MBWANA SAMATA kuuzwa bilioni 17

MBWANA SAMATA kuuzwa bilioni 17

jerryempire

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
5,830
Reaction score
10,090
STRAIKA wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atatua katika Klabu ya Middlesbrough ya England endapo klabu hiyo ikitoa kiasi cha Euro milioni 6.5 (bilioni 17) ambayo ndiyo thamani ya mchezaji huyo.

Samatta anayeongoza chati ya wafungaji katika Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa na mabao 15, anawindwa kwa ukaribu na baadhi ya timu za England sambamba na Fenerbahce ya Uturuki.

Kwa mujibu wa takwimu za Mtandao wa viwango wa Transfermarket, unaonyesha kwamba thamani ya nahodha huyo wa Taifa Stars imepanda maradufu kutoka ile aliyokuwa nayo Septemba, mwaka
jana.

Kwa sasa Samatta anayeshika nafasi ya tano kwa ubora ndani ya kikosi cha Genk, amepanda thamani kutoka Euro milioni nne (sawa na bilioni 10), mwaka jana hadi bilioni 17 kwa mwezi huu.

Timu ambazo zinamtaka mshambuliaji huyo anayekamata nafasi ya 183 duniani kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, zitalazimika kuilipa KRC Genk dau hilo la bilioni 17, kwa ajili ya kuipata huduma yake.

Wakati Samatta ambaye ndani ya Ligi kuu ya Ubelgiji akikamata nafasi ya 14 kwa ubora wa viwango vya wachezaji thamani yake ikipanda, swahiba wake Thomas Ulimwengu aliyejiunga na JS Saoura ya Algeria, mambo hayaendi sawa baada ya thamani yake kushuka kutoka dola 150,000 hadi dola 100,000,kwa msahahara huo huenda Samata akawa ndo mtu mwenye kulipwa mpunga mwingi Tanzania kushinda mfanyakazi yoyote
 
Oh okay sawa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Championship kunamfaa sana kwa kuanzia, msimu huu Middle wanategemea playoffs kupanda ambapo chance inakuwa very slim.

Ila wakikomaa msimu ujao wanapanda, kama akichukuliwa sasa hivi itakuwa poa sana ili azoee maisha mapya na msimu ujao awajaze magoli.
 
Safi sana;

Mapambano daima.

Hapo Euro 6.5 mil= 17 billion Walau ipo vyema kumrahisishia msomaji.

Redio nyingi sana hapa Tanzania hasa vipindi vya Michezo huwa hawaelezei/kutoa Tafsiri/kuzitoa pesa hizi za Euro,Paund €, £ na kuziweka katika Tsh ili wapenzi wa soka wapate picha kamili ya fedha katika mambo ya kandanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongelea Mshahara au Ada ya Usajiri? Wanavyosema thamani ya Samatta ni 17 billions hawamaanishi Mshahara Mkuu.
 
Back
Top Bottom