MCCM: Kikwete Acha Kucheza Mdundiko

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Aliyosema Nyerere yaanza kutokea

picture-10.jpg

Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 10 November 2010

Jamvi la Weledi

WAKATI wa uhai wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tulisikia mengi ambayo sasa tunayakumbuka.

Nikiwa kijana wa Umoja wa Vijana – Tanu Youth League – na baadaye Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), nilishiriki uongozi wa vijana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutunga na kufundishwa nyimbo zilizochochea uzalendo kwa vijana.

Naukumbuka wimbo mmoja uliosema, "Alisema, alisema,
Alisema Nyerere alisema,
Vijana wangu wote mmelegea,
Sharti muanze mchakamchaka…"

Nalazimika kuukumbuka wimbo huo kutokana na yaliyotokea ndani ya chama chetu wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika wiki iliyopita.

Matokeo ya uchaguzi huu, bila shaka yameshangaza wengi akiwamo mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete ambaye alituahidi ushindi wa kishindo. Ni kwa sababu, ameibuka na "ushindi kiduchu" na almanusura kura zisingetosha.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, wapigakura wachache sana wamejitokeza katika vituo vya kupigiakura; huku vyama vya upinzani vikipata kura nyingi mijini na vijijini.

Kwa wiki kadhaa sasa, watu mbalimbali wakweli kwa waongo, watajikita kuchambua mambo haya, lakini mimi leo napenda nijadili dhana ya "Alisema Nyerere."

Ni ukweli ulio wazi kuwa yaliyotokea ndani ya chama chetu yalitarajiwa, na baadhi ya watu walionya pasipo kusikilizwa. Mwenyekiti wetu na marafiki zake kwa sasa wanadai hali hii imesababishwa na mpasuko uliotokea wakati wa kura za maoni.

Mtazamo huu hauna ukweli wowote kwa sababu hata pale ambapo CCM iliteua wagombea walioshinda kikweli katika kura za maoni, bado upinzani umekuwa mkubwa na baadhi ya majimbo kwenda upinzani.

Kigezo cha kura za maoni si kipimo pekee cha matokeo mabaya ya CCM katika uchaguzi uliomalizika.

Nasema matokeo mabaya kwa sababu, CCM imeshuka chini kwa asilimia 20 ukilinganisha na matokeo ya 2005, wakati wapinzani wamepanda kwa asilimia 22 katika kipindi hicho.
Ndani ya CCM, kwa takribani miaka mitano, wapo waliosema kama Mwalimu na wanastahili kuimbwa kama alivyoimbwa lakini hawakusikilizwa.

Mathalani tunaweza kuimba waliosema na kwa ufupi ni hawa hapa: Joseph Butiku, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Matheo Qares, Juma Nkhangaa, John Malecela, Joseph Warioba, Hassy Kitine, Phillip Mangula, Salim Ahmed Salim, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Harrison Mwakyembe, Christopher Sendeka.

Baadhi yao walisema ndani ya vikao vya chama na Watanzania wengi hawakuwasikia. Lakini wachache wao, walisema hata nje ya vikao kwa nia njema, Watanzania wakawasikia, lakini wakaishia kuitwa majina mabaya na kuambuliwa kejeli nyingi.

Wengine walisema na kukosoa chama hadharani, lakini wakazibwa midomo kwa kupewa vyeo na kuteuliwa katika nyadhifa kadhaa.

Wapo walioandika na kuweka rekodi katika historia, lakini hawakujibiwa na wala maandiko yao hayakujadiliwa. Chama chetu kikaasisi utamaduni mpya wa kudharau maoni ya wanachama wake na kuwaona kama maadui wa chama hicho.

La ajabu ni kwamba, wapinzani waliorejea CCM baada ya kukidhalilisha chama kwa miaka mingi, wakasikilizwa na kuheshimika sana ndani ya chama.

Watu hawa wakapewa nyadhifa kubwa ndani ya serikali na chama na kutumika hata kuwanyamazisha viongozi wastaafu na wanachama waaminifu wa CCM.

Marafiki wa chama wakawa ni wale wanaotoa fedha za kukiendesha chama kwa jinsi wao wanavyotaka. Nguvu ya fedha ikachukua nafasi ya nguvu ya uadilifu kama msingi wa kuongoza chama.

Wahenga walisema, "Mkataa pema, pabaya panamwita." Mtandao wa mwenyekiti wetu ulikuwa na nguvu ya kukataa ushauri na maoni mema ya wazee, lakini haukuwa na nguvu ya kukataa matokeo ya ukaidi huo.

Chama chetu sasa kinakataliwa sehemu nyingi nchini. Ukienda mikoa ya pembezoni mwa nchi hali imebadilika sana na si sahihi kudhani hii ni kwa sababu ya kura za maoni au nguvu ya Dk. Willibrod Slaa.

Chama chetu kilipoacha misingi yake ya kiutu na utetezi wa wanyonge wa taifa, kimesababisha kukataliwa na wananchi walio wengi.

Katika kila makao makuu ya mkoa isipokuwa Singida mjini, CCM imepata taabu sana kukubalika na imebidi kutumia njia "chafu" ili kuibuka na ushindi unaohojiwa.
Mabadiliko haya haraka yanahitaji maelezo ya kina, lakini wenye kuitakia mema CCM tayari wanasema, uzembe na woga wa kushughulikia masuala mazito hapa nchini ndio umepelekea CCM kukataliwa na watu wa mijini na vijijini.

Hata mijini na vijijini, wapinzani wameonekana mashujaa kuliko wabunge wa CCM.
Kwa kweli, niseme wazi kuwa baadhi yetu tulitamani sana wapinzani washinde zaidi ya walivyoshinda ili tupate nafasi pana zaidi ya kukikosoa chama chetu. Walio wakali zaidi, walikuwa tayari kumpoteza hata mwenyekiti wetu ili liwe fundisho kwa viongozi wajao.

Kwenye CCM ya Nyerere, ushindi huu mdogo wa chama na mgombea wake, ungesababisha baadhi ya watu kuwajibika ili kuleta heshima mbele ya jamii. Lakini kwa Jakaya Kikwete hilo ni gumu kufanyika, labda kutokana na kafara katika ngazi za chini badala ya kushughulikia masuala ambayo chama kimeshindwa kuyashughulikia.

Kana kwamba lililotokea halitoshi, tayari tunaona watu wanachukua fomu za kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri bila kujali tuhuma za watu kuhusu uhusika wao katika kipigo cha chama katika uchaguzi.

Ili kurejesha heshima ya chama chetu, tunamhitaji Kikwete tofauti na huyu aliyemaliza muda wake. Kikwete mpya anahitaji kubadilika.

Anahitaji kuwa msikivu si kwa wasaidizi na washauri wake, bali kwa watu wanaoweza kumwambia ukweli bila kuhofia kupoteza nafasi zao.

Kikwete mpya anahitaji kuvua joho la uswahiba wa mtandao na kuvaa umakini na uchungu kwa taifa lake na watu wake ambao wametopea katika lindi la umaskini. Anahitaji kuwa wazi, mkweli ili kurejesha heshima ya ikulu machoni mwa wananchi.

Anatakiwa kukataa kinachodaiwa kuwa miradi ya giza anayopewa na kuandaliwa na marafiki zake kwa kisingizio cha kuwa "hata rais ana maisha binafsi."

Katiba yetu inamhakikishia ulinzi na matunzo rais mstaafu kwa hiyo aepukane kabisa na miradi yenye harufu ya kifisadi inayoweza kuanzishwa na watu wanaodai kuwa wako karibu naye.

Si vema kumwona rais anahangaika na kukutana na mameneja wake wa biashara na wawekezaji binafsi. Hali hii itamletea utumwa na kigugumizi cha kushughulikia ufisadi.

Kikwete apunguze safari za nje zisizo na tija. Aachane na tabia ya kuonekana mcheza "midundiko." Ni vema Kikwete akajua kuwa hoja nyingi za wapinzani zimekubalika kwa wananchi kutokana na kuonekana ni makini na wana uchungu na taifa.

Chanzo: Mwanahalisi Novemba 10, 2010.
 
Wananchi wengi sasa wanataka 'vidole juu' na 'pipooooooooooooz..........'. Wamechoka na kidumu chama cha .....
 
If I can ask....Do u think hayo uliyoyaandika hapo Kikwete hayajui???? Sikatai kuwa Jk has been within the system since then, lakini anavyoendesha kampeni n dhahiri gharama zake ni kubwa kuliko hata kipato cha chama....sasa hizo fedha anatoa nani??? obvious kuna mtu au kikundi cha watu kinachotoa fedha kwa kuendesha shughuli za chama......na huyo mtu au kikundi cha watu ndo kinachomdrive JK.....may b hao jamaa waliotoa wana ushahidi wa machafu yalitendwa na JK kwa nini asiwaogope???? kwa nini asifanye watakalo????

First thing comes first, Siasa ya Bongo ni Biashara...so now watu wanataka FAIDA.......Faida hii haitopatikana bila fake dealz na mikataba mibovu na koz JK ni wao na siom wetu then atairidhia.....then sisi tutaendelea kuwa masikini mpk KUFA kwetu....

I DONT EXPECT ANY CHANGES BRO' .................
 
mwammsheni mwambie ule mchango wa hiari aliopata kwa waingiza mafuta nchini sasa tayari wamepandisha mafuta mpaka 1,800 awaite awaaombe wapungze basi la sivyo watu wataanza kumpigia kelele:A S angry:
 
Aliyosema Nyerere yaanza kutokea

picture-10.jpg

Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 10 November 2010

Jamvi la Weledi

WAKATI wa uhai wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tulisikia mengi ambayo sasa tunayakumbuka.

Nikiwa kijana wa Umoja wa Vijana – Tanu Youth League – na baadaye Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), nilishiriki uongozi wa vijana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutunga na kufundishwa nyimbo zilizochochea uzalendo kwa vijana.

Naukumbuka wimbo mmoja uliosema, “Alisema, alisema,
Alisema Nyerere alisema,
Vijana wangu wote mmelegea,
Sharti muanze mchakamchaka…”

Nalazimika kuukumbuka wimbo huo kutokana na yaliyotokea ndani ya chama chetu wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika wiki iliyopita.

Matokeo ya uchaguzi huu, bila shaka yameshangaza wengi akiwamo mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete ambaye alituahidi ushindi wa kishindo. Ni kwa sababu, ameibuka na “ushindi kiduchu” na almanusura kura zisingetosha.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, wapigakura wachache sana wamejitokeza katika vituo vya kupigiakura; huku vyama vya upinzani vikipata kura nyingi mijini na vijijini.

Kwa wiki kadhaa sasa, watu mbalimbali wakweli kwa waongo, watajikita kuchambua mambo haya, lakini mimi leo napenda nijadili dhana ya “Alisema Nyerere.”

Ni ukweli ulio wazi kuwa yaliyotokea ndani ya chama chetu yalitarajiwa, na baadhi ya watu walionya pasipo kusikilizwa. Mwenyekiti wetu na marafiki zake kwa sasa wanadai hali hii imesababishwa na mpasuko uliotokea wakati wa kura za maoni.

Mtazamo huu hauna ukweli wowote kwa sababu hata pale ambapo CCM iliteua wagombea walioshinda kikweli katika kura za maoni, bado upinzani umekuwa mkubwa na baadhi ya majimbo kwenda upinzani.

Kigezo cha kura za maoni si kipimo pekee cha matokeo mabaya ya CCM katika uchaguzi uliomalizika.

Nasema matokeo mabaya kwa sababu, CCM imeshuka chini kwa asilimia 20 ukilinganisha na matokeo ya 2005, wakati wapinzani wamepanda kwa asilimia 22 katika kipindi hicho.
Ndani ya CCM, kwa takribani miaka mitano, wapo waliosema kama Mwalimu na wanastahili kuimbwa kama alivyoimbwa lakini hawakusikilizwa.

Mathalani tunaweza kuimba waliosema na kwa ufupi ni hawa hapa: Joseph Butiku, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Matheo Qares, Juma Nkhangaa, John Malecela, Joseph Warioba, Hassy Kitine, Phillip Mangula, Salim Ahmed Salim, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Harrison Mwakyembe, Christopher Sendeka.

Baadhi yao walisema ndani ya vikao vya chama na Watanzania wengi hawakuwasikia. Lakini wachache wao, walisema hata nje ya vikao kwa nia njema, Watanzania wakawasikia, lakini wakaishia kuitwa majina mabaya na kuambuliwa kejeli nyingi.

Wengine walisema na kukosoa chama hadharani, lakini wakazibwa midomo kwa kupewa vyeo na kuteuliwa katika nyadhifa kadhaa.

Wapo walioandika na kuweka rekodi katika historia, lakini hawakujibiwa na wala maandiko yao hayakujadiliwa. Chama chetu kikaasisi utamaduni mpya wa kudharau maoni ya wanachama wake na kuwaona kama maadui wa chama hicho.

La ajabu ni kwamba, wapinzani waliorejea CCM baada ya kukidhalilisha chama kwa miaka mingi, wakasikilizwa na kuheshimika sana ndani ya chama.

Watu hawa wakapewa nyadhifa kubwa ndani ya serikali na chama na kutumika hata kuwanyamazisha viongozi wastaafu na wanachama waaminifu wa CCM.

Marafiki wa chama wakawa ni wale wanaotoa fedha za kukiendesha chama kwa jinsi wao wanavyotaka. Nguvu ya fedha ikachukua nafasi ya nguvu ya uadilifu kama msingi wa kuongoza chama.

Wahenga walisema, “Mkataa pema, pabaya panamwita.” Mtandao wa mwenyekiti wetu ulikuwa na nguvu ya kukataa ushauri na maoni mema ya wazee, lakini haukuwa na nguvu ya kukataa matokeo ya ukaidi huo.

Chama chetu sasa kinakataliwa sehemu nyingi nchini. Ukienda mikoa ya pembezoni mwa nchi hali imebadilika sana na si sahihi kudhani hii ni kwa sababu ya kura za maoni au nguvu ya Dk. Willibrod Slaa.

Chama chetu kilipoacha misingi yake ya kiutu na utetezi wa wanyonge wa taifa, kimesababisha kukataliwa na wananchi walio wengi.

Katika kila makao makuu ya mkoa isipokuwa Singida mjini, CCM imepata taabu sana kukubalika na imebidi kutumia njia “chafu” ili kuibuka na ushindi unaohojiwa.
Mabadiliko haya haraka yanahitaji maelezo ya kina, lakini wenye kuitakia mema CCM tayari wanasema, uzembe na woga wa kushughulikia masuala mazito hapa nchini ndio umepelekea CCM kukataliwa na watu wa mijini na vijijini.

Hata mijini na vijijini, wapinzani wameonekana mashujaa kuliko wabunge wa CCM.
Kwa kweli, niseme wazi kuwa baadhi yetu tulitamani sana wapinzani washinde zaidi ya walivyoshinda ili tupate nafasi pana zaidi ya kukikosoa chama chetu. Walio wakali zaidi, walikuwa tayari kumpoteza hata mwenyekiti wetu ili liwe fundisho kwa viongozi wajao.

Kwenye CCM ya Nyerere, ushindi huu mdogo wa chama na mgombea wake, ungesababisha baadhi ya watu kuwajibika ili kuleta heshima mbele ya jamii. Lakini kwa Jakaya Kikwete hilo ni gumu kufanyika, labda kutokana na kafara katika ngazi za chini badala ya kushughulikia masuala ambayo chama kimeshindwa kuyashughulikia.

Kana kwamba lililotokea halitoshi, tayari tunaona watu wanachukua fomu za kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri bila kujali tuhuma za watu kuhusu uhusika wao katika kipigo cha chama katika uchaguzi.

Ili kurejesha heshima ya chama chetu, tunamhitaji Kikwete tofauti na huyu aliyemaliza muda wake. Kikwete mpya anahitaji kubadilika.

Anahitaji kuwa msikivu si kwa wasaidizi na washauri wake, bali kwa watu wanaoweza kumwambia ukweli bila kuhofia kupoteza nafasi zao.

Kikwete mpya anahitaji kuvua joho la uswahiba wa mtandao na kuvaa umakini na uchungu kwa taifa lake na watu wake ambao wametopea katika lindi la umaskini. Anahitaji kuwa wazi, mkweli ili kurejesha heshima ya ikulu machoni mwa wananchi.

Anatakiwa kukataa kinachodaiwa kuwa miradi ya giza anayopewa na kuandaliwa na marafiki zake kwa kisingizio cha kuwa “hata rais ana maisha binafsi.”

Katiba yetu inamhakikishia ulinzi na matunzo rais mstaafu kwa hiyo aepukane kabisa na miradi yenye harufu ya kifisadi inayoweza kuanzishwa na watu wanaodai kuwa wako karibu naye.

Si vema kumwona rais anahangaika na kukutana na mameneja wake wa biashara na wawekezaji binafsi. Hali hii itamletea utumwa na kigugumizi cha kushughulikia ufisadi.

Kikwete apunguze safari za nje zisizo na tija. Aachane na tabia ya kuonekana mcheza “midundiko.” Ni vema Kikwete akajua kuwa hoja nyingi za wapinzani zimekubalika kwa wananchi kutokana na kuonekana ni makini na wana uchungu na taifa.

Chanzo: Mwanahalisi Novemba 10, 2010.

Kaka JK hayo yote anayajua na kwake mafundisho ya mwalimu nyerere yamekufa.Chama cha CCM sasa kimekuwa ni chama cha Mafisadi na wafanya biashara badala ya Wakulima na Wafanyakazi.Hivyo mwache amalizie kucheza mdundiko miaka hii 5 iliyobaki kisha tutafute viongozi wenye maadili watuongozee inchi.
 
Duh..!
Mkuu miaka 5 hii nchi si itakuwa imesambaratika kabisaa..kwa mwenendo huu inatisha kwa kweli.
I can't wait anymore to witness the disaster..seriously, we are required to ponder over the way forward
 
Aliyosema Nyerere yaanza kutokea

picture-10.jpg

Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 10 November 2010

Jamvi la Weledi

WAKATI wa uhai wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tulisikia mengi ambayo sasa tunayakumbuka.

Nikiwa kijana wa Umoja wa Vijana – Tanu Youth League – na baadaye Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), nilishiriki uongozi wa vijana na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutunga na kufundishwa nyimbo zilizochochea uzalendo kwa vijana.

Naukumbuka wimbo mmoja uliosema, "Alisema, alisema,
Alisema Nyerere alisema,
Vijana wangu wote mmelegea,
Sharti muanze mchakamchaka…"

Nalazimika kuukumbuka wimbo huo kutokana na yaliyotokea ndani ya chama chetu wakati wa uchaguzi mkuu uliomalizika wiki iliyopita.

Matokeo ya uchaguzi huu, bila shaka yameshangaza wengi akiwamo mwenyekiti wetu, Rais Jakaya Kikwete ambaye alituahidi ushindi wa kishindo. Ni kwa sababu, ameibuka na "ushindi kiduchu" na almanusura kura zisingetosha.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, wapigakura wachache sana wamejitokeza katika vituo vya kupigiakura; huku vyama vya upinzani vikipata kura nyingi mijini na vijijini.

Kwa wiki kadhaa sasa, watu mbalimbali wakweli kwa waongo, watajikita kuchambua mambo haya, lakini mimi leo napenda nijadili dhana ya "Alisema Nyerere."

Ni ukweli ulio wazi kuwa yaliyotokea ndani ya chama chetu yalitarajiwa, na baadhi ya watu walionya pasipo kusikilizwa. Mwenyekiti wetu na marafiki zake kwa sasa wanadai hali hii imesababishwa na mpasuko uliotokea wakati wa kura za maoni.

Mtazamo huu hauna ukweli wowote kwa sababu hata pale ambapo CCM iliteua wagombea walioshinda kikweli katika kura za maoni, bado upinzani umekuwa mkubwa na baadhi ya majimbo kwenda upinzani.

Kigezo cha kura za maoni si kipimo pekee cha matokeo mabaya ya CCM katika uchaguzi uliomalizika.

Nasema matokeo mabaya kwa sababu, CCM imeshuka chini kwa asilimia 20 ukilinganisha na matokeo ya 2005, wakati wapinzani wamepanda kwa asilimia 22 katika kipindi hicho.
Ndani ya CCM, kwa takribani miaka mitano, wapo waliosema kama Mwalimu na wanastahili kuimbwa kama alivyoimbwa lakini hawakusikilizwa.

Mathalani tunaweza kuimba waliosema na kwa ufupi ni hawa hapa: Joseph Butiku, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Matheo Qares, Juma Nkhangaa, John Malecela, Joseph Warioba, Hassy Kitine, Phillip Mangula, Salim Ahmed Salim, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Harrison Mwakyembe, Christopher Sendeka.

Baadhi yao walisema ndani ya vikao vya chama na Watanzania wengi hawakuwasikia. Lakini wachache wao, walisema hata nje ya vikao kwa nia njema, Watanzania wakawasikia, lakini wakaishia kuitwa majina mabaya na kuambuliwa kejeli nyingi.

Wengine walisema na kukosoa chama hadharani, lakini wakazibwa midomo kwa kupewa vyeo na kuteuliwa katika nyadhifa kadhaa.

Wapo walioandika na kuweka rekodi katika historia, lakini hawakujibiwa na wala maandiko yao hayakujadiliwa. Chama chetu kikaasisi utamaduni mpya wa kudharau maoni ya wanachama wake na kuwaona kama maadui wa chama hicho.

La ajabu ni kwamba, wapinzani waliorejea CCM baada ya kukidhalilisha chama kwa miaka mingi, wakasikilizwa na kuheshimika sana ndani ya chama.

Watu hawa wakapewa nyadhifa kubwa ndani ya serikali na chama na kutumika hata kuwanyamazisha viongozi wastaafu na wanachama waaminifu wa CCM.

Marafiki wa chama wakawa ni wale wanaotoa fedha za kukiendesha chama kwa jinsi wao wanavyotaka. Nguvu ya fedha ikachukua nafasi ya nguvu ya uadilifu kama msingi wa kuongoza chama.

Wahenga walisema, "Mkataa pema, pabaya panamwita." Mtandao wa mwenyekiti wetu ulikuwa na nguvu ya kukataa ushauri na maoni mema ya wazee, lakini haukuwa na nguvu ya kukataa matokeo ya ukaidi huo.

Chama chetu sasa kinakataliwa sehemu nyingi nchini. Ukienda mikoa ya pembezoni mwa nchi hali imebadilika sana na si sahihi kudhani hii ni kwa sababu ya kura za maoni au nguvu ya Dk. Willibrod Slaa.

Chama chetu kilipoacha misingi yake ya kiutu na utetezi wa wanyonge wa taifa, kimesababisha kukataliwa na wananchi walio wengi.

Katika kila makao makuu ya mkoa isipokuwa Singida mjini, CCM imepata taabu sana kukubalika na imebidi kutumia njia "chafu" ili kuibuka na ushindi unaohojiwa.
Mabadiliko haya haraka yanahitaji maelezo ya kina, lakini wenye kuitakia mema CCM tayari wanasema, uzembe na woga wa kushughulikia masuala mazito hapa nchini ndio umepelekea CCM kukataliwa na watu wa mijini na vijijini.

Hata mijini na vijijini, wapinzani wameonekana mashujaa kuliko wabunge wa CCM.
Kwa kweli, niseme wazi kuwa baadhi yetu tulitamani sana wapinzani washinde zaidi ya walivyoshinda ili tupate nafasi pana zaidi ya kukikosoa chama chetu. Walio wakali zaidi, walikuwa tayari kumpoteza hata mwenyekiti wetu ili liwe fundisho kwa viongozi wajao.

Kwenye CCM ya Nyerere, ushindi huu mdogo wa chama na mgombea wake, ungesababisha baadhi ya watu kuwajibika ili kuleta heshima mbele ya jamii. Lakini kwa Jakaya Kikwete hilo ni gumu kufanyika, labda kutokana na kafara katika ngazi za chini badala ya kushughulikia masuala ambayo chama kimeshindwa kuyashughulikia.

Kana kwamba lililotokea halitoshi, tayari tunaona watu wanachukua fomu za kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri bila kujali tuhuma za watu kuhusu uhusika wao katika kipigo cha chama katika uchaguzi.

Ili kurejesha heshima ya chama chetu, tunamhitaji Kikwete tofauti na huyu aliyemaliza muda wake. Kikwete mpya anahitaji kubadilika.

Anahitaji kuwa msikivu si kwa wasaidizi na washauri wake, bali kwa watu wanaoweza kumwambia ukweli bila kuhofia kupoteza nafasi zao.

Kikwete mpya anahitaji kuvua joho la uswahiba wa mtandao na kuvaa umakini na uchungu kwa taifa lake na watu wake ambao wametopea katika lindi la umaskini. Anahitaji kuwa wazi, mkweli ili kurejesha heshima ya ikulu machoni mwa wananchi.

Anatakiwa kukataa kinachodaiwa kuwa miradi ya giza anayopewa na kuandaliwa na marafiki zake kwa kisingizio cha kuwa "hata rais ana maisha binafsi."

Katiba yetu inamhakikishia ulinzi na matunzo rais mstaafu kwa hiyo aepukane kabisa na miradi yenye harufu ya kifisadi inayoweza kuanzishwa na watu wanaodai kuwa wako karibu naye.

Si vema kumwona rais anahangaika na kukutana na mameneja wake wa biashara na wawekezaji binafsi. Hali hii itamletea utumwa na kigugumizi cha kushughulikia ufisadi.

Kikwete apunguze safari za nje zisizo na tija. Aachane na tabia ya kuonekana mcheza "midundiko." Ni vema Kikwete akajua kuwa hoja nyingi za wapinzani zimekubalika kwa wananchi kutokana na kuonekana ni makini na wana uchungu na taifa.

Chanzo: Mwanahalisi Novemba 10, 2010.

Naona hapo penye nyekundu umemsahau John Tendwa. Yeye alienda mbali hata zaidi ya yaliyotokea akasema wapinzani wanaweza kupata wabunge 100. Japo upande wa uraisi hakuthubutu kugusa
 
Back
Top Bottom