lackg
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 641
- 268
Nichukue nafasi hii kumuomba mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni naibu waziri wa ardhi Ndg Angeline Mabulla, kuwa wapiga kura wako wa kata ya Shibula kutoka mitaa mitano ya Monze B, Nyamwilolelwa, Kihili, Shubula na Bulyanghulu wanataka kuporwa maeneo yao na uwanja wa ndege jijini Mwanza. Mgogoro huu umeanza mwanzoni mwa mwaka huu lakini umekua ukikua kila kukicha baada ya watu wa uwanja wa ndege kupitisha mpaka na kuweka alama kwenye nyumba za wakazi wa eneo lisilo la uwanja bila taarifa kwa wananchi.