Mch. Gwajima asifu utendaji wa Magufuli, Dr Slaa ampongeza Gwajima

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
"Mhe Magufuli hayo unayo yafanya ndio watanzania tumekuwa tukiyapigia kelele miaka yote na tukaonekana wabaya. Tuko sambamba na wewe tunakuunga mkono safisha nchi.. usilegeze upanga wako wala usijali vitisho vyao. Tunakuombea ushujaa zaidi na roho ya Mungu iwe nawe"

Sehemu ya mahuburi yake leo Jumapili kanisani kwake.

Maoni yangu: Dhima ya Tamko la wananchi ni Maendeleo. Akitokea kiongozi anayesafisha nchi kwa maslahi ya wananchi na wewe ukamtukana na kuponda bidii yake hufai .. Binafsi hata chama ulichopo I better put my step away.

Tukubaliane nchi hii vasco aliifanya jalala. mimtu kama kamanda Kova imejifanyia kila wakitakacho kwa maslahi yao na matumbo yao. Nani asiyejua Afande Kova ni BILIONEA? Utajiri wake kautoa wapi..kama atapinga akane hadharani ili account zake nje ya nchi watu wajibinafsishie..

Magufuli kaanza vizuri, Tumpatie support ili abonyeze tu hawa kina kova, kina Riziwani mabilionea mbona zitawabana tu. Ila tusipo toa support wallah yatammeza.

Upinzani wanatakiwa kujua Magu anaangusha dola ya majizi ya pesa ambayo hayo hayo ndiyo yaliyokuwa majizi ya kura. Upinzani usipomsuport watakuwa wamelogwa, majizi yatanenepa na sahauni uchaguzi wa kidemokrasia nchi hii..

Magu anazitimiza sera za Ukawa.. why blaming? I'm..fine, may be he can change baadae.. basi ni hapo atapo change but if he still in this move why tusimsuport?? Mafisadi yanataka tumshambulie akose hewa aachane na mafisadi.. Hapo mtaisoma namba foreva.

=================


Dr Slaa tuache. Ulishapewa urithi wako wa nchi hii. Kula zako baba kula unenepe Tuache sisi tuko Tz wewe kula zako Bata huko Canada. Tuache na nchi Yetu, Tuache tufanye Yetu, wewe huna fungu na watu wa nchi hii. Ulishatutupa, ulishatuacha, kwaheri baba kwaheri kula nenepa tesa take your time TUACHE.. Gwajima tunae, yuko nasi, hajatoroka wala kutuacha yatima, anakula na kuteseka pamoja nasi, hakuna mzalendo kwenye nchi hii kama yeye. Wewe na Mwanakijiji kuleni maisha .sisi tumegandana na nchi hii..

Wewe umesaliti Demokrasia ya nchi hii, umesaliti haki na tumaini la watu kwa vipande vya Fedha.. Nakwambia HUTAKUWA NA FURAHA HUKO NJE HATA CHEMBE. tuachie Magufuli, Lowassa, Mbowe, Gwajima.. tuachie watu wetu tufanye yetu.. wewe starehe zako UONE kama utapata amani.
 
Hongera sana Uncle kwa kusema ukweli na kuamua kumuunga mkono Magufuli! Sasa tujenge nchi bila kusahau kutii sheria bila shuruti!

Magufuli ni Rais wa watanzania wote na sote tunapaswa kumuunga mkono na ninakuomba umshawishi Lowasa atoe tamko la kumuunga mkono maana anatenda yaliyo mema kwa nchi yetu!
 
Kama Dr. JPM ataendelea hivi mpaka kutimiza 100 siku akiwa ikulu basi kuna wakati wanasiasa wa upinzani watatamka wazi kuwa naye bega kwa bega, otherwise sidhani..!
 
Aache unafiki yeye abaki na mafisadi wenzake...kama ana makontena ya kimagumashi ajiandae
 
Kama Dr. JPM ataendelea hivi mpaka kutimiza 100 siku akiwa ikulu basi kuna wakati wanasiasa wa upinzani watatamka wazi kuwa naye bega kwa bega, otherwise sidhani..!

Mkuu hili litakuwa ni kosa la kihistoria. nchi yetu ipo katika critical juncture. Tumeanza kuona mwangwi wa kile tulichokiihitaji tangu enzi za mkwawa.

Magufuli wakati huu anahitaji constructive upinzani mkali sana kuliko siku zote za historia ya taifa hili.

Kwa ufupi ili rocket iondoke ivuke critical velocity (where above it there is no gravitational force) inahitaji strong opposite force.

Na hii inahitajika sana leo tanzania kuliko wakati wowote. Nahuzunika sana kama wapinzani watasinyaa na kujisalimisha kwa magufuli.

We need strongest creative oppositions in this country today than ever.

Mtu mwenye majipu tatizo sio Majipu ni Damu ndio imechafuka. Nani wa kumuonyesha magufuli kuwa tunapaswa kudeal na damu ili majipu yasiote tena. Dawa ni nini,

KWA UFUPI, newtons second law of motion.
 

We must learn to accept good job. Upinzani sio ukinzani
 

Kama Gwajima ameanza kujitambua basi asamehewe yale makwarukwaru yake na ajirudi sasa.
 

amekwishaa lamba ndim kwanza
hata na hivyo yeye ni mmoja ya jipu linalotakiwa kutumbuliwa
 
Aache unafiki yeye abaki na mafisadi wenzake...kama ana makontena ya kimagumashi ajiandae
Wewe ndo mnafiki na fisadi unayetaka kujivika u ccm ili ufiche maovu yako. Pombe John Magufuli siyo Rais wa Ccm ila ni Rais wa Watanzania.
 

Definetelly that would be ACT-Wazalendo ( Refer bold purple in ur comment)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…