Mbwembwe hazifai safarini

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,074
Leo katika safari yangu ya Dar es salaam to Dodoma kama kawaida nikakata siti ya dirishani.Mara ghafla kama maombi yangu kama yalikuwa yanasikilizwa akaja mtoto mmoja mzuri sana sema alikuwa amedress kawaida.Na mimi nikasema yeees leo mpaka tukifike Dom nitapiga hata mashuti 50 On target nikaandaa vifaa vya mashambulizi sasa.

Kwa mbwembwe nikachomoa Iphone5 yangu niliyoipata kwa kuungaunga kama gia fulani ya kunipush kwa mtoto kushangaa demu nikaona katoa zake Iphone6 + wala hana hata habari na mimi.

Nikasema huyu manzi vipi mbona anataka kunipiga knockout mapema hivi wakati nafikiria hayo nikaona isiwe kesi niendelee kupata azam embe yangu kucheki tena demu kumbe alikuja na savanna zake kama mbili nikashindwa kutupa kiazam embe changu ikabidi nikimalizie.

Tumefika Gairo nikanunua maindi mawili nimpatie na yeye moja kumuuliza manzi katikisa kichwa kuashiria hataki.Kumcheki tena manzi akachomka Pringles zake akawa anakula taratibu na kuniacha mimi na mahindi yangu yamoto.

Nikaamua kufanya maamuzi magumu ya kulala kwa lazima maana kila mbwembwe niliyotaka kufanya alikuwa akinilipa mara mbili,kabla sijalala nikawa nafkiria tactic ya kuanzisha ili nipate hata namba nikamuona yupo zake na Ipad4 yake anaangalia video.

Kusema za ukweli nilimchukulia poa sana ndo maana nilitegemea kasimu changu kuwa kanawza kuanzisha move ya kumpata mwisho wa siku niliishia kuaibika simu yangu nikaificha kwa aibu na bado hata mambo sikupata.

Mbwembwe safarini hazifai.
 
Huna akili, unaleta ushoga hapa, we wa Wapi, story Za kishamba
 
ok...cool and the gang
 
Haaa Haaa Haaa Haaa Haaa Haaa Haaa Haaa Haaa
 
Kwa swaga hizo hata mtoto wa praimary angekuona bw.ege tu!!!
 
kumbe wagogo washamba hivi ndio maana omba omba
 
!
!
vijana tupunguze kutumia madawa ya kuongeza nguvu mchezoni......haya ma iphone sijui manini ya nini?unatoa katochi kako akuu, unabadili line unatoa ya tigo unaweka airtel, unatoa ya airtel unatia voda mara kadimu chaji imeisha unaomba kutuma msg, unajitumia utaikutaga home huku unatafuta points. S@sa wewe, daaaah poyeee
 
Mgosia, hapo kwenye bold vipi tena? Tuombe chenji au bado umechanganyikiwa na Wa Mbati mwenye Iphone na Ipad?
 
Kiukweli watu tunatofautiana sana.

Mara nyingi nakua huru nikiwa na kimeo kuliko kuwa na simu kubwa.

After all kumuona mtu anavitu vya bei kali sio kikwazo cha kunifanya nisifanye yangu ikiwa nimedhamiria.

Huo wako unaitwa upoyoyo. ningekua na no yako ningekutumia video flani huenda ungejifunza.

Promo na kujipaisha kwa kipato au kujiona duni kwa kukosa kipato ni msiba kama misiba mengine.
 
Kizazi hiki kimeishiwa wanaume,wengi wamebakia kanyaboya,yani mtoto kutoa iphone 6+ ndio ukaogopa kumtongoza?

Acha ujinga,usiogope ukubwa wa samaki,uliza bei.
 
Wee Donkey, lugha gani hizi unatuwekea hapa? Hutaki, unaacha, Msula eve, heheheheee.....
Huna akili, unaleta ushoga hapa, we wa Wapi, story Za kishamba


Jamaa siyo Mgogo, unatamani sana awe na Ugonjwa wa macho na Ombaomba? Hamumpati ng'ooo... Huyo ni Ngosha wa nguvu, kama vipi. Hapo anatania tu maana tulikuwa wote na namba ya simu kapewa vilevile. Imeandikwa T3114....
Wagogo mna matatizo sana.Nini hiki sasa.
 
Nimeishia kucheka tu na kukuonea huruma maana bado una swaga za kizamani
 
Mleta mada asante kwa kuimaliza vizuri siku yangu.
 
....hahahahhaaaa burudani, ka kamba kazuri sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…