MCC na Wengineo: Fahamu Athari za Misaada ya Kigeni

Imani2

Member
May 6, 2014
93
43
MCC na Wengineo: Athari za Misaada ya Kigeni

Shirika la marekani- MCC limesitisha kutoa misaada yake kwa Tanzania kwa madai ya ukiukwaji wa demokrasia katika uchaguzi wa kitaifa Zanzibar na pia sheria ya uhalifu mtandaoni. Mengi yameandikwa hapa na nisingependa kurudia. Wapo wanaosema tunapaswa kuwapigia magoti wafadhili na wapo pia wanaona bora waondoke zao liwalo na liwe.

Ni kweli tunahitaji misaada lakini pia uhuru wetu wa kuamua mambo yetu, mahitaji na vipaumbele vyetu hauna budi kuheshimiwa. Hakuna mantiki ya kupewa msaada na kulazimishwa kutumia fedha hizo katika vitu fulani ama sekta fulani tu. Naungana na wanaosema ishu ya MCC sio demokrasia zanzibar wala cybercrimes act. Hoja yangu hapa ni dhidi ya misaada kwa ujumla na wala sio MCC tu. Hoja ya msingi ni kwamba misaada ya nchi wafadhili inabomoa zaidi ya kutujenga na hatuna budi kuanza kuondokana na gonjwa hili.

Tukumbuke tu kwamba nchi nyingi za kiafrika mara nyingi hutizama misaada kama chanzo cha mapato cha kudumu na cha uhakika na hivyo hujiachia wakiamini misaada itaendelea kumiminika milele. Hii imefanya nchi nyingi kutokuwa na mipango ya muda mrefu ya kifedha, kutokukusanya kodi ama kuwa na vyanzo ziada vya mapato. Lakini kama tulivyoona kwa MCC na wengineo waliosistisha misaada yao, unaona wazi kuwa misaada hii sio ya uhakika, haitabiriki na mrija unaweza kukatwa saa yoyote kwa sababu au kisingizio chochote kile na hivyo lazima uwe na plan B. Nchi inayohitaji kukua kiuchumi na kuboresha maisha ya watu wake haina budi kupunguza ama kuondokana na utegemezi wa misaada.

Nitabainisha kwa juu juu namna misaada inavyotudhoofisha kiuchumi na kuongeza umaskini zaidi na kwa kutumia MCC kama mfano.

1. Misaada huja na masharti kuwa fedha ziende sekta gani ama zitumike kununua bidhaa gani bila kujali hitaji ama vipaumbele vya nchi husika (aid inaenda kwenye procurement zao)

- Mara nyingi nchi wafadhili huweka masharti ya kwamba fedha zao zitumike katika sekta gani, ama kununua vifaa gani, na zaidi huelekezwa kwenye manunuzi ama uuzaji wa bidhaa fulani wanazotaka wao(procurement). Mfano mzuri ni fedha za MCC zinalenga kupanua soko la umeme la Symbion kwa mgongo wa Tanesco. Jiulize kwa nini fedha za MCC hazikupelekwa sekta ya elimu, afya,mifugo, michezo, ama mazingira? Sababu sekta ya nishati tanzania ni goldmine (kuna faida ya asilimia maelfu). Miradi ya MCC inalekekezwa vijijini kuweka miundo mbinu ya umeme. Wakati huohuo kampuni ya Symbion ambayo ni kama corporate branch ya MCC ndio ina mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme na kuwauzia watanzania. Ukiangalia hapa misaada ya MCC inalenga kutengeneza wigo mpana wa watumiaji wa umeme(consumer base) ili kupanua soko la biashara yao ya umeme. Hakuna msaada hapa, wataalam wanasema nothing goes for nothing. Unakula... kisha nawe unaliwa pia(JK)

2. Misaada huja tu ukinyenyekea na kukubali sera za wafadhili wako.

Misaada huja tu ukinyenyekea na hata kudhalilisha uhuru, utu ama utaifa wako. Tangu Magufuli aingie madarakani ameonesha taswira ya kutokuwa mlamba viatu wa magharibi. Ni kama hana habari vile. Sasa kwenye siasa za kimataifa vitu vidogo vina maana kubwa. It is the small gestures that matter. Mmemsikia JPM akisema hataki tena mikataba ya kipuuzi kama IPTL na mengineyo.. Message waliyopata wadau wa MCC ambao ni kivuli cha Symbion ni kuwa uhakika wao wa kunyonya faida kwenye soko la umeme upo kwenye hatihati. Pia ipo taswira fulani kwamba huyu JPM ni jeuri, hana shida ya kuwa international figure, sio mtu wa kurubuniwa na kuwekwa kwenye paylist zao ama kubabaishwa na zile red carpets wanazotandaziwa wakuu wetu ulaya. Tukumbuke pia JPM ni chaguo la wananchi na hakutegemewa kwa hiyo hana deep links na magharibi kama ma-cartels fulani yaliyokuwa yanahodhi siasa za tanzania. JPM ameamua kufocus kwenye matatizo ya ndani na sio safari za kila siku ughaibuni. Kitendo cha wafadhili kusitisha misaada ni hasira ya kutonyenyekewa na hivyo wanajaribu kuonyesha umuhimu wao (kutafuta relevance) na kutaka “kumuadhibu” JPM kwa mfumo ule wa “fimbo na karoti” (ukiwa mtoto mzuri kwao unapewa sifa, kapeti nyekundu na msaada(karoti) ukiwa mkorofi unapata vikwazo, vitisho na kunyimwa misaada(fimbo). Watz, tukumbuke haiwezi kuwa bahati mbaya MCC na nchi 10 kujitoa ghafla kwa mkupuo kwenye bajeti support ambapo mwaka mmoja tu ulopita tulikuwa tunaitwa “darling of the west” (Tz kipenzi cha nchi za magharibi)

3. Misaada hudumaza uchumi na hukuza rushwa

Fedha za bure zinapoingizwa kwenye mzunguko wa uchumi kuna hatari kubwa ya mfumuko wa bei na kudodora kwa uchumi. Pale viongozi wa umma huko serikalini wanapoiba hizi fedha kwa mafungu na lumbesa na kisha kuziingiza kwenye mzunguko wa pesa wa kawaida kinachotokea ni kwamba kunakuwa na fedha nyingi kwenye mzunguko wakati hakuna bidhaa zozote zilizozalishwa nchini. Tumesikia wakuu wa REA wakisema hawajawahi kutegemea fedha za MCC kuendesha miradi yao. Sasa jiulize pesa hiyo imeenda wapi?. Misaada husababisha rushwa kukithiri. Kwa sababu fedha hizi ni za bure, viongozi waandamizi hugawana juu kwa juu bila hofu ya kuwajibishwa.

Ukiwa na fedha nyingi na bidhaa chache, maana yake ni pesa kushuka thamani na bei ya vitu kupaa juu. Pili, watu wanapowaona wanasiasa waliokula hizi fedha wakiendesha vogue, benz nk, na ”kuishi kama malaika”, watu wanaanza kuamini siasa tu ndo inalipa, na wanaanza kutoa rushwa kupata nafasi hizo za kisiasa ili nao wakanufaike na hizo grants. Tamaa ya kunufaika harakaharaka na Misaada hii inafanya hata wasomi, wanataaluma na wengineo kuacha kufanya shughuli zao kitaalamu na za uzalishaji na kukimbilia siasa.

4. Misaada ya kula tu na sio ya kuwekeza

Mara nyingine misaada hii huja kama fedha za bure na si mkopo,ijapokuwa zinarudi kwa mlango wa nyuma na wakati mwingine ukipewa msaada unatakiwa kutoa mikataba kwa kampuni zao fulani.Tunapopata fedha nyingi za bure, wakati hatuna viwanda vya kuwekeza, fedha zinalala tu na mwisho wake ni kuanza kutafutiwa namna ya kuzila na kuziingiza kwenye mzunguko wa uchumi. Uchumi wetu unashindwa kuhimili fedha nyingi zilizomwagwa tu bila production yoyote kufanyika. Hakuna viwanda vya kutumia hizo fedha kuzalisha mali na faida, matokeo yake serikali inabidi kutafuta namna ya kutumia tu hizo fedha (consume) na sio kuwekeza. Tunaishia kutumia hizi fedha kuendesha warsha, trainings, semina na semina elekezi kwa gharama za mabilioni. Na hata mikopo ya riba tunakopa na kula tu na si kuwekeza (tunatumia kulipia mishahara ya watumishi na huduma za jamii na haizalishi faida ndio maana ya deni la taifa kufikia takribani trilioni 40). Tatizo ni kwamba hawa wafadhili wanataka tuendelee kukopa na kukopa. Utasikia wanakupamba uchumi wako unakua hata kama watu wako hawajui wanakula nini kesho. Wao wana fedha zilizolala tu na kawaida mtaji (fedha ) hauwezi kuzalisha faida bila ku-exploit labour.

5. Masharti ya demokrasia na haki za binadamu ni visingizio tu.

Kuna hoja kuwa tumenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya ukiukwaji wa demokrasia zanzibar na ile sheria ya uhalifu mtandaoni. Nchi wafadhili wanaamini siku zote demokrasia na utawala wa sheria ndio dawa dhidi ya rushwa na ufisadi,na kuondoa upendeleo na kulindana (cronysm). Kwanza ni kweli demokrasia husaidia kukuza uchumi, kulinda haki za kiraia na kijamii nk. Demokrasia pia huwapa watu fursa na haki ya kushriki kuchagua serikali yao na kushiriki katika vyombo vya maamuzi. Aliyesaini na kupitisha sheria ya cybericrimes ni JK, kwa nini hakuwekewa vikwazo ama kunyimwa pesa?. Tangu Magufuli ameingia madarakani ameonyesha moyo wa dhati kukabili rushwa na ufisadi. Pia ukilinganisha nchi yetu na nchi kama misri, ethiopia, saudi arabia na wengine wenye rekodi mbaya za haki za binadamu, utagundua kuwa tuna demokrasia bora kwa ulinganisho. Natambua uchaguzi wa Znz ulikuwa na dosari, ila naungana na wanaosema ishu sio Zanzibar kwani chaguzi za Zanzibar zimekuwa na dosari zake mara kwa mara na haijawahi kuwa ishu kwa wafadhili. Ingekuwa wafadhili wana nia ya kweli, Magufuli angepaswa kuongezewa misaada kwa juhudi za dhati za kukabili rushwa, ufisadi, na umaskini.

Watanzania tusilalamike kunyimwa msaada, bali iwe ni fundisho kuwa misaada hii si ya kudumu na sio ya uhakika siku zote. Tufahamu kuwa misaada sio dawa ya kuondoa umaskini na kuleta maedeleo. Badala yake tumsapoti JPM kwenye juhudi za kukusanya mapato ya ndani na kukabili ufisadi. Ikibidi tufungue akaunti ya kumchangia Magufuli, kuonesha sapoti yetu, watz mil 40 kila mmoja akichangia 1000 kwa mwaka tutapata bilioni 40 kwa mwaka.
 
Na pia kumbuka hao jamaa wakikupa dola billioni moja wao watavuna angalau kuanzia dola billioni mbili kwa kuanzia.Maana wataleta watu wao wakandalasi wao kama ni mradi bwawa au barabarawanaweza kutana na madini uko msipokuwa na TISS iliyosimama watakwapua etc
Akili kumkichwa
 
MCC na Wengineo: Athari za Misaada ya Kigeni

Shirika la marekani- MCC limesitisha kutoa misaada yake kwa Tanzania kwa madai ya ukiukwaji wa demokrasia katika uchaguzi wa kitaifa Zanzibar na pia sheria ya uhalifu mtandaoni. Mengi yameandikwa hapa na nisingependa kurudia. Wapo wanaosema tunapaswa kuwapigia magoti wafadhili na wapo pia wanaona bora waondoke zao liwalo na liwe.

Ni kweli tunahitaji misaada lakini pia uhuru wetu wa kuamua mambo yetu, mahitaji na vipaumbele vyetu hauna budi kuheshimiwa. Hakuna mantiki ya kupewa msaada na kulazimishwa kutumia fedha hizo katika vitu fulani ama sekta fulani tu. Naungana na wanaosema ishu ya MCC sio demokrasia zanzibar wala cybercrimes act. Hoja yangu hapa ni dhidi ya misaada kwa ujumla na wala sio MCC tu. Hoja ya msingi ni kwamba misaada ya nchi wafadhili inabomoa zaidi ya kutujenga na hatuna budi kuanza kuondokana na gonjwa hili.
Haya uliyoandika ni porojo tu.Uchumi wetu Tanzania bado ni tegemezi
 
Analysis yako imetulia nakuunga mkono, lakini je uroho Wa viongoz wetu umeisha? Mbona wanajitapa kuwa tutapata wafadhiri wengine au hao hawana mashart ?
 
Tukumbuke tu kwamba nchi nyingi za kiafrika mara nyingi hutizama misaada kama chanzo cha mapato cha kudumu na cha uhakika na hivyo hujiachia wakiamini misaada itaendlea kumiminika milele. Hii imefanya nchi nyingi kutokuwa na mipango ya muda mrefu ya kifedha, kutokukusanya kodi ama kuwa na vyanzo ziada vya mapato. Lakini kama tulivyoona kwa MCC na wengineo waliosistisha misaada yao, unaona wazi kuwa misaada hii sio ya uhakika, haitabiriki na mrija unaweza kukatwa saa yoyote kwa sababu au ksingizio chochote kile na hivyo lazima uwe na plan B. Nchi inayohitaji kukua kiuchumi na kuboresha maisha ya watu wake haina budi kupunguza ama kuondokana na utegemezi wa misaada.

Nitabainisha kwa juu juu namna misaada inavyotudhoofisha kiuchumi na kuongeza umaskini zaidi na kwa kutumia MCC kama mfano.

1. Misaada huja na masharti kuwa fedha ziende sekta gani ama zitumike kununua bidhaa gani bila kujali hitaji ama vipaumbele vya nchi husika (aid inaenda kwenye procurement zao)

- Mara nyingi nchi wafadhili huweka masharti ya kwamba fedha zao zitumike katika sekta gani, ama kununua vifaa gani, na zaidi huelekezwa kwenye manunuzi ama uuzaji wa bidhaa fulani wanavyotaka wao(procurement). Mfano mzuri ni fedha za MCC zinalenga kupanua soko la umeme la Symbion kwa mgongo wa Tanesco. Jiulize kwa nini fedha za MCC hazikupelekwa sekta ya elimu, mifugo, michezo, ama mazingira? Sababu sekta ya nishati tanzania ni goldmine (kuna faida ya asilimia maelfu). Miradi ya MCC inalekekezwa vijijini kuweka miundo mbinu ya umeme. Wakati huohuo kampuni ya Symbion ambayo ni kama corporate branch ya MCC ndio ina mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme na kuwauzia watanzania. Ukiangalia hapa misaada ya MCC inalenga kutengeneza wigo mpana wa watumiaji wa umeme(consumer base) ili kupanua soko la biashara yao ya umeme. Hakuna msaada hapa, wataalam wanasema nothing goes for nothing. Unakula... kisha nawe unaliwa pia(JK)

2. Misaada huja tu ukinyenyekea na kukubali sera za wafadhili wako.

Misaada huja tu ukinyenyekea na hata kudhalilisha uhuru, utu ama utaifa wako. Tangu Magufuli aingie madarakani ameonesha taswira ya kutokuwa mlamba viatu wa magharibi. Ni kama hana habari vile. Sasa kwenye siasa za kimataifa vitu vidogo vina maana kubwa. It is the small gestures that matter. Mmemsikia JPM akisema hataki tena mikataba ya kipuuzi kama IPTL na mengineo.. Message waliyopata wadau wa MCC ambao ni kivuli cha Symbion ni kuwa uhakika wao wa kunyonya faida kwenye soko la umeme upo kwenye hatihati. Pia ipo taswira fulani kwamba huyu JPM ni jeuri, hana shida ya kuwa international figure, sio mtu wa kurubuniwa na kuwekwa kwenye paylist zao ama kubabaishwa na zile red carpets wanazotandaziwa wakuu wetu ulaya. Tukumbuke pia JPM ni chaguo la wananchi na hakutegemewa kwa hiyo hana deep links na magharibi kama ma-cartels fulani yaliyokuwa yanahodhi siasa za tanzania. JPM ameamua kufocus kwenye matatizo ya ndani na sio safari za kila siku ughaibuni. Kitendo cha wafadhili kusitisha misaada ni hasira ya kutonyenyekewa na hivyo wanajaribu kuonyesha umuhimu wao(kutafuta relevance) na kutaka “kumuadhibu” JPM kwa mfumo ule wa “fimbo na karoti” (ukiwa mtoto mzuri kwao unapewa sifa, kapeti nyekundu na msaada(karoti) ukiwa mkorofi unapata vikwazo, vitisho na kunyimwa misaada(fimbo). Watz, tukumbuke haiwezi kuwa bahati mbaya MCC na nchi 10 kujitoa ghafla kwa mkupuo kwenye bajeti support ambapo mwaka mmoja tu ulopita tulikuwa tunaitwa “darling of the west” (Tz kipenzi cha nchi za magharibi)

3. Misaada hudumaza uchumi na hukuza rushwa

Fedha za bure zinapoingizwa kwenye mzunguko wa uchumi kuna hatari kubwa ya mfumuko wa bei na kudodora kwa uchumi. Pale viongozi wa umma huko serikali wanapoiba hizi fedha kwa mafungu na lumbesa na kisha kuziingiza kwenye mzunguko wa pesa wa kawaida kinachotokea ni kwamba kunakuwa na fedha nyingi kwenye mzunguko wakati hakuna bidhaa zozote zilizozalishwa nchini. Tumesikia wakuu wa REA wakisema hawajawahi kutegemea fedha za MCC kuendesha miradi yao. Sasa jiulize pesa hiyo imeenda wapi?. Misaada husababishsa rushwa kukithri. Kwa sababu fedha hizi ni za bure, viongozi waandamizi hugawana juu kwa juu bila hofu ya kuwajibishwa.

Ukiwa na fedha nyingi na bidhaa chache, maana yake ni pesa kushukua thamani na bei ya vitu kupaa juu. Pili, watu wanapowaona wanasiasa waliokula hizi fedha wakiendesha vogue, benz nk, na ”kusihi kama malaika”, watu wanaanza kuamini siasa tu ndo inalipa, na wananza kutoa rushwa kupata nafasi hizo za kisiasa ili nao wakanufaike na hizo grants. Tamaa ya kunufaika harakaharaka na Misaada hii inafanya hata wasomi, wanataaluma na wengineo kuacha kufanya shughuli zao kitaalamu na za uzalishaji na kukimbilia siasa.

4. Misaada ya kula tu na sio ya kuwekeza

Mara nyingine misaada hii huja kama fedha za bure na si mkopo,ijapokuwa zinarudi kwa mlango wa nyuma na wakati mwingine ukipewa msaada unatakiwa kutoa mikataba kwa kampuni zao fulani.Tunapopata fedha nyingi za bure, wakati hatuna viwanda vya kuwekeza, fedha zinalala tu na mwisho wake ni kuanza kutafutiwa namna ya kuzila na kuzingiza kwenye mzunguko wa uchumi. Uchumi wetu unashindwa kuhimili fedha nyingi zilizomwagwa tu bila production yoyote kufanyika. Hakuna viwanda vya kutumia hizo fedha kuzalisha mali na faida, matokeo yake serikali i kutafuta namna ya kutumia tu hizo fedha (consume) na sio kuwekeza. Tunaishia kutumia hizi fesha kuendesha warsha, trainings, semina na semina elekezi kwa gharama za mabilioni. Na hata mikopo ya riba tunakopa na kula tu na si kuwekeza(tunatumia kulipia mishahara ya watumishi na huduma za jamii na haizalishi faida ndio maana ya deni la taifa kufikia trakribani trilioni 40). Tatizo ni kwamba hawa wafadhili wanataka tuendelee kukopa na kukopa. Utasikia wanakupamba uchumi wako unakua hata kama watu wako hawajui wanakula nini kesho. Wao wana fedha zilizolala na kawaida mtaji (fedha ) haziwezi kuzalisha faida bila ku-exploit labour.

5. Masharti ya demokrasia na haki za binadamu ni visingizio tu.

Kuna hoja kuwa tumenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya ukiukwaji wa demokrasia zanzibar na ile sheria ya uhalifu mtandaoni. Nchi wafadhili wanaamini siku zote demokrasia na utawala wa sheria ndio dawa dhidi ya rushwa na ufisadi,na kuondoa upendeleo na kulindana (cronysm). Kwanza ni kweli demokrasia husaidia kukuza uchumi, kulinda haki za kiraia na kijamii nk. Demokrasia pia huwapa watu fursa na haki ya kushriki kuchagua serikali yao na kushiriki katika vyombo vya maamuzi.. Aliyesaini na kupitisha sheria ya cybericrimes ni JK, kwa nini hakuwekewa vikwazo?. Tangu Magufuli ameingia madaraki ameonyesha moyo wa dhati kukabili rushwa na ufisadi. Pia ukilinganisha nchi yetu na nchi kama misri, ethiopia, saudi arabia na wengine wenye rekodi mbaya za haki za binadamu, utagundua kuwa tuna demokrasia bora kwa ulinganisho. Natambua uchaguzi wa Znz ulikuwa na dosari, ila naungana na wanaosema ishu sio Zanzibar kwani chaguzi za Zanzibar zimekuwa na dosari zake mara kwa mara na haijawahi kuwa ishu kwa wafadhili. Ingekuwa wafadhili wana nia ya kweli, Magufuli angepaswa kuongezewa misaada kwa juhudi za dhati za kukabili rushwa, ufisadi, na umaskini.

Watanzania tusilalamike kunyimwa msaada, bali iwe ni fundisho kuwa misaada hii si ya kudumu na sio ya uhakika siku zote. Tufahamu kuwa misaada sio dawa ya kuondoa umaskini na kuleta maedeleo. Badala yake tumsapoti JPM kwenye juhudi za kukusanya mapato ya ndani na kukabili ufisadi. Ikibidi tufungue akaunti ya kumchangia Magufuli, kuonesha sapoti yetu, watz mil 40 kila mmoja akichangia 1000 kwa mwaka tutapata bilioni 40 kwa mwaka.
Mkuu umenena vizuri sana,ila subiri uone wapenda misaada watakavyo kushambulia.

Unajua mimi huwa nashangaa hivi sisi watanzania nani katuroga?
 
Na pia kumbuka hao jamaa wakikupa dola billioni moja wao watavuna angalau kuanzia dola billioni mbili kwa kuanzia.Maana wataleta watu wao wakandalasi wao kama ni mradi bwawa au barabarawanaweza kutana na madini uko msipokuwa na TISS iliyosimama watakwapua etc
Akili kumkichwa
kiukweli inatakiwa iitwe
biashara ya misaada. Ni bizness ya kuvuna faida.
 
Analysis yako imetulia nakuunga mkono, lakini je uroho Wa viongoz wetu umeisha? Mbona wanajitapa kuwa tutapata wafadhiri wengine au hao hawana mashart ?
uroho na ulafi bado upo. Sasa kuacha uroho na kusimamia uzalendo jukumu letu wenyewe. hata wakipatikana wafadhili wengine bado misaada sio jambo la kutegemea kuendesha serikali. Lazima kuwe na mwanzo wa kuachana nayo.
 
Mkuu wapo hao watetezi wa misaada
wasiotaka kusikia ubaya wa fedha za bure. Wapo mpaka wanaolipwa kujaribu ku-influence public opinion na kushawishi ionekane tz tutaumia sana tukikosa misaada ya wafadhili.
 
Tuungane kupinga kuyumbishwa na misaada uchwara. Misaada iheshimu utu wetu, uhuru na utaifa wetu pia
pinga kwanza wamama kuzaa chini na watoto wa shule kukaa chini wakati magu anakula 9.8 million in 1week.

swissme
 
pinga kwanza wamama kuzaa chini na watoto wa shule kukaa chini wakati magu anakula 9.8 million in 1week.

swissme
Mkuu 9.8m kwa rais wa JMT ni pesa kidogo sana tena kwa shilingi ya kitanzania yenye thamani ndogo. ,Kuhusu wamama na watoto,ndio ninachosema hapo juu. Sisi tunajua shida na vipaumbele vyetu ikiwemo afya na elimu, ila wanaotoa hiyo msaada watakuambia haupaswi kutumia kununua vitanda ama madawati.
 
Back
Top Bottom