Mbunge wa Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea anasema hawezi kuhamia CCM. Na zaidi ametoa kauli zinazoonesha kuwa anapigwa majungu ndani ya Chadema.

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Mbunge wa Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea anasema hawezi kuhamia CCM. Na zaidi ametoa kauli zinazoonesha kuwa anapigwa majungu ndani ya Chadema.
Sababu za Saed Kubenea za kutohamia CCM sio sababu nzito. Anasema ametibiwa nje ya nchi mara kadhaa bila gharama za serikali. Na ameomba kutibiwa macho nje ya nchi, amekataliwa. Kwa hivyo hawezi kuhamia CCM.

Sitagusia mkanganyiko huu wa Serikali vs CCM lakini najua Humphrey Polepole sasa ameshaona 'loop hole' kupitia changamoto za Mh. Kubenea. Bila shaka Polepole na timu yake watazifanyia kazi changamoto za mheshimiwa Kubenea ili Mh. aunge mkono juhudi.

Pamoja na hayo, Chadema inahitaji kujitathmini. Inaonekana wazi kuna viongozi na maofisa wengi ndani ya chama wasiojua dhumuni la Chadema. Mbunge anapotoa sababu za kutohamia CCM kama hizo, sio ishara nzuri.
Chadema ni chama chenye itikadi zake, na malengo yake ya kisiasa. Sasa unapokuwa mwanaChadema lazima ujue madhumuni ya chama, yanayoendana na itikadi zake. Unapokuwa MwanaChadema kwa sababu za kiitikadi, huwezi kuhama hadi pale Chadema itakapobadili itikadi hizo, au miiko yake, au malengo yake. Si kwa kusaidiwa au kutosaidiwa na serikali ya/au CCM.

Wanaosubiri msaada wa serikali ya CCM kama kigezo cha kuhamia huko, wamtafute Humphrey Polepole awasaidie.

Kuhusu taarifa za Mh. Kubenea kupigwa majungu ndani ya chama, si taarifa za kupuuza. Kwanza hadi kusema hadharani ni ishara kwamba amezidiwa. Ndani ya Chadema, kama CCM siasa za majungu hazihepukiki isipokuwa zitakuwa na viwango tofauti. Wengi waliopo Chadema ni wanasiasa wa kitanzania kama waliopo CCM, tofauti ni akina Tundu Lissu na baadhi wachache. Kubenea aamue kupambana ndani ya Chadema au ahamie CCM, atajua mwenyewe.
Bado tuwasikie akina Anthony Komu na Joshua Nassari, na wengine wanaotajwa kutaka kuhama.
A. Komu ni mtu mzima, pengine malengo yake ya baadae ndio haya ya sasa. Joshua Nassari ni kijana, aangalie kinachofaa. Na kwakuwa bado ana safari ndefu, kinachofaa sasa kinaweza kisifae kesho.

mr mkiki.
 
Naye aende akitaka..... Nyie majamaa vipi?
Chadema ijitafakari vip kama mkiona mnashindwa mnaua watu.....
 
Naye aende akitaka..... Nyie majamaa vipi?
Chadema ijitafakari vip kama mkiona mnashindwa mnaua watu.....
Sawa inawezekana kurudi Chama kimoja . Lakini chama chenyewe kisiwe ccm hawana jipya. Afadhali tusiwe na chama Jeshi watawale kuliko ccm !
 
Back
Top Bottom