Mbunge Waitara awatembelea wakazi wa Bonde la Msimbazi katika Kata za Ukonga, Gongolamboto na Pugu

JUkonga

Member
Dec 30, 2015
14
13
Leo nitakuwa katika Kata ya Ukonga mtaa wa Mongolandege ambako jana wakazi wake walianza kuwekewa alama ya X kwenye nyumba zao. Nitazungumza na wakazi wote ambao nyumba zao zimewekewa alama ya X tayari kwa kubomolewa na baada ya hapo tayari tumeshapata mwanasheria kwa ajili ya kuchukua hatua stahili za kisheria.

Msimamo wangu kama mbunge kwenye kadhia hii ya wakazi mambondeni uko wazi kabisa, wakazi hawa waliuziwa haya maeneo kihalali na serikali inajua tangu wakati wanauziwa, baadaye wanaanza kujenga na kuanza kuishi maeneo hayo na serikali kupeleka huduma za jamii kama umeme na Maji.
Mbaya Zaidi ni wananchi hao wa mabondeni wengine wana hati za makazi na wanalipia kodi ya majengo kunahalalisha wananchi hao wanaishi maeneo hayo kihalali.
Tunachokitaka ni serikali kutumia busara kwenye jambo hili, lazima ubinadamu utumike pia, mfano katika hizo nyumba za mabondeni zinazotakiwa kubomolewa kuna watoto wadogo, wazee, wagonjwa, yatima na wajane hawa wote wanahitaji serikali kulinda haki yao ya kuishi.

Kuna swala la haki za binadamu, haki ya watoto hawa, wazee na wagonjwa lazima ilindwe kwa gharama yeyote.
 
Back
Top Bottom