Mbunge wa Tarime na mgogoro wa Nyamongo

Amedai wabunge toka kwenye majimbo mengine waombe ruhusu ya kuzuru kwenye majimbo mengine kupitia mbunge wa Jimbo husika. Hapa nahisi alikuwa anawasema Lisu na Lema kwamba waombe ruhusa yake kuzuru Tarime! Kwa maelezo yake ni kwamba alikuwa anaomba ushirikiano na Wanatarime kwa kuwa wanaipenda CCM na serikali iliyopo madarakani ila anasikitika kuna wahuni wachache wanatumiwa na vyama vingine kuvuruga mambo huko Tarime; akaongeza pia kuwa Wanatarime wamechoka na hali hii wanataka watulie wafanye kazi za kujiletea maendeleo. Nimkumbushe tu Mh. Nyambari wakati yeye anauza vitabu Lisu alikuwa na Wanatarime kwenya matatizo mbali mbali ya Migodi ya Tarime toka Buhemba na sasa chini ya Barrick. Lisu amejijengea imani kwa Wanatarime na wanamhesabu si kama mtetezi wao bali kama ndugu yao. Taarifa nilizonazo ni kwamba wakati wa msiba wa mama yake Lisu kulikuwa na watu zaidi ya ishirini toka Tarime walioshiriki kwenye msiba huko Singida. Sasa kwa hali hii Lisu asikie kuna maafa yamefanyika Tarime asiende aombe hurusa toka kwa wewe Nyambari??? Joandae Kukabidhi Jimbo maana umewakimbia wananchi wakati wakikuhitaji!!
 
maskini hata Nyambari Nyangwine hajui kuongea.
..

Hapo kweli umenena, Thomas, mimi namwita Thomas hayo ya Nyambari sijui Nyanguinini yake. Yule jamaa hajui kuongea na hajui la kuongea. Huwezi amini alipokuwa mwanafunzi pale UDSM alikuwa anaongozana na jamaa fulani wakali, wanamsaidia kila kitu, kuandika notes, kuwa nao katika Take Home Essay, Kufanya presentation, katika presentation yeye kazi yake ilikuwa kutafuta viti vya kukalia kule mbele, kuandika introduction ubaoni na kufuta ubao, wakali wake alikuwa akiwanunulia RnB (Rice and Beans) wanamfanyia kila kitu. Sijui kwa nini hayuko na wale wasaidizi wake labda wangemsaidia, yeye mwenyewe mwizi balaa. Halafu jamaa kwa kuchakachua vitabu vya watu, jamaa hatari, nahisi hata kule mgodini nae anatamani kwenda kuchoropoa mawe kadhaa. Polisi waanze kumkamata yeye na kesi zake lukuki kule Central polisi na COSOTA.
 
icon1.png
Matusi Redioni


Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi Clouds Fm, Kibonde, Kayanda na Wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa ATC, mjadala umeenda vizuri japo Kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, Hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....Clouds FM imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.


Usishangane, ndo matatizo ya kujiona kuwa wewe upo sawa kila wakati na unaongea ukweli tu. Unapokuwa hupati upinzani katika mazungumzo yako unafikia hatua unaropoka hata yale yasiyokuwapo. Tatizo la maneno, ukishaongea hayarudi tena, iliyopo ni kuomba radhi.
Shame on you Kibonde na kujikomba kwako, hivi kwani hata ukatibu tarafa hajapewa tuu, maana yeye na JK, JK ni zaidi ya Mungu kwake.
 
kumbe hajui anafanya nini bungeni?
kwani sheria wanazo tunga ni za jimbo?
clouds fm iko kinondoni,yeye pale sio mbunge,anafanya nini huku dar?
mbweha mkubwa

Speaker hujui kuwa wale hawachaguliwi majimboni? Wao wanakuja kuchakachua huku NEC yao. Wapiga kura wake wapo huku, kule hawakupigiwa ndo maana wanakukimbia. Na akienda tena watampopotoa tuu!
 
quote_icon.png
Originally Posted by matola
icon1.png
matusi redioni
leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi clouds fm, kibonde, kayanda na wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa atc, mjadala umeenda vizuri japo kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....clouds fm imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.
nilimsikia! Kweli kabisa alitoa hilo tusi.

Hata mimi nilisikia halafu wakalipotezeakwa kurudia ........nenda kafanye kazi kwa mama yako......wakizuga kama ndokasema hivyo.
 
icon1.png
Matusi Redioni


Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi Clouds Fm, Kibonde, Kayanda na Wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa ATC, mjadala umeenda vizuri japo Kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, Hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....Clouds FM imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.

Nilikuwa nasikiliza. Nakumbuka kama alisema 'kudadadeki' unless kama sikusikia vizuri. Kama kuna wengine walisikia vizuri humu jamvini watuambie.
 
Nilikuwa nasikiliza. Nakumbuka kama alisema 'kudadadeki' unless kama sikusikia vizuri. Kama kuna wengine walisikia vizuri humu jamvini watuambie.

Inatosha tu kujua kuwa alitoa matusi makubwa ya nguoni. Hakuna haja ya kuyaanika humu jamvini, kwani kibonde anajulikana kuwa ana matatizo.
 
Kama anatangaza matatizo anayokutana nayo ktk utendaji wake akiwa ni mbunge, na kama anatangaza sasa kuwa hawezi kusolve peke yake mpaka asaidiwe na serikali kwa maana ya Polisi, basi aachie ngazi tu. Awaachie wanaoweza. Sio ujinga kuanza upya. Mbunge gani huyo asiye na uhuru wa kutembelea jimbo lake mpaka apate escort ya Polisi?
 
Nyambari, siasa haimfai bora aachane nayo yeye aendelee kututungia na kuchapisha vitabu kwa ajili ya wanafunzi wa Secondary !
 
Mbunge unatia aibu unashindwa hata kutumia hata sekunde moja kutoa salamu tu za pole kwa wafiwa na wananchi wako walioumia bila sababu ktk sakata hili unaonekana kuzungumzia kuchukua hatua kuwalinda wawekezaji je vipi kuhusu wananchi wako waliokupa kazi ?? Wewe ni mbunge wa wawekezaji au wa watu wa tarime ??. Inaelekea hata katiba huijui bila hivyo usingezungumzia issue ya kutunga sheria watu wasiende jimboni mwako.
 
Back
Top Bottom