Jamaa kaingia nyumbani kwa
mchungaji
akionekana ana majonzi makubwa;
MCHUNGAJI: Vipi ndugu yangu?
JAMAA: Familia yangu ina njaa,
nimemuibia mtu
mbuzi yuko hapo nje, najisikia
vibaya naomba
tafadhali umchukue
MCHUNGAJI: Aaa wapi, sipokei mali
ya wizi mimi.
Kwanini usimrudishie mwenye mbuzi
wake?
JAMAA: Mwenye mbuzi kamkataa
MCHUNGAJI: Basi kama hivyo huyo
halali yako
kalishe familia yako
JAMAA:Asante sana mzee asante
sana.
Mchungaji alipoamka kesho yake
akagundua
mbuzi wake kaibiwa.