Mbwa wala korodani za mtoto wa miezi sita

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125



bulldogfight2.jpg

MTOTO wa miezi sita ametafunwa korodani zake na mbwa baada ya kuachwa peke yake ndani ya gari katika nyumba moja huko California, Marekani.

Mtoto huyo aliachwa katika kiti cha gari na mama yake Carrie McKinney, 22, wakati amekwenda kumwangalia rafiki yake wa kiume aitwaye Doug Ritchey.

Baada ya kuondoka tu, mbwa wawili wa Ritchey waliweza kufungua gari na kutafuna korodani za mtoto huyo ambaye kwa mujibu wa polisi, alikimbizwa hospitali ya Loma Linda University Medical Center kwa ajili ya upasuaji ili kuokoa korodani zake.

McKinney atakabiliwa na mashitaka ya uzembe wa uhalifu ambapo amepoteza kwa muda haki ya kukaa na mtoto wake huyo ambaye anaangaliwa na Shirika la Kuhudumia Watoto.

Mbwa hao waliohusika wataadhibiwa kwa kuuawa kwa njia maalum isiyoleta mateso.

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mbwa-wala-korodani-za-mtoto-wa
 
Back
Top Bottom