Kajuni
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 483
- 186
Huu ni uzi wa wazi kabisa kwa mbunge wangu John Myika John.
Mheshimiwa hiki ni kipindi chako cha pili ukiwa mbunge wa Ubungo na sasa Kibamba. Kwa mujibu wa eneo lako la utawala Msumi A na B ni maeneo yako. Napenda kukutanabaisha ya kwamba miaka mitano Imepita lakini shida Ulizotukuta nazo ni zile zile.
Maji bado ni tatizo kubwa sana. Ni aibu kuona bomba la maji kutoka Ruvu linapita na kupeleka maji kwingineko lakini cha ajabu maji ni tatizo kubwa. Wakina mama wanateseka, wanabeba maji kichwani kutoka mbali japokuwa wapo kilometer 24 kutoka Ikulu ya Magogoni. Tunakuomba ututanyie haraka tupate maji kama binadamu wengine. Fikiria ndoo moja ya lita 20 ni Shilingi 200 kwa usawa huu tunafika?
Tatizo lingine kubwa ni Umeme. Nimejaribu kukutafuta kupitia mtandao kwa kuandika barua pepe kadhaa lakini majibu yamekuwa kimya. Wananchi bado wanaimani kubwa na wewe please timiza wajibu wako lasivyo hakuna atakaye linda kura ifikapo 2020.
Barabara nalo limekuwa tatizo kubwa wenzetu tunaona Kila siku zinakwanguliwa lakini huku kwetu bado majanga. ulituaidi lami ndani ya mwezi mmoja!! Pengine ilikuwa janja ya Kupata kura kama sio kula. Basi umefanikiwa nasi tupatie maendeleo.
Mwisho kabisa kwa utafiti nilifanya viwanja vingi havijapimwa hasa huku mashambani kwetu so tunakuomba walete wataalamu watupimie kwa bei nafuu kwani kwa sasa kiwango cha chini ni takriban million tano.
Jamani kama mwananchi mkereketwa wa Jimbo la Kibamba nimejipa kazi ya Miaka mitano ya kulala na Mbunge wangu mchana na usiku. Na nitahakikisha na mkumbusha kuteleleza wajibu wake. Sio majungu ni kweli Mbunge wangu ni kama kazi imemshinda miaka mitano iliyo pita na sasa tumempatia awamu ya pili ya lala salama. Kama hatafanyakitu asitegemee kutuongoza tena. Aende huko akaimarishe chama.
Wako mpiga kura wako mtiifu Msumi.

Last edited: