Alphaking2023
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 2,092
- 2,123
Mafanikio aliyoyapata mchezaji nyota wa Tanzania Mbwana Samatta ni makubwa sio kwake tu bali kwa taifa zima kwani amepeperusha bendera ya Tanzania kwa mara ya kwanza mchezaji bora wa Afrika anatoka Tanzania.
Cha kushangaza Serikali haijali rekodi kama hizi sijui itajali nini. Nimeshangaa sana Serikali imeshindwa kumpatia Ulinzi Mbwana Samatta aliposhuka Uwanja wa Ndege akitokea Abuja.
Watanzania wengi walijitokeza kumpokea huku wakishangilia ushindi kwa Taifa kwa ujumla lakini Serikali haikuweza kumpa hata askari mmoja tu aweze kumlinda kwani ilikuwa ni hatari sana kwa Usalama wa Samatta, mashabiki walimsonga sana kila mtu akitaka kumkumbatia sijui kama Serikali haikulijua hili, au hawakujua kama Samatta atarudi usiku anahitaji Ulinzi.
Mchango wa TFF kwa wachezaji wetu ni upi? Waziri wa Michezo alikuwa wapi? Au walikuwa wanasubiri JPM atume walinzi kumpokea Samatta.?
Mnatuvunja moyo katika jitihada zetu za kuliinua Taifa letu.

Last edited by a moderator: