Mbunge wa Ubungo John Mnyika aishukia serikali

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Ikiwa leo ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) ameitaka serikali kutumia siku hiyo kutoa taarifa za kina kuhusu utatuzi wa kero ya maji kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam. Mnyika alisema Rais Jakaya kikwete, atumie siku hiyo kutoa kauli kuhusu utekelezaji wa ahadi mbalimbali za kuboresha huduma ya maji na kwamba kinyume chake itaunganishwa nguvu ya umma katika kuchukuwa hatua za ziada kukabiliana na kero husika. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mnyika ilieleza kuwa licha ya serikali kutoa ahadi mbalimbali za kuboresha na kutokomeza kero ya maji jijini, lakini zimekuwa hazitekelezwi.
Mwananchi Machi 22 2011
 
Wabaneni mbavu hivyo hivyo Viongozi wachovu hadi wakose muda wa kuchakachua, muda wote wahisi wanaonwa, wakija kutahamaki 2015 hiyoooooooooooooooooooooooooo AIBU YAO
 
Wabaneni mbavu hivyo hivyo Viongozi wachovu hadi wakose muda wa kuchakachua, muda wote wahisi wanaonwa, wakija kutahamaki 2015 hiyoooooooooooooooooooooooooo AIBU YAO

hapa kuna point. Cdm mmebana mpaka muda wa kufisadi unakuwa issue bwn!dah!sasa uongozi umekuwa shubiri!
 
Kwa hili lla maji inabidi niongee.
Ndugu Mnyika,
Tafadhali tumia muda huu wa wiki za maji au nyinginezo kutuma ujumbe wa ahadi zilipofikia (kwa mtazamo wako) Kuwasubiri haitakuwa tofauti.
Sie tunataka kuhama huku kwa ajili ya shida ya maji ambayo haina kichwa wala mguu.
Inakuwaje bomba linapita hapa mbezi, hatuna maji, lakini watu wa huko mbali wananyeshea ukoka?????
Yani mie nadhani utapita muda mfupi nitamchanganya mbunge wetu na diwani kati ya kundi la mafisadi.

Mie sielewi kabisa ugumu uko wapi katika kuwapa maji watu wa mbezi Luis 1km kutoka bomba kuu!!!

Mnyika unataka uwe waziri wa maji ndio maji yatoke huku?
au siasa na wewe zimekushinda??
 
hee makubwaa! Ila kwawakilisha watanzania sio kazi ndogo aisee! Watu wenye njaa na dhiki, halafu wagonjwa(ona loliondo), halafu shule adimu, halafu less or mis-informed, halafu siasa chafu.....hebu nichanganyie hapo kisha niambie unapata nini. Pole Mnyika, wapo pia wanaokuelewa usjali!

Back
Top Bottom