Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,469
- 3,540
Niende kwenye mada moja kwa moja. Ndugu zetu Wamasai kwa sasa hofu imetanda; hawalali usingizi tena, hawajui nini kitatokea. Katika hali hiyo, wanalala wima kwa sababu ya hali ya sintofahamu inayowakabili. Nadhani hawalali usingizi tena.
Tuhamasishane kupeleka misaada ya chakula, maji, na madawa. Kwa hali halisi hakuna namna wanaweza kupata misaada ya kibinadamu.
Kama mitandao yetu na vyombo vya habari vinavyosaidia kupaza sauti katika hali mbalimbali inapotokea, basi tupaze sauti lakini kwa kuhamasisha mashirika na sekta binafsi na hata mtu mmoja mmoja kupeleka misaada ya kibinadamu Ngorongoro.
Jiografia ya maeneo yao maji ni shida kubwa na upatikanaji wa huduma zote haupo tena.