiko umelirudia zaidi ya mara 3 na nimeona mpaka thread yako au na wewe kakuoyesha hili andiko maana mpaka limechuja kila sehemu una copy na ku paste tu vp hoja zimekuishia??
na kama wewe ni mtu wa rohoni ilikuwa haina haja ya kubandika post lako ungepiga magoti na kumwomba Mungu akupe solution sio unakuja hapa na mawazo yako ambayo ni uchwara na kutaka utuaminishe.... huna tofauti na wale waimba mipasho maana umeleta mipasho hapa

na wewe umeingia choo cha kike
 
Back
Top Bottom