Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
I agree! Na hilo ni iwapo kutajitokeza wagombea wengi. Lakini kama atajitokeza mmoja kama ambavyo mara nyingi huwa inakuwa, basi haitakuwa shida kusema fulani endelea.
Kamanda Lukolo mimi nipo Mongolandege.
Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa kama kuna mambo umejaribu kumtumia yakafanikiwa basi una bahati nzuri.
Mimi niliwahi kumfuatilia sana kuhusu ufunguzi wa zahanati ya Mongolandege, ambayo ujenzi wake ulikamilika mwishoni mwa mwaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu lakini haukuwahi kutoa huduma kwa takribani mwaka mzima hadi pale wananchi walipopiga kelele sana.
Baada ya kubana nae, nakumbuka alinijibu siku moja kuwa kuendesha manispaa kubwa kama ilala ni sawa na kuendesha meli, kwakweli nilicheka tu kimya kimya. Nikajiuliza kama Jery alikuwa anatambua ukubwa na uzito wa kazi ya umeya aliyokuwa anaililia.
Anyway, hata hivyo zahanati imefunguliwa mwaka jana, ingawa haina vifaa tiba, wameleta wauguzi na manesi kama watatu au wanne ambao wanatibu kwa "kupiga ramli" kwakuwa hakuna kifaa chochote cha kufanyia kipimo, hata kipimo cha maleria hakuna. Na kichekesho zaidi ni kwamba zahanati hiyo inafunguliwa Jumatatu hadi Jumamosi, na siku za Jumapili inafungwa!!! Sasa jiulize kama jumapili watu hawaumwi ama hawahitaji matibabu???... eti meya aliyeshindwa kazi naye anafanya kampeni za kutaka kuwa mbunge.
Btw, tutafutane weekend moja tuone ni namna gani tunaweza kuunganisha nguvu na viongozi wa Chadema jimbo la Ukonga ili tuhakikishe kuwa 2015 hatupotezi jimbo kwa kuliacha kwa wauza sura wa magamba, ambao wamethibitika pasipo shaka kuwa hawawezi kutukwamua kamwe.
Ama hivi Ukonga ni Jimbo? Miye nikadhani lilibadilishwa jina kuwa Segerea.....ni taabu sana kuwa na jimbo lina jina la gereza aisee
Nimekua ukonga tangu 80s hili jimbo letu halijawahi kuwa na mbunge makini hata siku moja tangu enzi za Rupia hadi sasahivi chondechonde 2015 tusirudie makosa
Mkuu Lukolo demokrasia ndani ya chama chetu ndiyo itakayoamua nani atapeperusha bendera yetu mwaka 2015.
Mkuu Safari_ni_Safari tafadhali tuheshimiane kidogo.
Sasa mbona unalifananisha jimbo la Ukonga na Segerea ambayo yote yanatumia majina ya magereza!!? au ndio sababu ya kukosa mwakilishi makini? au wananchi wake wanajiona kama vile wako maagereza wamefungwa...???
Huyu ni Mwita Maranya ni huyu aliyekuwa mwenyekiti wa FOS?baadae akawa raisi wa DARUSO?any way awe yeye au siyo yeye nitamuunga mkono kwenye mchakato,yaani ile barabara jamani mvua zikinyesha haipitiki,kitunda yetu jamani tutaindeleza sisi yenyewe.Tumpe Mwita Maranya, kama hatakuwa tayari; basi mimi nitagombea kwa tiketi ya CHADEMA.
Ama hivi Ukonga ni Jimbo? Miye nikadhani lilibadilishwa jina kuwa Segerea.....ni taabu sana kuwa na jimbo lina jina la gereza aisee
leo utakuwa umevuta,huandikagi ujinga kama huu!kwani segerea hamna gereza?umenishangaza kweli!au unatania?
Mkuu mimi pia ni mkazi wa ukonga,na nimetamani siku nyingi sana kupata watu wa kusaidiana nao,kuhakikisha 2015 tunamsimamisha mtu makini kuchukua hili jimbo,na jinsi huyu mama alivyo unga hata 2010 kama chadema tungekuwa makini tungechukuwa jimbo,naomba kwenye hicho kikao mkakati nishirikishwe na tena kisichelewe,kamanda Mwita vipi watu wanakutaka ugombee,jimbo jeupe hili.
Mkuu nisamehe bure.....niliangalia kwa context hiyo tu ya majina ya magereza.....no disrespect to anyone....hivi kuna jimbo la Keko?
leo utakuwa umevuta,huandikagi ujinga kama huu!kwani segerea hamna gereza?umenishangaza kweli!au unatania?
Huyu ni Mwita Maranya ni huyu aliyekuwa mwenyekiti wa FOS?baadae akawa raisi wa DARUSO?any way awe yeye au siyo yeye nitamuunga mkono kwenye mchakato,yaani ile barabara jamani mvua zikinyesha haipitiki,kitunda yetu jamani tutaindeleza sisi yenyewe.
wow! good news. Sikujua kabisa kama kuna list kubwa kiasi hicho. Inapendeza na inatia moyo sana mkuu. Thanks kwa info hii.Mkuu nachotaka kukuhakikishia ni kwamba mwaka 2015 Ukonga litakuwa ni mojawapo ya majimbo yatakayokuwa na mchuano mkali ndani ya chama chetu. So far kuna watu sita wameshatangaza waziwazi nia ya kuutaka ubunge wa Ukonga, hadi kufikia mwaka kesho naamini list itakuwa ni ndefu kweli kweli.
Muhimu ni sisi wenyewe tu kujipanga jimbo hili ni letu kabisa. Ukirudi tutafutane mkuu.
Wazo la msingi sana hili. Nafikiri Mwita Maranya ataweza kuunganisha nguvu na uongozi wa CDM Ukonga ili mikakati ianze.Nimekuelewa kamanda,ombi moja kimbunga cha M4C Ukonga vipi hakiwapitii magamba,hebu nahuku kazi ianze mapema.