Mch. Gwajima asifu utendaji wa Magufuli, Dr Slaa ampongeza Gwajima

uko sawa mkuu, upinzani tuliouzoea huu sio wakati wake. Hata kupinga yanayofaa sio kosa, ila upunge yanayofaa kwa kutuonyesha yele yanayofaa zaidi. Yawezekana jambo linafaa lakini lafanyika na mtu asiyefaa/spidi kali sana isiyona ufanisi/lafaa leo lakini kesho litakuwa na madhara/lafaa lakini linafanyika katika muda usio sahihi/ lafaa lakini lisipofanyika litasababisha kufanyika mengine mengi ambayo faida au kufaa kwake ni kukubwa zaidi.

Hapa ndio maana wapinzani wanapaswa kuupdate opposition style yao. Zama za umaarufu wa kashfa zimepita, leo utakuwa maalufu kwa uwezo wako wa kuinyoosha serikali katika njia bora. Kashfa wawili tu wameonyesha wanaweza kudeal nazo japo kwa hatua ya awali.

Umenena vema mkuu. LIKE
 
"Mhe Magufuli hayo unayo yafanya ndio watanzania tumekuwa tukiyapigia kelele miaka yote na tukaonekana wabaya. Tuko sambamba na wewe tunakuunga mkono safisha nchi.. usilegeze upanga wako wala usijali vitisho vyao. Tunakuombea ushujaa zaidi na roho ya Mungu iwe nawe"

Sehemu ya mahuburi yake leo Jumapili kanisani kwake

Km sio uongo lete sauti, au video ndo tukuamini
 
Huyo nae! Magu atamtembelea pale alipo. Anajisogeza sogeza wakat ana scandal kibao. Magu haongeki kwa pesa wala maneno.
Kwa hiyo Gwajima kama ana jipu atulie litatumbuliwe kwa wakati wake..Teh Teh Teh...
 
Kama ni kweli kafanya hivyo, basi hili litakuwa chungaji malaya sana. Linisamehe tu. Watumishi wa Mungu aliye hai, jifunzeni hapo. Usijifiche mvua kwenye mgongo wa mwanasiasa. Utaaibika tuu.
Kote anajikomba atii TRA wasimfuatilie. Ajue kuwa, sasa ndo kafungulia mbwa. Amulikwe
 
Ukizungumzia katiba ya wananchi mnamwita mzalendo.Akikemea maovu wengi mnamsifu.?kipongeza mazuri mnamwita MNAFIKI. Jamani watanzania tujifunze kuwa na heshima kwa wengine.Gwajima ni mtanzania,Magufuli ni Rais wake,kwanini asimpongeze?
 
Aache unafiki yeye abaki na mafisadi wenzake...kama ana makontena ya kimagumashi ajiandae

Acha zako, Gwajima ni mtanzania na ana haki ya kumsifu, ukumbuke Rais hushinda kwa wingi wa kura, zaidi ya asilimia 40 hawakumchagua, Lakini sasa wanampenda na kumshukuru Mungu kuliko waliomchagua, kwa kuwa waliotaka upinzani walikerwa na ccm na kwa kuwa JPM amejitofautisha basi ujue ni wapinzani watakaompenda zaidi kuliko Wana ccm.

Ninyi msiompenda ndio mnazungumzia bado uchama, u ccm na makundi, ambayo hata JPM amesema wakati wa kampeni umekwisha. Sasa hapa kazi tu, JPM ni Rais wa watanzania wote, mimi pia si kumchagua, lakini nampenda sasa kuliko unavyompenda, hapo hakuna sheria
 
Mkuu hili litakuwa ni kosa la kihistoria. nchi yetu ipo katika critical juncture. Tumeanza kuona mwangwi wa kile tulichokiihitaji tangu enzi za mkwawa.

Magufuli wakati huu anahitaji constructive upinzani mkali sana kuliko siku zote za historia ya taifa hili.

Kwa ufupi ili rocket iondoke ivuke critical velocity (where above it there is no gravitational force) inahitaji strong opposite force.

Na hii inahitajika sana leo tanzania kuliko wakati wowote. Nahuzunika sana kama wapinzani watasinyaa na kujisalimisha kwa magufuli.

We need strongest creative oppositions in this country today than ever.

Mtu mwenye majipu tatizo sio Majipu ni Damu ndio imechafuka. Nani wa kumuonyesha magufuli kuwa tunapaswa kudeal na damu ili majipu yasiote tena. Dawa ni nini,

KWA UFUPI, newtons second law of motion.

safi sana tunasubiria bunge lianze magufuli na ccm yake tuzidi kuwatikisa
 
gwajima ashasoma alama za nyakati hapo anatafuta pakuibukia
 
"Mhe Magufuli hayo unayo yafanya ndio watanzania tumekuwa tukiyapigia kelele miaka yote na tukaonekana wabaya. Tuko sambamba na wewe tunakuunga mkono safisha nchi.. usilegeze upanga wako wala usijali vitisho vyao. Tunakuombea ushujaa zaidi na roho ya Mungu iwe nawe" Sehemu ya mahuburi ya Mch.Gwajima leo Jumapili kanisani kwake.
 
Mimi in Mkristo, Gwajima kiimani ni baba. Namuuliza maana nina uhakika kywa kama siyo yeye wa kanisani kwake wanaoita humu. Je unabii wake ulitoka kwa MUNGU baba wa BWANA na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareth?
 
Mimi in Mkristo, Gwajima kiimani ni baba. Namuuliza maana nina uhakika kywa kama siyo yeye wa kanisani kwake wanaoita humu. Je unabii wake ulitoka kwa MUNGU baba wa BWANA na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareth?

Akasemaje mkuuu
 
Gwajima kamtosa rasmi Lowassa daah!! Lowassa mpaka leo hamtambui Dr.Magufuli kama rais Gwajima anamtumbua Dr.Magufuli kama rais wa Tanzania.
 
Gwajima alimkimbia Lowassa siku aliposhindwa Urais, na matokeo yake, kala malimau yote mwenyewe
 
Namimi nawauliza je, unabii wa Gwajima umetoka kwa Mungu ama kwa wanadamu? Naomba mnijibu
 
Kuwe na ubongo bana nyie humu siyo watoto pili elewe uchaguzi umeisha gwajima in mchungaji na anakanisa anawaumini zaidi ya miatano sasa unataka kwenye uhalisia alete siasa?
 
Back
Top Bottom