Mbuzi wanaozurura mijini ni wa nani? Inakuwaje hawaibwi na vibaka na hurudi nyumbani hata km 10 wenyewe?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,478
119,292
Hawa mbuzi bana eti wanaogopwa sana. Kuna kila aina ya stori juu yao.

Kila siku huwa wanaonekana wakiranda randa. Inavosemekana eti hawana mwenyewe. Pia wanadaiwa eti ni mbuzi wa kishirikina.

Eti kwa mfano ukimkamata mmoja na kwenda kumchinja utapatwa na mambo mabaya.

Mi binafsi siamini kabisa katika hizo stori. Naona ni hofu potofu tu. Na tena siku moja nina mpango wa kukamata mmoja nimchinje halafu nimchome.



20160604_154049.jpg
 
Haaa kuna kipindi nilikwenda Tabora maeneo ya stand kulikuwa na Mbuzi wanaranda randa wanajua kukwepa magari tena wanene kweli nikamuuliza mwenyeji wangu akaniambia hawa mbuzi hawana mwenyewe ukijaribu kumchukua kamwe huwezi kumchinja. Kuna Mchagga mmoja alijaribu kesho yake asubuhi na mapema akamreshesha mwenyewe bila kupenda.
 
Haaa kuna kipindi nilikwenda Tabora maeneo ya stand kulikuwa na Mbuzi wanaranda randa wanajua kukwepa magari tena wanene kweli nikamuuliza mwenyeji wangu akaniambia hawa mbuzi hawana mwenyewe ukijaribu kumchukua kamwe huwezi kumchinja.Kuna Mchagga mmoja alijaribu kesho yake asubuhi na mapema akamreshesha mwenyewe bila kupenda.
Ukiamini ushirikina hata kivuli chako mwenyewe unaweza kukiogopa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom